Social Icons

Thursday, August 26, 2010

KUAMBIANA, STAA WA MAISHA PLUS… ILIBAKI KIDOGO TU WATOANE ROHO!

Nyota wa filamu ya Fake Pastors, Adam Kuambiana na staa wa Maisha Plus, season one 2009, Moshi Mahona juzikati ilibaki kidogo tu watoane roho baada ya kuchenjiana vibaya, Musa Mateja anakupa kitu kamili.
Event hiyo iliyoshuhudiwa na ‘polisi’ wa Amani vibes ili-take place ndani ya Baa ya Miller, Sinza kwa Remmy, Dar, mwishoni mwa wiki ambapo wawili hao walikutana katika mishemishe za kutandika ulabu a.k.a mma.
Awali ilidaiwa kwamba, kuhitilafiana na kutaka kutandikana kwa wawili hao kulisabibishwa na majigambo ya Kuambiana ambaye alipomuona Moshi alisikika akiji-proud kwa kumwambia kwamba alipendeza sana na asingekuwa na uhusiano na rafiki yake, Efrancyia Mangii, basi yeye angekuwa halali yake.
Maneno ya Kuambiana yalimkera Moshi ambaye alipandwa na hasira kisha kumjibu ndivyo sivyo.
Kuambiana alipojibiwa rafu aliona kama ishara ya dharau na kuanza kurushiana maneno mbofu mbofu huku kila mmoja akitaka kumtafuna mwenzake kabla ya kuamua kuondoka eneo hilo.
‘Polisi’ wa Amani alipotaka kujua kulikoni, Moshi alijibu kuwa Kuambiana alimletea za kuleta ndipo akaona isiwe ishu kama bhita na iwe bhita.

Adam Kuambiana katika pozi

0 comments: