Social Icons

Wednesday, August 31, 2011

WAISLAMU KOTE DUNIANI WASWALI SWALA YA EID EL FITR LEO

LEO ni sikukuu ya Eid El Fitr ambapo waislamu kote duniani wamekusanyika katika misikiti na kuswali mara baada ya kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, ikiwa ni moja ya nguzo tano za dini ya kiislamu. mara baada ya kumalizika mfungo wa mwezi wa ramadhan waislamu hufanya ibada na kusherehekea kwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukumbushana mambo muhimu yanayohusu dini ya kiislamu.
Kama wanavyoonekana katika picha ni waumini wa dini ya kiislamu wakiswali katika msikiti wa Mtoni kwa Kabuma wilayani Temeke jijini Dar es salaam.
Hapa wakiswali kwa kusujudu.
Samaki mkunje angali mmbichi watoto wakitoka kuswali msikitini huku wenzao wakiwaangalia.
Vijana mbalimbali wakirejea nyumbani mara baada ya swala ya Eid asubuhi hii.
Asubuhi hii pilikapilika mbalimbali barabarani waislamu wakienda kuswali misikitini.
PICHA/HABARI NA FULL SHANGWE

Tuesday, August 30, 2011

CARNIVAL BABUKUBWA KATIKA MABALA YA ULAYA YAFANA

Msafara wa maandamano ukizunguka katika kitongoji cha Notting hill.
URBAN PULSE CREATIVE wakishirikiana na Miss Jestina Blog wanatujuza matukio katika picha ya 'Notting hill Carnival' iliyofanyika Jumapili tarehe 28 agosti 2011. Hii ilikuwa siku ya kwanza Carnival ya watoto ambayo hufanyika kila mwaka tangu mwaka 1964 ambayo siku ya pili inafuatiwa na siku ya watu wazima.

Maelfu ya watu zaidi walijitokeza katika mitaa ya Notting hill wakati wa Carnival hiyo ambayo ni tofauti na miaka yote pia iliyokuwa na usalama wa polisi 1000 wa ziada na kufanya Jumla ya polisi kufikia 6500, kwa ajili ya usalama na kufanikisha shuguli nzima ya wanachi walio hudhuria.

Hii inatoka na maasi yaliyo tokea hivi karibuni katika kitongoji cha Tottenham na sehemu nyingine nchini Uingereza.
Jumla ya watu 53 wanashikiliwa na polisi kutokana kutaka kufanya fujo katika carnival hiyo.












VODACOM MISS SPORTS LADY 2011 NI LOVENESS

Vodacom Miss Sports Lady 2011, Loveness Flavian akiwa katika pozi la ukweli baada ya kushinda na kutangazwa kutwaa taji hilo na kuwa mrembo wa tatu kati ya warembo 15 waliojikatia tiketi ya kutinga katika Nusu fainali za Vodacom Miss Tanzania 2011, zinazotarajia kufanyika Septemba 10, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Vodacom Miss Top Model, Mwajabu Juma (katikati) ambaye alikuwa mrembo wa kwanza kuingia hatua ya Nusu Fainali ya Vodacom Miss Tanzania 2011 akiwa na mrembo wa pili kuingia katika hatua hiyo ya 15 bora Vodacom Miss Photogenic Tracy Mabula (kushoto) wakipozi kwa picha na mwenzao wa tatu kutinga katika hatua hiyo baada ya kutwaa taji la Vodacom Miss Sports Lady, Loveness Flavian, usiku wa kuamkia jana katika Jumba la Vodacom Dar es Salaam.
Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Vodacom Miss Sports Lady wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutangzwa mshindi usiku wa kuamkia jana. Kutoka kushoto ni Rose Hurbert, Husna Maulid, Loveness Flavian, Salha Izrael na Delillah Ghalib. Mchujo waa warembo hawa ulifanyika katika siku ya michezo ya Vodacom Miss Tanzania wiki iliyopita.
Vodacom Miss Sports Lady, Loveness Flavian, akipongezwa na warembo wenzake wa Vodacom Miss Tanzania waliofanikiwa kuingia tano bora ya kuwania taji hilo la michezo baada ya mwenzao huyo kutajwa kuwa ndiye mshindi na anakuwa mrembo wa tatu kuingia katika hatua ya Nusu fainali za Vodacom Miss Tanzania mwaka huu.

REDD'S YATOA ZAWADI IDD EL FITR KWA WAZAZI NDANI YA HOSPITALI YA MWANANYAMALA

Mshiriki wa miss Tanzania Jenifer kakolaki(kushoto),Tanzania akimbembeleza mtoto mchanga ndani ya Hospitali hiyo.
Warembo wakimsikiliza Mganga Mkuu katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar.
Mrembo akisaini kitabu cha wageni kwa niaba ya warembo wenzake.
Miche ya sabuni na nepi kwaajili ya watoto wachanga waliozaliwa, zawadi hizo zilikabidhiwa hospitalini hapo na warembo kupitia kinywaji cha REDD'S.
Mrembo akionyesha upendo kwa mama na mtoto.
Salha Israel (kushoto, akimbeba kwa furaha mtoto mchanga wodini hapo.
Ni upendo wa hali ya juu sana kwa warembo wa Miss Tanzania kuonyesha ushirikiano na watu tofautitofauti katika jamii yetu,hii imekuwa ikiwezeshwa na Redd's kinywaji murua.
Mrembo toka Tanga akishangaa mtoto alietoka kuzaliwa kama dakika kumi zilizopita,mi kupita REDD'S utatambua haya.
Brand Manager wa REDD'S ,Victoria akiongea na waandishi wa habari nia ya kutoa zawadi hizi kwa wamama waliojifungua miche ya sabuni na nepi kwaajili ya watoto wao wachanga.
Miss tanzania Geneviev Mpangala akiongoza warembo hao ambao walikuwa katika picha ya pamoja na madaktari wa hospitali ya Mwananyamala jijiniDar.
Ziara ilisitishwa kwa picha hii,pongezi REDD'S kuwafikia akina mama waliojifungua kipindi hiki cha Idd.

FUTARI YA KISOMO NA HITIMA YA JUMUIYA YA KIISLAMU NCHINI MAREKANI (TANZANIA MUSLIM COMMUNITY WASHINGTON DC YAFANA

Mgeni rasmi katika futari hiyo akitoa hutuba fupi ya kuwa pongeza na kuwashukuru viongozi pamoja na wana Jumuiya ya kiislamu Tanzania, na hotuba fupi ya kuhamasisha Watanzania waliokuwepo Marekani kujumuika na kusheherekea miaka 50 ya Uhuru wa nchi Tanzania.
Mgeni rasmi wa shughuli hiyo Balozi Mwanaidi Maajar, akiwa na waumini katika futari iliyoandaliwa na jumuiya ya Kiislamu Tanzania waishio nchini humo, kwenye ukumbi wa Hillandale Local Park, New Hampshire Avenue, Silver Spring Maryland Nchini Marekani.
Waumini wakipata futari ilioandaliwa na jumuiya ya Kiislamu Tanzanian Muslim Community Washngton DC
Waumini wa jumuiya ya Kiislamu Tanzanian Muslim Community wakiwa katika futari
Washauri waTanzanian Muslim Community Washngton DC, Jabiri Jongo katika picha ya chini na juu Mh Uwesu Bakar wakiwa katika dua ya kisomo cha kumuombea Marehemu Baba wa Dada yetu Jasmine Rubama, pamoja na kuwaombea jamaa zetu wote waliotangulia mbele. M/mungu awarehemu na awajaliee makazi meema peponi Amin.

Waumini wa dini ya kiislamu kwa upande wa wanawake wakiwa katika futari ya pamoja iliyofanyika jana jumapili Aug 28,2011 Silver Sring Maryland.
Dada yetu naye alihudhuria katika futari ya pamoja kwenye ukumbi wa Hillandale Local Park, mitaa ya New Hampshire Avenue, Silver Spring Maryland.
Ndugu jamaa na marafiki waliohudhuria katika kisomo pamoja na futari ilioandaliwa na jumuiya ya Kiislamu Tanzanian Muslim Community kenye ukumbi wa Hillandale Local Park New Hampshire Avenue,
Silver Spring Maryland.Saadie Fuad akipata flash ya pamoja na Amina Saleh katika futari ya pamoja
Waumini wa dini ya kiislamu kwa upande wa wanawake wakipata flash ya pamoja baada ya kumaliza futari ya pamoja iliyoandaliwa na jumuiya ya Kiislamu Tanzanian Muslim Community, katika ukumbi wa Hillandale Local Park New Hampshire Avenue, Silver Spring Maryland. Jana Jumapili Ramadhani ya 28, Aug 28,2011 picha zikiwa ni kama kumbukumbu ya Mwezi mtukufu wa ramadhani 2011 kutoka kwa mpiga picha wenu wa swahilivilla Editor Abou Shatry.
Dada yetu huyu naye alihudhuria katika futari ya pamoja kwenye ukumbi wa Hillandale Local Park, mitaa ya New Hampshire Avenue, Silver Spring Maryland.

AUAWA KWA WIZI WA KUKU

Marehemu NASIB EXZAVERY maalufu kama Mkemia akiwa amechomwa moto eneo la viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge Jijini Mbeya kwa kosa la wizi wa kuku ambaye Mwenye Kuku huyo hajafahamika.

Marehemu NASIB pamoja na Kuku waliodaiwa kuwaiba na kumsababishia kifo.
Inasikitisha sana
Jeshi la Polisi likiwa limefika eneo la Tukio kuuchukua Mwili wa marehemu na kuupeleka katika hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya.

PICHA/HABARI: MBEYA YETU BLOG

Monday, August 29, 2011

TWANGA KUTUMBUIZA SIKUKUU YA IDDI MANGO GARDEN


BENDI ya Muziki wa dansi chini ya The African Stars International 'Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani', katika sikukuu ya Iddi mosi, wanatarajia kufanya maonesho yake ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mateja20, makao makuu ya ofisi za Bendi hiyo Kinondoni jijini Dar Meneja wa bendi hiyo Hassan Rehani alisema, katika sikukuu hiyo Twanga pepeta itatoa burudani zake ndani ya Ukumbi huo mchana na usiku na kesho yake watakuwa ndani ya Ukumbi wa TCC Club Chang'ombe.

"Burudani zetu zote zitaishia hapo siku ya sikukuu Iddi na 4/09/2011, tutakua ndani ya Ukumbi wa Msasani Beach Kawe jijini Dar es Salaam, katika shoo maalum", Alisema Hassani.

BEI ZA VIINGILIO KATIKA MECHI YA TAIFA STARS NA TIMU YA ALGERIA VYWAWEKWA HADHALANI LEO

VIINGILIO kwa ajili ya mechi ya mchujo kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya Taifa Stars na Algeria vitakuwa kama ifuatavyo;
Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Bw. Boniface Wambura amesema "Viti vya kijani ni sh. 3,000, viti vya bluu sh. 5,000, viti vya rangi ya chungwa sh. 7,000, VIP C sh.10,000, VIP B sh. 20,000 na VIP A sh. 30,000. Tiketi zitaanza kuuzwa Septemba Mosi mwaka huu".
Taifa Stars tayari iko kambini tangu jana (Agosti 28 mwaka huu) na inaendelea na mazoezi Uwanja wa Karume ambapo wachezaji wote wa ndani waliripoti jana mchana na kuanza mazoezi jioni.
Wachezaji wan je waliofika jana usiku ni Abdi Kassim na Dan Mrwanda kutoka Vietnam na Mbwana Samata kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Athuman Machupa (Sweden), Henry Joseph (Norway) na Idrisa Rajab (Kenya) wanaingia leo jioni.
Nizar Khalfan wa Vancouver Whitecaps ya Canada ndiye atakayekuwa mchezaji wa mwisho kuripoti kambini. Khalfan atatua nchini kesho saa 5.15 usiku kwa ndege ya PrescisionAir akitokea Nairobi.

JAPAN YAIPA TANZANIA BILIONI 40 KWA AJILI YA UJENZI WA DARAJA LA LUSUMO NA BARABARA JIJINI DAR

Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (leo) jijini Dar es salaam mara baada ya kusaini msaada wa shilingi bilioni 40 kwa ajili ya miradi miwili ya maendeleo. Mradi wa kwanza ni ujenzi wa daraja la Rusumo lilopo mpakani wa Tanzania na Rwanda na uimarishaji wa barabara jijini Dar es salaam. kulia ni Balozi wa Japan nchini Hiroshi Nakagawa.

Picha/Habari na Tiganya Vincent,

Hadija Chumu na Moshi Stewart-Maelezo

Dar es Salaam

SERIKALI imesaini msaada wa shilingi bilioni 40 na serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miradi miwili ya maendeleo hapa nchini.

Akiongea na wanahabari leo Waziri wa Fedha na Uchumi Mustapha Mkulo amesema, miradi hiyo ni ya ujenzi la wa daraja la Rusumo litakalounganisha nchi ya Tanzania na Rwanda na upanuzi wa barabara ya Kilwa ambapo itasaidia shughuli za maendeleo baina ya nchi hizo.

Waziri Mkulo alisema

Alisema upanuzi wa barabara ya kilwa utapunguza kwa kiasi kikubwa foleni na adha nyingine za kimiundombinu ndaji ya jiji la Dar es salaam,

Nae Balozi wa Japani nchini Bw Hiroshi Nakagawa amesema msaada huo ni matokeo ya ushirikiano uliopo kati ya Japani na Tanzania ambapo utasaidia kuimarisha uchukuzi na usafirishaji nchini,

Balozi Nakagawa alisema kiasi cha bilioni 1.86 za kijapani zitasaidia upanuzi wa daraja la Rusumo, wakati Yen Milioni 37 zimetolewa kukamilisha upanuzi wa barabara ya kilwa

Nae mwakilishi wa shirika la JICA nchini Bw Yukihide Katsuta amesema fedha zilizotolewa na shirika hilo ni milioni 769 za kitanzania ambazo zitasaidia kupata mwongozo sahihi wa kitaalam utakaopelekea ubora katika ujenzi na upanuzi wa barabara ya kilwa unaotegemea kukamilika hivi karibuni

Aidha mwakilishi wa TANROADS Mhandisi Mfugale amesema watahakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati na ubora unaohitajika ili kuhakikisha na kusimamia upanuzi wa daraja hilo pamoja na ule wa upanuzi wa barabara ya kilwa unatimizwa kulingana na fedha zinazotolewa.

WATEJA WA MTANDAO WA VODACOM KUSHINDANIA KITITA CHA SHILINGI BILIONI MOJA KATIKA PROMOSHENI YA MEGA

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba akielezea namna ya kushiriki katika promosheni Mpya ya Mega inayowawezesha wateja kushiriki na kushinda bila kutozwa fedha. Mazungumzo hayo yalifanyika Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano ya Wateja, Charity Safford.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba akiongea na waandishi wa habari kuhusu promosheni Mpya ya Mega inayowawezesha wateja kushiriki na kushinda bila kutozwa fedha. Mazungumzo hayo yalifanyika Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano ya Wateja, Charity Safford.
Dar es salaam Agosti 29, 2011.

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetangaza promosheni ya aina yake kwa wateja wake nchi nzima ambao watawania zawadi ya shilingi milioni kumi na moja pamoja na televisheni za kisasa aina ya Samsung LCD mia moja kila siku kwa siku mia moja.
Akitangaza promosheni hiyo iitwayo Mega Promotion jijini Dar es salaam Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba amesema promoheni hiyo ni kubwa kuwahi kuendeshwa na Vodacom tangu ilipofanya mabadiliko makubwa ya kimuono na falsafa mapema mwaka huu yaliyohusisha mabadiliko ya rangi kutoka buluu kuwa nyekundu pamoja na nembo ya kampuni. Mwamvita amesema promosheni hiyo itadumu kwa siku mia moja kuanzia Agosti 26 hadi Desemba 6 mwaka huu na ili kushinda mteja wa Vodacom atapaswa kujiunga katika shindano la kujibu maswali kupitia simu yake ya mkononi ambapo kupitia majibu ya maswali hayo mteja atakuwa akijikusanyia pointi zitakazoshindanishwa kwenye droo za kila siku.
"Vodacom ni ya kwanza kuleta promosheni ya aina hii. Nasema hivi kwa sababu Mega Promosheni inampa mteja fursa ya kuchagua hatua ya ushiriki.
Ushiriki wa BURE wa droo za Standard ambapo mteja hujiunga BURE na kuwa na nafasi ya BURE kushinda televisheni moja ya kisasa aina ya Samsung LCD kila siku na hatua nyengine ni ya droo za Premium ambapo mteja atajiunga kwa gharama NAFUU ya shilingi mia tano na hamsini kwa siku kuwania kitita cha shilingi milioni kumi na moja kila siku"
Alisema Mwamvita. Mwamvita ameongeza kuwa ili kushiriki droo ya bure mteja atapaswa kutuma ujumbe mfupi wa neno BURE ama FREE kwenda nambari 15015 na mara moja atapokea swali la kwanza litakaloanza kumpatia pointi ambazo mwisho wa siku zitashindanishwa katika droo ya wazi itakayooneshwa moja kwa moja kupitia televisheni ya ITV kila siku saa moja na dakika hamsini na tano usiku.
Burudani ya aina yake katika promosheni ya Mega ipo katika droo ya Premium ambayo kupitia droo za kila siku inatoa mshindi mmoja wa zawadi ya kitita cha fedha taslimu shilingi milioni kumi na moja.Hata hivyo mteja ana uhuru wa kuchagua kuondoa ushiriki wake katika droo hii wakati wowote.
"Ifahamike kuwa mshiriki wa droo hii ya Premium kwanza lazima ujiunge na hatua ya kwanza ambayo ni ya BURE kuwania televisheni kupitia droo ya Standard na baada ya hapo mteja atakuwa na uamuzi wa kuendelea na hatua ya Premium ambapo mbali na kushiriki na kushinda zawadi ya fedha bado anakuwa na mshiriki wa droo ya Standrd hivyo anaweza kushinda zawadi mbili kwa mpigo
"Alifafanua Mwamvita.
Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa Promoheni hiyo ya Mega Mkurugenzi wa Mahusiano ya Wateja wa Vodacom Charity Safford amesema Vodacom ina imani kwamba promosheni hiyo itawavutia wateja wake hasa kutokana upekee ilionao.
"Wateja wetu ni kipaumbele chetu cha kwanza kabisa na daima tunajituma kuhakikisha tunawapa huduma bora zaidi kuweza kukidhi mahitaji yatokanayo na shughuli zao za kila siku na kwa mara nyengine tunawaomba watanzania wafurahie hiki tunachowatangazia sasa ambapo kunatoa fursa ya kushinda zawadi kwa kila mmoja aliye tayari kujiunga kwa kulipia au hata yule ambae hayupo tayari kujiunga kwa kulipia lakini anapenda kushinda zawadi"

Sunday, August 28, 2011

AIRTEL YAVUMA NYANDA ZA JUU KUSINI

Kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimuelekeza sehemu ya kuweka sahihi mke wa Bw, Albert Gerge Mwasibata (katikati), wakwanza toka kulia mshindi wa gari ya airtel katika promosheni iliyoisha ya Jivinie ikiwa ni ishara ya kupokea zawadi ya gari yao mpya aina ya Corolla kutoka Airtel


Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea na wananchi wa Tukuyu Mbeya wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa minara ya mawasiliano ya Airtel pamoja na kukabidhi zawadi ya gari mpya aina ya Toyota Corolla mshindi mkazi wa mkoa huo Bw, Albert George Mwasibata aliyeibuka mshindi katika promosheni ya jivunie


Katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe Tukuyu Bw, Moses Mwidete (watatu toka kulia) akikabidhi ufunguo wa gari mpya aina ya Toyota corolla kwa mshindi wa promosheni ya Airtel JIVUNIE bw Albert Mwasibata katikati. Wakwanza kushoto ni Ofisa Masoko wa airtel Kanda ya Kusini Bw Jonas Mbaga akishuhudia makabidhiano kwa pamoja na wafanyakazi wenzake kulia katika viwanja vya mpira Tukuyu


Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando kulia akimpongeza mshindi wa Promosheni iliyoisha ya Airtel JIVUNIE bw Albert Mwasibata katikati ni Katibu Tawala wa Wilaya Rungwe Tukuyu Bw Moses Mwidete ambae alikuwa mgeni rasmi wakati wa makabidhiano hayo katika viwanja vya mpira wa miguu Tukuyu Mbeya.wishoni mwa wiki.

Mshindi wa gari ya promosheni ya Airtel JIVUNIE wa mkoani mbeya Bw Albert George Mwasibata akiwapungia mikono wakazi wenzake wa mkoani humo kwa kufuraha mara baada ya kukabidhiwa gari yake mpya aina ya Corolla katika viwanja vya Tukuyu mbeya baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya gari hiyo.


Mshindi wa gari ya promosheni ya Airtel JIVUNIE Bw, Albert George Mwasibata akiwasha gari lake jipya aina ya Corolla mara baada ya kukabidhiwa katika hafla ya makabidhiano iliyoandaliwa na Airtel katika viwanja vya Tukuyu Mbeya.


Baadhi ya wakazi wa Tukuyu Mbeya wakishangilia na wengine kulibusu gari jipya aina ya Toyota Corolla lililotolewa zawadi na kampuni ya simu za mkoni ya airtel kwa Bw Albert George Mwasibata aliyeibuka mshindi katika promosheni iliyoisha ya Airtel JIVUNIE katika viwanja vya Tukuyu Mbeya mwishoni mwa wiki hii.


Umati uliyofulika kushuhudia zoezi hilo.
... wakishangaa gari hilo


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel mwishoni mwa wiki hii imezindua huduma za mawasiliano mjini na vijijini ikiwa ni katika muendelezo wa dhamira yake ya kufikia wanananchi wengi na kuinua shughuli za uchumi nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari Meneja wa Kanda wa Airtel bw Fredrick Mwakitwang alisema “Airtel leo tunazindua na kupanua huduma zetu mkoani mbeya –Tukuyu katika vijiji vya Katumba, Watco, Ibililo, Ikuti na Mkoani Ruvuma katika kijiji cha Litola kilichopo Mbinga.

Wakazi wa Mbinga na Tukuyu sasa wataboresha shughuli zao za kilimo na biashara kwa urahisi na kupata taarifa mbalimbali zitakazo wawezasha kufanikisha kazi zao za kila siku kupitia mawasiliano ya Airtel kwa uhakika.

Wakati huo huo Airtel ilikabidhi gari mpaya aina ya Corolla kwa mshindi wa promosheni ya Airtel Jivunie Bwana Albert George Mwasibata mkazi wa Tukuyu Mbeya. Shindano ili liliwashirikisha wateja wote wa Airtel na bwana Mwasibata kuibuka mmojawapo wa mshindi kati ya washindi wengi waliopatikana nchini kote.

Akiongea katika halfa maalumu iliyoandaliwa na Airtel mkoani Mbeya Tukuyu Meneja mahusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema, Airtel imejidhatiti na kujipanga kuwapatia wateja wake huduma bora na kwa bei nafuu

leo hii tumefikisha huduma hii hapa Tukuyu vijijini, hii inaonyesha wazi kuwa tunaendelea kutekelezaji dhamira ya kuchangia maendeleo ya nchi kupitia sekta ya mawasiliano. Airtel tunaimani kuwa kuboresha mawasiliano katika vijiji itaongeza chachu ya kipeeke katika kuchangia maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Leo hii Vijiji vya Ibililo, watcoIkuti, na Litola wilaya ya Rungwe Tukuyu mnaweza kutumia mawasiliano ya Aitel ya Robo shilingi kwa sekunde kwa kufanya biashara na watu walioko mikoa mingine na kujipatia faida kubwa itakayosaidia kuboresha maisha yenu” alisema mmbando

Aidha Bwana Mmbando alichukua fulsa hiyo kukabidhi gari kwa mshindi wa Mshindi wa promosheni ya Airtel Jivunie Bw, Abert George Mwasibata nakumpongeza kwa kuibuka kuwa mshindi wa promosheni hiyo.

“ wakazi wa Tukuyu hii ni bahati kwetu! sasa tushiriki na tuamini promosheni zinazoendelea kwani kila mteja anaweza kuibuka mshindi kama mwenzetu huyu!

Akiongea baada ya kukabidhiwa Zawadi hiyo bwana Mwasibata alisema nashukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kunikabidhi gari hili leo, hii ni furaha ya pekee kuona Airtel kwa kupitia promosheni ya jivunie imeweza kunikabidhi rasmi zawadi hii, najisikia Faraja ya pekee.

Naye katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe Tukuyu by Moses Mwandete akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Tukuyu alisema “Tunaipongeza kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kutufikishia mawasiliano na kuwa mtandao pekee na wakwanza kupatikana katika vijiji vya Katumba watco, ibililo / ikuti na itola kanda ya kusini.

Airtel imeweka kielelezo na kutoa changamoto kwa wadau wengine katika sekta hii kufikisha huduma zao mahali ambapo mawasiliano hayapo ili kuweka ushindani wa kibiashara ili kuendelea kutupatia unafuu zaidi.

Leo hii Katumba Watco, Ibililo, Ikuti Itola pamoja na vijiji vya jiraji watafaidiaka na huduma za mawasiliano za mtandao wa simu ya Airtel. Tunawaahidi kuwapa ushirikiano kutoka serikalini katika kufanikisha shughuli zenu za biashara hapa nchini ambazo ni chachu kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Pamoja na hilo nichukue fulsa hii kumpongeza mshindi wa promosheni ambaye ametokea Tukuyu mbeya namsihi aendelee kuwa balozi mzuri wa Airtel.