‘PREZI DAA’ wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Nyoshi El- Saadat hatimaye ameendelea kuboresha afya yake ambapo sasa ni ‘full shavu’ kutokana na uzito wake kuongezeka na kuwa wa kawaida. Nyoshi alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kupungua uzito na kudhoofika kwa muda mrefu, lakini sasa yuko njema.
Akichonga na Mateja20,hivi karibuni, Nyoshi alisema kwamba kwa hivi sasa amekuwa akila vyakula kwa mpangilio maalum ili kuondoa tatizo la kupungua uzito lililokuwa linamnyemelea, hali iliyosababisha afya yake kurudi kwenye ‘mstari’ kwa haraka, huku akipiga mazoezi ya nguvu ili kujenga mwili.
Nyoshi aliiambia Mateja20 kwamba, kitu kingine kilichofanya afya yake kuzidi kuwa bora, ni pamoja na mipango mizuri ya bendi yao, kwani hapo awali alikuwa akipungua uzito kutokana na msongo wa mawazo uliokuwa unamkabili wakati akiumiza kichwa jinsi ya kuinua bendi yake.
Aidha Nyoshi aliweka wazi kwamba katika mchakato wa kurekebisha bendi yao, tayari wameshaseti mambo na kilichobaki ni uzinduzi wa albamu yao mpya inayokwenda kwa jina la Vuta Nikuvute Mathematics 'Mayemba', na kwamba wanatarajia kuizindua albamu hiyo yenye jumla ya nyimbo 12 siku ya Idd Mosi, ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Tuesday, August 31, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment