Social Icons

Friday, August 27, 2010

LINAH WA THT AKILI KUTOA PENZI KWA AMINI!!

STAA chipukizi katika gemu ya Muziki wa kizazi kipya Bongo, Estalinah Sanga ‘Linah’ anayeiwakilisha ‘gemu’ kutoka nyumba ya vipaji THT amemuanika mtu anaye vunja naye amri ya sita na kuzima minongo’no iliyoenea mtaani kuwa anatoka na nguli wa hip hop nchini Ibrahimu Musa ‘Roma’

Linah anayetamba kwenye chati za Bongo Fleva hivi sasa na ngoma ya ‘Wrong number’ aliyomshirikisha Barnaba ameliambia Ijumaa kuwa, ameamua kuweka kila kitu wazi ili kuepuka maneno ya watu ambao anahisi wanataka kuharibu uhusiano wake.

“Nimesikitishwa na taarifa za kuwa mimi natoka na Roma, huo ni uzushi kwani Roma ni shemeji yangu na kila anaye fahamu ukweli anajua kuwa mtu wangu ni Amini Mwinyimkuu yule aliyeimba wimbo maarufu wa Bado Robo saa,” alisema Linah.

Nyota huyo alitanabaisha kuwa, anampenda Amini kuliko kitu kingine chochote hivyo hafikirii kufanya jambo lolote ambalo litatishia uhai wa uhusiano wao mpaka mpango na hadi yao ya kufunga ndoa itakapotimia.





0 comments: