Irene Uwoya katika pozi na Diamond
MUIGIZAJI ‘high level’ katika kiwanda cha filamu Bongo, Irene Uwoya ‘Oprah’, alijikuta akifanya kile kilichotajwa kuwa ni kumsaliti mumewe, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ baada ya kukutwa akijiachia klabu usiku wakati mwenza wake huyo huwa hapendi.
Irene alinaswa Jumatano ya wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Club Bilicanas uliopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam akisugua kisigino wakati Bendi ya muziki wa dansi nchini, African Stars International ‘Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani’ ilipokuwa ikiporomosha burudani zake kama kawa.
Awali, mwanadada huyo mkali katika kuigiza ‘scene’ za kimapenzi katika filamu mbalimbali alionekana akikatiza ukumbini humo huku akiwa ametinga nguo zilizoonesha kuwa ni shabiki pure wa Timu ya Yanga.
Katika kuweka kumbukumbu vizuri, Mateja20 alimfuata kwa lengo la kutaka ‘kumfotoa’ lakini tofauti na ilivyotarajiwa, Irene aligoma kukaa mbele ya kamera kwa maelezo kuwa, zikitoka picha kwenye gazeti zinazomuonesha yuko klabu atamkwaza ‘mai hazbandi’ wake.
“Picha hiyo itakuwa na madhara kwenye ndoa yangu ikiwa mume wangu atagundua kuwa nimekuja huku Club wakati huwa hapendi hasa niwapo Bongo kujichanganya pande hizi, nimekuja kiubishi ubishi tu,” alisema Irene huku akiwaagiza wapambe wake kuhakikisha hapigwi picha mpaka anaondoka .
Mateja20 ambaye hakutaka kuleta mazingira ya shari ukumbini hapo aliamua kuwa mpole lakini akimshuhudia mrembo huyo akiwa amekosa amani.
Irene ameshakwea pipa kuelekea nchini Cyprus kwa mumewe baada ya kuwepo Bongo kwa siku kadhaa katika mapumziko mafupi.

0 comments:
Post a Comment