Social Icons

Tuesday, August 31, 2010

RAMADHANI YAMTAMANISHA JOAN!!!

KUFUATIA kuendelea na Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa Waislamu, muigizaji wa filamu na muaandaji wa Script Bongo, Joan Matovolwa amepata mchecheto wa kuwasindikiza Waislamu kwa kufunga siku moja moja.
Akipiga Stori na Mateja20, Joan alisema kuwa, mwezi huu ni wa Waislamu japokuwa yeye ni Mkristo anajaribu siku moja moja kufunga kwani hata siku ikifika ya Wakristo kufunga huwa haimpi shida kwani anakuwa ameshazoea kulidhibiti tumbo lake.
Aidha, alifafanua kuwa pindi anapokuwa kwenye mfungo, kitu kikubwa anachopendelea kufuturu ni uji kwani anaupenda sana kuliko hata futari inavyopikwa na ndiyo maana muda ukifika wa kufuturu huwa anakimbilia kikombe cha uji.
“Mimi ni Mkristo, ila ninauheshimu mwezi huu wa Mfungo wa Ramadhani kuliko kitu kingine na ndiyo maana siku moja moja huwa nawasindikiza Waislamu kufunga,” alisema Joan.



0 comments: