Social Icons

Saturday, August 28, 2010

FUTARI ..... BENNY KINYAIYA!!!

MTANGAZAJI wa Shirika la Habari la Taifa, TBC1 kupitia Kipindi cha B&M, na mkurugenzi wa Kinyaiya Pub iliyopo Kinondoni nyuma ya Ukumbi wa Mango Garden Benny Kinyaiya juzikati nusura yamkute ya kumkuta baada ya kufakamia futari kwa pupa na kujikuta akiungua mdomo.
Ishu hiyo ilitokea katika Ofisi za Clouds Entertainment zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na uzinduzi wa kipindi cha Televisheni ya Clouds kiitwacho Take One uliokwenda sambamba na kuwafuturisha watu mbalimbali.
Akiwa miongoni mwa wageni waalikwa, Benny alinaswa akiwa ameshikilia sahani iliyokuwa imesheheni futari huku akionekana kama aliyekuwa na ‘ubao’ mkali.
Paparazi wetu wa Mateja20 aliendelea kumtolea macho kwa mbali akijua chochote kingeweza kutokea kwa staa huyo na ghafla aliinuka na kutoka nje huku akiwa ameshikilia mdomo wake.
Taarifa iliyopatikana baadae ilidai kuwa, kilichomfanya staa huyo atoke nje ni kwenda kujipatia huduma ya kwanza baada ya kuungua mdomo kwa futari.
Akiongea na Mateja20 Benny alisema: “Ni kweli nimeungua mdomo lakini pia kuna kitu kimenikwama ambacho nahisi ni mfupa, sijui nina balaa gani. Hata hivyo najisikia freshi kidogo baada ya kunywa kama maji hivi' Alimalizia kwa kusema hivyo mkurugenzi wa Kinyaiya Pub.



0 comments: