USIKU wa kuamkia leo Mateja20, nilikuwa mmoja wageni wa heshima katika sherehe ya kutimiza miaka 27 ya mfanyakazi mwezangu Joseph Paul Shaluwa. Ambayo ilifanyikia ndani ya kiwanja kimoja murua pande za Sinza Makaburini jijini Dar es Salaam. Nikiwa pale niliteuliwa kufanikisha zoezi zima la kufungua Shampen ambalo nililifanya kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba hakuna aliye chafuka kwa Shampeni hiyo. Aidha Shaluwa alitumia muda huo kumtambulisha laazizi wake, na baadaye zoezi la kulishana Keki lilichukua nafasi kubwa mahali hapo. 'So' kutokana na burudani niliyoipata pande hizo nampongeza sana shaluwa kwa maandalizi yake mazuri na Mungu amuongezee maisha marefu zaidi Ameni. Hii ndiyo Keki iliyotumika katika Birthday hiyo Joseph Shaluwa kushoto akisaidiwa kukata keki hiyo. Mateja akinyanyua Shampen juu marabaada ya kuifunguwa. Aloyce James kushoto akisubilia kumiminiwa shampen na Mateja20 katikati ni Ally Mbetu naye akisikilizia zoezi hilo. Joseph Shaluwa akibanjuka na Coletha aliyekuwa MC wa shughuli hiyo.
Kigogo, mhariri mwandamizi Global akiwa na toto lake!!!
Kigogo, mhariri mwandamizi Global akiwa na toto lake!!!
0 comments:
Post a Comment