Social Icons

Thursday, August 26, 2010

KIMOBITEL ACHEZEA VIGANJA!!!

First Lady wa Bendi ya Extra Bongo next level ‘Wazee wa kujinafasi’, Khadija Mnoga ‘Kimobitel’, amepigwa makofi na mwimbaji mwenzake.
Kimobitel, alipewa kisago na Bob Kisa hivi karibuni huku chanzo kikitajwa kwamba ni Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Bob Kisa alimkung’uta Kimobitel makofi kwenye Ukumbi wa Nanenane, Morogoro kwa maelezo kwamba alimsema vibaya Mzee wa Farasi wakati hayupo.
Chanzo chetu kilisema na baadaye kuthibitishwa na Bob Kisa kuwa wakiwa nje ya ukumbi huo baada ya shoo, Kimobitel alianza kuchonga kuhusu Mzee wa Farasi.
Alisema, Kimobitel alikuwa anatuhumu kuwa Mzee wa Farasi akiwa Mkurugenzi wa Extra Bongo, ana tabia ya kutoa upendeleo kwa baadhi ya wanamuziki.
Aliendelea kusema, Kimobitel alishusha tuhuma kwamba Mzee wa Farasi anampendelea zaidi mwanamuziki Pentagon na kuwasahau mastaa wanaoibeba bendi akiwemo yeye.
“Kimobitel alidai Choki anampendelea Pentagon kuliko yeye na mastaa wengine wa bendi. Maelezo hayo yakaonekana yamemkera Bob Kisa, kwahiyo akamjibu kwamba asimseme mtu ambaye hayupo.
“Bob Kisa akamwambia Kimobitel kuwa bendi ni timu na hakuna staa, kauli ambayo ilimuudhi Kimobitel, kwahiyo wakaanza kutupiana maneno, baadaye Bob Kisa hasira zilizidi akamfuata na kumtandika makofi,” alisema mtoa habari wetu.
Paparazi wetu alipozungumza na Bob Kisa alisema: “Mimi sikupenda sana tabia yake ya kumsema mtu hayupo, hali kama ile kwenye bendi ni majungu, na nilipojaribu kumwambia Khadija aache kuchonga, alinitukana.”
Kwa upande wa Mzee wa Farasi, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza: “Kwa ufafanuzi nadhani ni vizuri ukazungumza na wahusika.”

Khadija Mnoga katika pozi.

0 comments: