
Hayo ni kwa uchache tu, zaidi ungana nami uweze kujua yale ambayo huenda ulikuwa huyajui kuhusu mwanadada huyu.
TQ:Kwanini uliamua kuwa mtangazaji na si kazi nyingine? Je,kuna aliyekushawishi?
GEA:Hakuna mtu aliyenishawishi kuwa mtangazaji ila mimi mwenyewe nilikuwa napenda sana kusaidia jamii kutokana na hilo njia pekee niliamua kusomea fani hii.
TQ:Ni matatizo gani ambayo umekuwa ukikumbana nayo kupitia fani yako?
GEA:Aah! Kusema kweli kutokana na ugumu wa kazi ya uandishi wa habari matatizo nakutanayo mengi tu ingawa mara nyingi nayachukulia kama changamoto za kazi.
TQ:Wanawake wengi wamekuwa wakikumbwa na skendo ya kutoa rushwa ya ngono ili kufanikisha mambo yao na inadaiwa hata wewe ulipitia njia hiyo kupata kazi yako je, unalizungumzia vipi hilo?
GEA:Kwa upande wangu sijawahi kutoa rushwa ya ngono kwakuwa najiamini,nina uwezo mkubwa wa kufanya kazi. Wanaoitanguliza hiyo bora waiache kwani madhara yake ni makubwa kuliko wanavyofikiri.
TQ:Sawa! Turudi kwenye maisha yako ya kimapenzi najua umeolewa je,unaifurahia ndoa yako?
GEA:Yah! Naifurahia sana ndoa yangu maana naamini mume wangu ananipenda kuliko kitu chochote kile.
TQ: Je, ni kitu gani kinachokuvutia zaidi kwa mumeo?
GEA:Duh! We naye, naweza kusema kila kitu cha mume wangu kinanivutia.
TQ:Katika familia yako umejaaliwa kupata watoto? Na je ungependa kuzaa watoto wangapi?
GEA: Nina watoto wawili hadi sasa na malengo yangu ni kuwa na familia ya watoto watatu tu.
TQ:Najua wewe ni muumini wa dini ya Kiislamu ambayo inaruhusu mume kuwa na mke zaidi ya mmoja, je akitaka kuongeza mke wa pili utakuwa tayari kwa hilo?
GEA: Siku zote kwa hilo siko tayari labda aoe bila taarifa yangu na asiniambie ukweli.
TQ:Unadhani ni kipi kilichomfanya mumeo akuoe wewe na si mwanamke mwingine?
GEA:Naweza kusema ilikuwa imeishapangwa na Mungu anioe mimi.
TQ:Ni jambo gani la huzuni lililokuumiza sana katika maishani yako?
GEA: Siku nilipofiwa na baba yangu mzazi na siku mdogo wangu, mtoto wa mama mdogo aliponifia mikononi mwangu hospitalini. Nikikumbuka matukio hayo mawili hadi leo huwa nakosa raha.
TQ:Nini malengo yako ya baadaye?
GEA: Ni kujiendeleza zaidi katika kazi yangu ya utangazaji.
TQ: Unawashauri nini mastaa wenzako wa kike?
GEA: Wajiheshimu wawapo mbele za watu. Waache majivuno yasiyo na msingi na kwamba wanapopata kazi wafanye kwa bidii bila kusubiri kusukumwa.
TENQUESTION UTAISOMA KUPITIA MATEJA20 KILA SIKU YA IJUMAA.
0 comments:
Post a Comment