Social Icons

Tuesday, August 31, 2010

SHEILA OUT!!

BAADA ya Jumamosi kujirusha vilivyo kwa magoma ya ukweli yaliyokuwa yakisababishwa na Dj Steve B kutoka Tanzania, mwakilishi wa Kenya katika Mjengo wa BBA ‘All Stars’, Sheila Kwamboka wa Kenya, Jumapili naye alioneshwa mlango wa kutokea.
Sheila na Munya walikuwa wakipigiwa kura ya nani abaki mjengoni ambapo kwa bahati mbaya kura za Sheila zilishindwa kutosha na kujikuta akimwaga chozi kabla ya kwenda kuungana na wenzake katika Jumba la Big Brother Barn.
Sheila ambaye amechafuka kwa kuhusishwa na soo la usagaji mjengoni humo akiwa na Merly, sasa atakuwa ‘vere klozi’ na Tatiana Durao wa Angola ambaye naye ana ‘elementi’ za usagaji.

DJ FETTY MWOGA BALAA!!!!

MTANGAZAJI First Class wa redio ya watu Clouds Fatma Hassan 'DJ Fetty' ameonyesha fearness ya aina yake, hebu cheki hii:saa 03:50 usiku hivi,nimeshtuka kuna mtu kama anakata nyavu ya dirisha langu kiaina, yaani nashindwa hata kuhema kwa woga. In case of anything , haya ndiyo maandishi yangu ya mwisho God help me.

NANI KUWAKILISHA TUZO ZA MTV?

WAKATI event ya utoaji wa Tuzo za MTV Africa Music Awards (MAMA) ikitarajiwa kufanyika Desemba 11, mwaka huu Lagos Nigeria, wabongo bado wana shauku kubwa ya kumfahamu msanii atakayenyanyua Bendera ya TZ pande hizo.
Mwaka jana, Ambwene Yessaya ‘A.Y’ na Sarah Kaisi ‘Shaa’ waliiwakilisha Bongo vyema, mwaka huu bado mwakilishi hajatajwa.
Tuzo hizo zilizodhaminiwa na MTV kwa kushirikiana na Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel (Zain kwa Tanzania), zitachukua nafasi katika Ukumbi wa EKO EXPO Hall, jijini Lagos, hii ikiwa ni mara ya tatu kwa tuzo hizo kufanyika barani Afrika.
Kwa mara ya kwanza Tuzo za MAMA zilizinduliwa Velodrome, Abuja nchini Nigeria mwaka 2008, na mwaka 2009 zikafanyikia Nairobi, Kenya. Wasanii waliowahi kunyakua tuzo hizo

NYOSH 'FULL' SHAVU

‘PREZI DAA’ wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Nyoshi El- Saadat hatimaye ameendelea kuboresha afya yake ambapo sasa ni ‘full shavu’ kutokana na uzito wake kuongezeka na kuwa wa kawaida. Nyoshi alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kupungua uzito na kudhoofika kwa muda mrefu, lakini sasa yuko njema.
Akichonga na Mateja20,hivi karibuni, Nyoshi alisema kwamba kwa hivi sasa amekuwa akila vyakula kwa mpangilio maalum ili kuondoa tatizo la kupungua uzito lililokuwa linamnyemelea, hali iliyosababisha afya yake kurudi kwenye ‘mstari’ kwa haraka, huku akipiga mazoezi ya nguvu ili kujenga mwili.
Nyoshi aliiambia Mateja20 kwamba, kitu kingine kilichofanya afya yake kuzidi kuwa bora, ni pamoja na mipango mizuri ya bendi yao, kwani hapo awali alikuwa akipungua uzito kutokana na msongo wa mawazo uliokuwa unamkabili wakati akiumiza kichwa jinsi ya kuinua bendi yake.
Aidha Nyoshi aliweka wazi kwamba katika mchakato wa kurekebisha bendi yao, tayari wameshaseti mambo na kilichobaki ni uzinduzi wa albamu yao mpya inayokwenda kwa jina la Vuta Nikuvute Mathematics 'Mayemba', na kwamba wanatarajia kuizindua albamu hiyo yenye jumla ya nyimbo 12 siku ya Idd Mosi, ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.



RAMADHANI YAMTAMANISHA JOAN!!!

KUFUATIA kuendelea na Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa Waislamu, muigizaji wa filamu na muaandaji wa Script Bongo, Joan Matovolwa amepata mchecheto wa kuwasindikiza Waislamu kwa kufunga siku moja moja.
Akipiga Stori na Mateja20, Joan alisema kuwa, mwezi huu ni wa Waislamu japokuwa yeye ni Mkristo anajaribu siku moja moja kufunga kwani hata siku ikifika ya Wakristo kufunga huwa haimpi shida kwani anakuwa ameshazoea kulidhibiti tumbo lake.
Aidha, alifafanua kuwa pindi anapokuwa kwenye mfungo, kitu kikubwa anachopendelea kufuturu ni uji kwani anaupenda sana kuliko hata futari inavyopikwa na ndiyo maana muda ukifika wa kufuturu huwa anakimbilia kikombe cha uji.
“Mimi ni Mkristo, ila ninauheshimu mwezi huu wa Mfungo wa Ramadhani kuliko kitu kingine na ndiyo maana siku moja moja huwa nawasindikiza Waislamu kufunga,” alisema Joan.



Monday, August 30, 2010

BURUDANI MIX

Align CenterLulu Mathias akiwa kwenye pozi muda mfupi baada ya kutoka kuangalia burudani ya Twanga Pepeta ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar, hivi karibuni.
Rapa tegemezi wa African Stars International, 'Fagason' akijaribu kucheza staili ya kubebwa mgogongoni na mmoja wa mashabiki wake.
Mnenguaji wa Bendi ya FM Academia (Alia) akiawajibika jukwaani ndani ya Ukumbi wa Mbalamwezi Beach usiku wa kuamkia leo.
Alia na sitaili ya 'Bodaboda gooo'
Huyu naye ni mnenguaji wa Fm Academia 'Wazee wa Ngwasuma' akitetea kazi yake.

Saturday, August 28, 2010

SITAKI NATAKA BABU WEEE!

'Nitakunaniliiii......

FUTARI ..... BENNY KINYAIYA!!!

MTANGAZAJI wa Shirika la Habari la Taifa, TBC1 kupitia Kipindi cha B&M, na mkurugenzi wa Kinyaiya Pub iliyopo Kinondoni nyuma ya Ukumbi wa Mango Garden Benny Kinyaiya juzikati nusura yamkute ya kumkuta baada ya kufakamia futari kwa pupa na kujikuta akiungua mdomo.
Ishu hiyo ilitokea katika Ofisi za Clouds Entertainment zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na uzinduzi wa kipindi cha Televisheni ya Clouds kiitwacho Take One uliokwenda sambamba na kuwafuturisha watu mbalimbali.
Akiwa miongoni mwa wageni waalikwa, Benny alinaswa akiwa ameshikilia sahani iliyokuwa imesheheni futari huku akionekana kama aliyekuwa na ‘ubao’ mkali.
Paparazi wetu wa Mateja20 aliendelea kumtolea macho kwa mbali akijua chochote kingeweza kutokea kwa staa huyo na ghafla aliinuka na kutoka nje huku akiwa ameshikilia mdomo wake.
Taarifa iliyopatikana baadae ilidai kuwa, kilichomfanya staa huyo atoke nje ni kwenda kujipatia huduma ya kwanza baada ya kuungua mdomo kwa futari.
Akiongea na Mateja20 Benny alisema: “Ni kweli nimeungua mdomo lakini pia kuna kitu kimenikwama ambacho nahisi ni mfupa, sijui nina balaa gani. Hata hivyo najisikia freshi kidogo baada ya kunywa kama maji hivi' Alimalizia kwa kusema hivyo mkurugenzi wa Kinyaiya Pub.



B.BENDI NA SWAGGER ZA MASHABIKI!!!

MZEE Zahir Ally Zorro akiwajibika jukwaani usiku wa kuamkia leo ndani ya Ukumbi wa Thai Villager Masaki jijini Dar, ambapo bendi hiyo ilikuwa ikifanya makamuzi yake

Mmoja wa waimbaji wa bendi hiyo akifanya makamuzi.
Baadhi ya Mashabiki wa bendi hiyo wakiwa katika pozi.
Haa! mambo haya yanapatikana katika onesho la B.bendi baana!!!
Shumileta akiwa kwenye pozi na Zamda ndani ya Thai Village Masaki jijini Dar.
















Friday, August 27, 2010

LIL KIM ASAMBALATISHA NDOA YA MSHIKAJI DAR!!

WAKATI bado ‘memori’ ya shoo ‘hevi’ iliyoangushwa na staa wa muziki kutoka nchini Marekani, Kimbely Denise Jones ‘Lil Kmi’ katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar wiki tatu zilizopita haijafutika, imedaiwa kuwa ujio wa nyota huyo umeipasua ndoa ya Hussein Nazir ’Pacha’ (25) na Shamsa Habib (22), wakazi wa Ilala.
Chanzo makini cha Ijumaa kilitonya kwamba, mapema baada ya Lil Kim kuondoka Bongo, gogoro kubwa liliibuka ndani ya familia hiyo baada ya mke, kunasa picha zinazomuonesha ‘my hazibendi’ wake akiwa amemkumbatia kimahaba mwanamuziki huyo wakiwa stejini.
Baada ya kuinyaka ishu hiyo kutoka kwa chanzo hicho makini, Mtandao bora wa Burudani Bongo, Mateja20 ulifunga safari hadi ofisini kwa mwanamke huyo ndani ya Mjengo wa Mliman City, Dar na kukutana naye ambapo bila kujali vituo wala koma, aliweka wazi dukuduku alilonalo kwa laazizi wake lililomfanya kuchukua uamuzi wa kufungasha virago na kurudi kwao.
Shamsa ambaye ndoa yake imetoa uzao wa watoto wawili, wa kike na kiume, alisema: “Ukweli ni kwamba nilipoziona picha za mume wangu akiwa amekumbatiana na Lil Kim, nilihisi uchungu moyoni kwakuwa nampenda sana.
“Nilimshaanga sana mume wangu kwenda kufanya jambo lile na kukata mauno mbele ya ‘kadamnasi’ huku tukiwa katika maandalizi ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.”
Katika hatua nyingine, Shamsa, mwenye asili ya Kiarabu aliongeza kwamba, siku zote amekuwa na nidhamu ya kutosha kwa mwenza wake huyo katika kuhakikisha ndoa yao inakuwa salama na yenye amani lakini kitendo hicho kilimkosesha raha na kuhisi kuna matukio mengi ya aina hiyo yanampita hivyo kunusa harufu ya usaliti kwa mumewe.
“Pamoja na kuniomba msamaha, bado jambo hilo linaniumiza moyo kwani hata siku moja sikutarajia mume wangu angefanya kitendo kama kile,” alisema Shamsa na kuongeza:
“Mbaya zaidi alinidanganya anakwenda kwenye biashara zake na hakutaka tuambatane, binafsi picha hizo nimeziona na kiukweli nimechukia sana.”
Hata hivyo, kwa mujibu wa wadau walioongea na Ijumaa, mwanamke huyo alitakiwa kuondoa shitaka moja la kukumbatiana na Lil Kim kwani ni jambo la kawaida kwa mashabiki kuserebuka na kupiga picha na msanii wa kimataifa kama huyo.
Wadau hao walimtaka Shamsa kushikilia shitaka moja la mumewe ‘kumchiti’ kuwa anakwenda kwenye biashara wakati alikuwa anakwenda kujirusha.
Kwa upande wake, Pacha, mbele ya Ijumaa nyumbani kwa familia yake Mtaa wa Sadani, Ilala Dar alikiri kutokea kwa ‘gogoro’ zito kati yake na mzazi mwenzake.
“Ni kweli ujio wa Lil Kim umeniachia machungu kwenye ndoa yangu,” alisema Pacha na kuongeza: “Nimejitahidi kuomba msamaha lakini nimeambulia patupu labda mnisaidie kuniuombea msamaha. Bado sijakata tamaa na nikifanikiwa nitawaambia.”


IRENE AMSALITI MMEWE!!!

Irene Uwoya katika pozi na Diamond
MUIGIZAJI
‘high level’ katika kiwanda cha filamu Bongo, Irene Uwoya ‘Oprah’, alijikuta akifanya kile kilichotajwa kuwa ni kumsaliti mumewe, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ baada ya kukutwa akijiachia klabu usiku wakati mwenza wake huyo huwa hapendi.

Irene alinaswa Jumatano ya wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Club Bilicanas uliopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam akisugua kisigino wakati Bendi ya muziki wa dansi nchini, African Stars International ‘Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani’ ilipokuwa ikiporomosha burudani zake kama kawa.
Awali, mwanadada huyo mkali katika kuigiza ‘scene’ za kimapenzi katika filamu mbalimbali alionekana akikatiza ukumbini humo huku akiwa ametinga nguo zilizoonesha kuwa ni shabiki pure wa Timu ya Yanga.
Katika kuweka kumbukumbu vizuri, Mateja20 alimfuata kwa lengo la kutaka ‘kumfotoa’ lakini tofauti na ilivyotarajiwa, Irene aligoma kukaa mbele ya kamera kwa maelezo kuwa, zikitoka picha kwenye gazeti zinazomuonesha yuko klabu atamkwaza ‘mai hazbandi’ wake.
“Picha hiyo itakuwa na madhara kwenye ndoa yangu ikiwa mume wangu atagundua kuwa nimekuja huku Club wakati huwa hapendi hasa niwapo Bongo kujichanganya pande hizi, nimekuja kiubishi ubishi tu,” alisema Irene huku akiwaagiza wapambe wake kuhakikisha hapigwi picha mpaka anaondoka .
Mateja20 ambaye hakutaka kuleta mazingira ya shari ukumbini hapo aliamua kuwa mpole lakini akimshuhudia mrembo huyo akiwa amekosa amani.
Irene ameshakwea pipa kuelekea nchini Cyprus kwa mumewe baada ya kuwepo Bongo kwa siku kadhaa katika mapumziko mafupi.

LINAH WA THT AKILI KUTOA PENZI KWA AMINI!!

STAA chipukizi katika gemu ya Muziki wa kizazi kipya Bongo, Estalinah Sanga ‘Linah’ anayeiwakilisha ‘gemu’ kutoka nyumba ya vipaji THT amemuanika mtu anaye vunja naye amri ya sita na kuzima minongo’no iliyoenea mtaani kuwa anatoka na nguli wa hip hop nchini Ibrahimu Musa ‘Roma’

Linah anayetamba kwenye chati za Bongo Fleva hivi sasa na ngoma ya ‘Wrong number’ aliyomshirikisha Barnaba ameliambia Ijumaa kuwa, ameamua kuweka kila kitu wazi ili kuepuka maneno ya watu ambao anahisi wanataka kuharibu uhusiano wake.

“Nimesikitishwa na taarifa za kuwa mimi natoka na Roma, huo ni uzushi kwani Roma ni shemeji yangu na kila anaye fahamu ukweli anajua kuwa mtu wangu ni Amini Mwinyimkuu yule aliyeimba wimbo maarufu wa Bado Robo saa,” alisema Linah.

Nyota huyo alitanabaisha kuwa, anampenda Amini kuliko kitu kingine chochote hivyo hafikirii kufanya jambo lolote ambalo litatishia uhai wa uhusiano wao mpaka mpango na hadi yao ya kufunga ndoa itakapotimia.





Thursday, August 26, 2010

MAMBO YA FASHION BAANA!!!!!

MREMBO anakwenda kwa jina la Regina Mponi, ni mmoja wa ma-Actor wa movie za kibongo hapa nchini, upande mwingine ni Manager Director wa C & R B0utique iliyopo Sinza Kumekucha jijini Dar es Salaam.

Regina katika Pozi.
Hapa kila jambo linawezekana.
Kama model vile!!!
Siyo hudhuni ila ni moja ya pozi zake!!!!
Mpango mzima uko hivi!!
Mambo ya kiofisi zaidi.
Hata za Club zipo!

KIMOBITEL ACHEZEA VIGANJA!!!

First Lady wa Bendi ya Extra Bongo next level ‘Wazee wa kujinafasi’, Khadija Mnoga ‘Kimobitel’, amepigwa makofi na mwimbaji mwenzake.
Kimobitel, alipewa kisago na Bob Kisa hivi karibuni huku chanzo kikitajwa kwamba ni Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Bob Kisa alimkung’uta Kimobitel makofi kwenye Ukumbi wa Nanenane, Morogoro kwa maelezo kwamba alimsema vibaya Mzee wa Farasi wakati hayupo.
Chanzo chetu kilisema na baadaye kuthibitishwa na Bob Kisa kuwa wakiwa nje ya ukumbi huo baada ya shoo, Kimobitel alianza kuchonga kuhusu Mzee wa Farasi.
Alisema, Kimobitel alikuwa anatuhumu kuwa Mzee wa Farasi akiwa Mkurugenzi wa Extra Bongo, ana tabia ya kutoa upendeleo kwa baadhi ya wanamuziki.
Aliendelea kusema, Kimobitel alishusha tuhuma kwamba Mzee wa Farasi anampendelea zaidi mwanamuziki Pentagon na kuwasahau mastaa wanaoibeba bendi akiwemo yeye.
“Kimobitel alidai Choki anampendelea Pentagon kuliko yeye na mastaa wengine wa bendi. Maelezo hayo yakaonekana yamemkera Bob Kisa, kwahiyo akamjibu kwamba asimseme mtu ambaye hayupo.
“Bob Kisa akamwambia Kimobitel kuwa bendi ni timu na hakuna staa, kauli ambayo ilimuudhi Kimobitel, kwahiyo wakaanza kutupiana maneno, baadaye Bob Kisa hasira zilizidi akamfuata na kumtandika makofi,” alisema mtoa habari wetu.
Paparazi wetu alipozungumza na Bob Kisa alisema: “Mimi sikupenda sana tabia yake ya kumsema mtu hayupo, hali kama ile kwenye bendi ni majungu, na nilipojaribu kumwambia Khadija aache kuchonga, alinitukana.”
Kwa upande wa Mzee wa Farasi, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza: “Kwa ufafanuzi nadhani ni vizuri ukazungumza na wahusika.”

Khadija Mnoga katika pozi.

BABY MADAHA AMNYAKA GERRY

Staa wa kike mwenye heshiuma tele katika Bongo Flava, Baby Joseph Madaha, ameendelea kuzua minong’ono kibao kwa jamii kutokana na ukaribu aliyonao na msanii chipukizi mwenzake, Elius George ‘Gerry’, Mateja20 haipitwi.
Kwa mujibu wa sosi makini wa Amani, habari kubwa iliyozagaa kitaa ni kwamba Baby kwa sasa amemnasa chipukizi huyo aliyeshirikishwa kwenye ngoma ya Mama Ntilie inayosumbua katika runinga na redio mbalimbali.
Inaelezwa kuwa Baby amekuwa akionekana ‘vere klozi’ na dogo huyo, jambo linalosababisha kuenea kwa ‘rumansi’ hizo kama moto wa kifuu.
Kama kawa kama dawa, baada ya kuinyaka ishu hiyo, Mateja20 ilimuinulia mkonga wa simu Baby na kumsomea ‘eituzedi’ ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Jamani jamani, yule kweli ni rafiki yangu lakini siwezi kuvunja naye amri ya sita kwenye vitabu takatifu.”

HAPPY BIRTHDAY SHALUWA!!!

USIKU wa kuamkia leo Mateja20, nilikuwa mmoja wageni wa heshima katika sherehe ya kutimiza miaka 27 ya mfanyakazi mwezangu Joseph Paul Shaluwa. Ambayo ilifanyikia ndani ya kiwanja kimoja murua pande za Sinza Makaburini jijini Dar es Salaam. Nikiwa pale niliteuliwa kufanikisha zoezi zima la kufungua Shampen ambalo nililifanya kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba hakuna aliye chafuka kwa Shampeni hiyo. Aidha Shaluwa alitumia muda huo kumtambulisha laazizi wake, na baadaye zoezi la kulishana Keki lilichukua nafasi kubwa mahali hapo. 'So' kutokana na burudani niliyoipata pande hizo nampongeza sana shaluwa kwa maandalizi yake mazuri na Mungu amuongezee maisha marefu zaidi Ameni. Hii ndiyo Keki iliyotumika katika Birthday hiyo Joseph Shaluwa kushoto akisaidiwa kukata keki hiyo. Mateja akinyanyua Shampen juu marabaada ya kuifunguwa. Aloyce James kushoto akisubilia kumiminiwa shampen na Mateja20 katikati ni Ally Mbetu naye akisikilizia zoezi hilo. Joseph Shaluwa akibanjuka na Coletha aliyekuwa MC wa shughuli hiyo.

Kigogo, mhariri mwandamizi Global akiwa na toto lake!!!

KUAMBIANA, STAA WA MAISHA PLUS… ILIBAKI KIDOGO TU WATOANE ROHO!

Nyota wa filamu ya Fake Pastors, Adam Kuambiana na staa wa Maisha Plus, season one 2009, Moshi Mahona juzikati ilibaki kidogo tu watoane roho baada ya kuchenjiana vibaya, Musa Mateja anakupa kitu kamili.
Event hiyo iliyoshuhudiwa na ‘polisi’ wa Amani vibes ili-take place ndani ya Baa ya Miller, Sinza kwa Remmy, Dar, mwishoni mwa wiki ambapo wawili hao walikutana katika mishemishe za kutandika ulabu a.k.a mma.
Awali ilidaiwa kwamba, kuhitilafiana na kutaka kutandikana kwa wawili hao kulisabibishwa na majigambo ya Kuambiana ambaye alipomuona Moshi alisikika akiji-proud kwa kumwambia kwamba alipendeza sana na asingekuwa na uhusiano na rafiki yake, Efrancyia Mangii, basi yeye angekuwa halali yake.
Maneno ya Kuambiana yalimkera Moshi ambaye alipandwa na hasira kisha kumjibu ndivyo sivyo.
Kuambiana alipojibiwa rafu aliona kama ishara ya dharau na kuanza kurushiana maneno mbofu mbofu huku kila mmoja akitaka kumtafuna mwenzake kabla ya kuamua kuondoka eneo hilo.
‘Polisi’ wa Amani alipotaka kujua kulikoni, Moshi alijibu kuwa Kuambiana alimletea za kuleta ndipo akaona isiwe ishu kama bhita na iwe bhita.

Adam Kuambiana katika pozi

Wednesday, August 25, 2010

MAMBO YALIKUWA HIVI CLOUDS TV

Wadau walijenga pozi kama hivi.

'Adam Kuambiana, haa!! Benny, yaani umepata ... paja? aah ... na mimi basi wangu!!!

Oya kama ume... tusepe wangu...

'Kibonde, hata mwezi ... kikuku hakivuki? okay but siyo issue tuchonge mzazi!!!

Baada ya hapa kuvuma kimataifa kama kawa!!!

Mchomvu, swagger kama kawa!!!

Wakuvanga we' mwenzangu tofauti yetu kampuni tu, 'Mchovu freeshi baana!!

Kujiramba ilikuwa kawaida.


Wakuvanga, sali kwanza acha kuvunga.'Lazima viazi vinikome leo'
'Nahisi chai kama ya moto hivii!!!

Mama na mwana.

'Msosi siyo ishu issue ni kupata kumbukumbu.