Social Icons

Monday, January 31, 2011

MP-PESA YAWANUFAISHA 263 WA FESTULA NA MDOMO WA SUNGURA

Mkurugenzi msaidizi wa hospitali ya CCBRT Haika Mawala akimkaribisha Mkurugenzi wa mahusiano na Vodacom Foundation Mwamvita Makamba wa pili toka kushoto akiambatana na Mkuu wa kitengo cha Safaricom Foundation-Kenya Sanda Ojiambo walipotembelea hospitali ya CCBRT kwa lengo la kujionea jinsi gani huduma ya Vodafone M pesa inavyosaidia wagonjwa wa fistula na mdomo wa sungura kwa kutumiwa fedha za nauli na matumizi ya njiani kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini na kuja kutibiwa hospitalini hapo zaidi ya wagonjwa 263 wamenufaika na huduma hiyo.

Mkurugenzi msaidizi wa hospitali ya CCBRT Haika Mawala akimkaribisha
Mkurugenzi wa mahusiano na Vodacom Foundation Mwamvita Makamba

Mkurugenzi wa Vodafone Foundation wa Egypt Noha Saad kushoto akisaini kitabu cha wageni katika hospitali ya CCBRT mara baada ya kutembelea hospitalini hapo na wakurugenzi wenzake Mwamvita Makamba,Mkuu wa kitengo cha Safaricom Foundation-Kenya Sanda Ojiambo wakiwa na lengo la kujionea jinsi gani huduma ya Vodafone M pesa inavyosaidia wagonjwa wa mdomo wa sungura na fistula kwa kutumiwa fedha za nauli na matumizi ya njiani kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini na kuja kutibiwa hospitalini hapo zaidi ya wagonjwa 263 wamenufaika na huduma hiyo.

Mkuu wa kitengo cha Safaricom Foundation-Kenya Sanda Ojiambo(kushoto)akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya CCBRT walipotembelea hospitalini hapo kwa lengo la kujionea ni jinsi gani huduma ya M pesa inavyosaidia wagonjwa wa fetula na wa mdomo wa sungura kwa kutumiwa fedha za nauli na matumizi ya njiani kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini na kuja kutibiwa hospitalini hapo zaidi ya wagonjwa 263 wamenufaika na huduma hiyo,katikati Mkurugenzi wa Vodafone Foundation Uingereza Andrew Dunnet,Mkurugenzi wa Vodafone Foundation Tanzania Mwamvita Makamba.

Mkurugenzi wa hospitali ya CCBRT Tom Vanneste akifafanua jambo kuhusu ugonjwa wa mdomo kisungura na fistula kwa maafisa wa Vodafone M pesa Afrika walipotembelea hospitalini hapo hawapo pichani kujionea jinsi gani huduma ya M pesa inavyosaidia wagonjwa kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini na kuja kutibiwa hospitalini hapo zaidi ya wagonjwa 263 wamenufaika na huduma hiyo.


KISURA WAZAMA KAMBINI

Pichani kati Mwenyekiti na Mwanzilishi wa mradi wa Kisura wa Tanzania (BTA), Juliana Urio,akizumgumza na baadhi ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusina kuanza kambi wa warembo wa shindano la Kisura wa Tanzania 20110.kushoto ni Meneja masoko wa SBC,Bwa.George Michael,Afisa Mipango Ujana wa FHI Bwa.Aziz Itaka,Mwisho kabisa ni Meneja Masoko wa ATCL,Bwa. Musyangi Kajeri

WAREMBO wanaowania taji la Kisura wa Tanzania 2010/11, wameingia kambini mapmea jana katika Hoteli ya Kiromo View Resort, iliyopo nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo,Pwani, tayari kwa fainali zitakazofanyika Machi 12, mwaka huu. Kambi hiyo itahusisha wasichana 25 kutoka mikoa mbalimbali nchini, waliofanikiwakutinga katika hatua ya fainali za shindano hilo, baada ya mchujo uliofanyika kwa miezi miwili.
Mchakato wa kuwapata wasichana
hao, ulianza Desemba 11, mwaka jana, na kumalizika mapema mwezi wa kwanza, ukihusisha warembo kutoka mikoa ya Mwanza,Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora, Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Dodoma, Iringa,Mbeya na Ruvuma.
Akizungumza wakati wa kuwatambulisha warembo hao katika Hoteli ya Kiromo ViewResort, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa mradi wa Kisura wa Tanzania, Juliana Urio kutoka kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), alisema kuwa warembo walioingia kambini, ni wale waliopita katika mchujo baada ya kukidhi vigezovinavyotakiwa.
Vigezo hivyo urefu wa sentimita174, mapaja 36, kiuno 25, kifua 36 na umri ni kati ya miaka 18-27, bila kujali kama mshiriki ameolewa, kuzaa au la.“Mwaka huu idadi ya warembo walioingia kambini imeongezeka, kutoka 20 kama ilivyokuwa awali hadi 25, hii ikitokana na mdhamini wetu Kiromo View Resort kutupa nafasi ya pekee ya kuongeza wasichana watano zaidi,” alisema.Urio aliwataja warembo walioingia kambini kuwa ni Neema Methew na Silipa Swai kutoka Mwanza, Lilian Bussa na Gaudencia Joseph (Mara), Beatrice James (Kagera),
Monica Fikiri na Angella Mombeki (Tabora).Wengine ni Suzana Manoko, Winnfrida Sabega, Rita Swai, Lethina Christoper, Joyce Joseph, Happiness Salimenya, Grace David (Dar es salaam), Dotinata Soro, Neema Kilango, Neema Seley (Arusha), Kipoyane Laibon (Manyara), Mariam-Kissa Isaack, Asha Hamisi, Flavian Makungwa, Lucy John (Dodoma) na Queen Kabisama (Ruvuma)Alisema kuwa wakiwa kambini, warembo hao watapewa mafunzo mbalimbali kuhusiana na maisha yao binafsi na jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowazunguka katika maisha yao ya kila siku, ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo tofauti. Urio aliwapongeza warembo waliopata bahati ya kutinga fainali za shindano hilo,ikiwa ni pamoja na kuwashukuru wazazi waliowaruhusu watoto wao kujiunga shindano hilo, akiwaahidi ‘kuwapika’ vilivyo warembo hao ili waweze kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii ya kitanzania kutokana na matendo yao.
Mdhamini mkuu wa shindano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa, ni Family Health International (FHI), wakati wadhamini wengine ni TBC1, Kiromo View Resort, TanFoam (Arusha), SBC Limited, Flare Magazine, Hugo Domingo, BASATA, GRM Production, Clouds FM, ATCL na MJ Records

MHASIBU MBARONI KWA KUKWAPUA SH BILIONI 1.3 ZA TANESCO



OFISA wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), ametiwa mbaroni na Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kwa tuhuma za kuliibia shirika hilo fedha zaidi ya Sh1.3bilioni.

Tuhuma dhidi ya ofisa huyo (jina linahifadhiwa kwa sasa), zimekuja wakati ambao Tanesco wanaelezwa kuwa na hali mbaya kifedha, kutokana na madai kuathirika kimapato hali inayochangiwa na hujuma zinazofanywa na watu wasiofahamika katika miundombinu yake.

Kadhalika Tanesco hivi sasa wanakabiliwa na kibarua kigumu cha kuilipa kampuni ya kufua umeme ya Dowans fidia ya Sh94 bilioni kufuatia tuzo iliyotolewa na Mahakama ya Kimtaifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC).

Tuzo hiyo kwa Dowans ambayo iko katika mchakato wa kusajiliwa Mahakama Kuu ya Tanzania ili iweze kulipwa, ilitolewa na ICC kufuatia Tanesco kuvunja mkataba baina yake na Dowans kinyume cha makubaliano ya pande hizo mbili.

Habari za zilizolifikia Mwananchi jana kutoka katika vyanzo vya kuaminika na kuthibitishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, William Mhando, zilisema fedha zilizoibwa na mtumishi huyo zilitokana na mauzo ya umeme wa Luku.

Habari hizo zinadai kuwa ofisa huyo ambaye ni Mhasibu Mwandamizi wa mapato ndani ya shirika hilo, anatuhumiwa kuiba fedha hizo kati ya Oktoba 2009 na 2010 katika ofisi za Tanesco mkoa wa Kinondoni Kaskazini, alikokuwa akifanyia kazi kabla ya kuhamishiwa makao makuu mwaka jana.

Melezo ya Mkurugenzi Mkuu Mhando
Akizunguma na Mwananchi kwa simu jana, Mhando alisema ofisa huyo anatuhumiwa kutenda makosa kwa kushirikiana na wafanyabiashara mbalimbali waliokuwa wakinunua umeme katika ofisi hizo.

“Ni kweli huyo mtu tunaye na anatuhumiwa kushirikiana na ma-vendor wetu (wauzaji wa rejareja). Inaonekana alikuwa akiwauzia umeme mwingi kuliko umeme aliotakiwa kuutoa kulingana na gharama walizolipia,” alisema Mhando.

Alisema suala hilo lilibainika baada ya kufanyika kwa ukaguzi wa ndani ambao uliwezesha kugundulika upotevu wa kiasi hicho kikubwa cha pesa na kwamba baada ya kubaini tatizo hilo hatua zilizochukuliwa ni kumhamishia afisa huyo makao makuu ili kupisha uchunguzi.

“Kwa kawaida huwezi kumfukuza tu mtu kazi kienyeji, kwa hiyo kwanza “tulim-charge” tukamtaka aandike maelezo ni kwa nini asifukuzwe kazi ,” alisema Mhando.

Alisema baada ya timu iliyoundwa kushughulikia suala hiyo kukaa na kupitia maelezo yake ilibainika kuwa afisa huyo ana hatia na kwamba hatua iliyokuliwa ni kukatisha mkataba wale wa ajira.

“Lakini kwa kuwa hizo ni pesa nyingi na ni za umma tukaona ku-terminate (kukatisha) tu mkataba wake haitoshi hivyo wakaguzi wakaamua kumfikisha polisi kwa hatua zaidi za kisheria;“Kwa hiyo baada tu ya kukatisha mkataba wake na askari wakamkamata hapohapo ofisini,” alisema Mhando.

Kwa mujibu wa habari kutoka kwa vyanzo hivyo afisa huyo alitiwa mbaroni Ijumaa iliyopita akiwa ofisini kwake makao makuu ya Tanesco, ambako alihamishiwa wakati uchunguzi wa tuhuma zake ukiendelea .

“Mpaka ninavyokwambia hivi sasa yuko Central (Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam), kilidokeza chanzo chetu na kuongeza kuwa huenda leo ofisa huyo akapandishwa kizimbani kwa tuhuma hizo tuhuma hizo zinazomkabili,".

Hata hivyo kwa mujibu wa habari kutoka katika vyanzo vyetu wafanyabiashara hao bado hawajakamatwa na kwamba bado jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka ili kuwaunganisha katika tuhuma hizo.

Watoa habari wetu walidokeza kuwa kutokana na unyeti wa tuhuma hizo hasa kwa kuzingatia kiwango cha pesa zilizoibwa, polisi wamehofu kumpa dhamana kituoni hapo kwa kudhani kuwa anaweza kutoroka na hivyo kusubiri afikishwe mahakamani kwanza.

Maelezo ya Polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alipoulizwa kuhusiana na taarifa za kukamatwa kwa mhasibu huyo alisema kuwa suala hilo haliko chini yake, bali liko ofisi ya Kanda Maalum, hivyo alilielekeza Mwananchi kuwasiliana na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda hiyo, (ZCO), Ahmed Msangi.

Hata hivyo ZCO Msangi alipotakiwa kutoa ufafanuzi alisema kwa upande wake yeye hawezi kulizungumzia, kwa maelezo kwamba si msemaji mkuu isipokuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Naibu Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova.

Naye Kova alipoulizwa alisema asingeweza kulitolea ufafanuzi kwa kuwa alikuwa nje ya ofisi na kwamba mahali alipokuwa hakukuwa na mawasiliano mazuri.

“Kwa sasa siko ofisni, niko nje kidogo ya jijini na mawasiliano huku si mazuri maana hata nakupata kwa shida, lakini kesho nitafanya Press Conference (mkutano wa waandishi wa habari) hivyo njoo kesho nitatoa ufafanuzi wa kutosha,” alisema Kova.
Habari za Kitaifa

Wizi kupitia mashine za Luku
Septemba 7, mwaka jana
Tanesco lilitanga kubaini kuwepo kwa mtandao wa wezi wa umeme kupitia mashine za Luku na vituo feki vya kuuzia umeme huo.

Kufuatia hali hiyo, shirika hilo lilianzisha operesheni endelevu ya kuwasaka wahusika wakiwemo watumishi wake wanaohisiwa kuhusika.

Katika siku ya kwanza ya utekelezaji wa operesheni mashine 7 kati 11 za Luku ambazo awali zilibainika kuwa na tatizo, zilihakikiwa katika maeneo ya Mwenge na Kariakoo zilihusishwa na wizi wa umeme.

Msemaji wa Tanesco, Badra Masoud alisema kupitia kitengo maalumu cha Luku kilichoanzishwa na shirika hilo walikuwa wakifuatilia taarifa za kuwepo kwa hujuma katika shirika hilo kupitia Luku na mita za kawaida, zinayofanywa na baadhi ya wafanyakazi halali wa shirika hilo.



CHANZO: MWANANCHI

AROBAINI YA DOKTA REMMY YAFANA


Familia ya Dokta Remmy wakiwasha mishumaa

Leo Januari 29 ni siku ya arobaini ya mwanamuziki galacha hapa nchini, Ramazan Mtoro Ongala ‘Dokta Remmy’ iliyofanyika nyumbani kwake Sinza na baadaye baadhia ya watu waliohudhuria walikwenda kufanya maombi katika kanisa la Christian Centre Sinza Palestina.
Baada ya zoezi hilo, walikwenda makaburini kwa ajili ya kuwasha mishumaa na kuweka mashada.



Mtoto wa marehemu aitwae Godfrey akigawa shada la maua kwa ndugu zake.


Mzee Makasi aliyevaa miwani akiongoza sala (katikati kushoto) ni mke wa marehemu, Toni na mtoto wake Godfrey.



Mtoto wa marehemu aitwae Amani mwenye ulemavu na wenzake wakifuatilia mambo yaliyojiri kwenye shughuli hiyo.


Watoto wa marehemu wakitupia kokoto juu ya kaburi.


Mke wa marehemu aliyevaa nguo nyeusi akitoa shukrani kwa waliohudhuria

MOTO UNAZIDI KUWAKA CAIRO


MOTO unazidi kuwaka Cairo, unasambaa pia. Tumeona picha za askari wale vijana wakitabasamu na kupeana mikono na wananchi. Ni ukweli, wengi wa wanajeshi hao wamekuwa recruited ( kuingizwa jeshini) wakitokea kwenye familia za kimasikini.

Kwa wanajeshi hawa, wana uelewa mkubwa wa wanachokipigania watu wa Misri. Ni suala la wakati tu kabla wanajeshi kuchukua uamuzi wa jumla wa kusimama upande wa umma. Na hilo likitokea, basi, mwisho wa zama za Hosni Mubarak utakuwa umeharakishwa, kwa nguvu ya umma ukisaidiwa na jeshi.

Maana, hata Hosni Mubarak akifanikiwa kuning’inia madarakani, bado, siku zake zitakuwa zikihesabika. Hosni Mubarak hana support ya umma, hivyo basi, hana uhalali wa kuendelea kuongoza dola kubwa na kongwe ya Egypt.

Watawala Afrika wana cha kujifunza?
Katika Afrika, mtawala atakayepuuzia moto unaowaka katika Dunia ya Waarabu ama ni mgonjwa au ni mjinga tu . Ni ukweli, kuwa Dunia ya Waarabu i-karibu nasi sana. Ni mwendo wa saa tano tu kwa ndege kutoka Dar es Salaam, Nairobi au Kampala kabla ya kutua Egypt, Tunisia, Yemen au Algeria. Ndio, ni umbali mfupi sana kabla ya aliye kwenye ndege kuanza kuuona moshi wa moto unaotokana na moto uliowashwa na umma unaotaka mabadiliko.

Ni dhahiri, kuwa yanayotokea kwenye Dunia ya Waarabu yana athari kubwa kwa ‘ Dunia Ya Waafrika’. Kihistoria na Kiutamaduni, Waafrika tuna mengi yanayotufanya tuwe karibu na Waarabu. Yaliyokuwa yakitokea Ulaya Mashariki miaka ile ya 80, ingawa yalisaidia kuleta mabadiliko pia barani Afrika, lakini, bado, yalitokea mbali na Afrika.

Lakini, harakati za vijana wa Kiarabu kuleta mabadiliko na hata kufanikiwa katika harakati zao, yana kila uwezekano wa kuwatia hamasa vijana wa Kiafrika katika nchi zao. Ikumbukwe, mengi wanayopigania vijana wa Kiarabu yanafanana na ya wenzao wa Afrika. Inahusu ukandamizaji, mgawanyo wa rasilimali wa haki na kukua kwa demokrasia ili kuchangie ustawi wa mataifa yao. Kupelekee kupata ajira na kuongeza vipato vyao. Kwa vijana hawa, kukua kwa uchumi wa nchi zao hakuna maana kama hali za watu wa kawaida zinakuwa ngumu kila kukicha na huku pengo la walio na wasio nacho likikua kwa kasi ya kutisha.

Kwa viongozi Afrika busara ni mapema kupunguza nywele zao kabla ya kulazimishwa kutia maji na kunyolewa vipara! Inahusu mabadiliko makubwa ya Katiba za nchi zetu ambazo bado zina ukakasi wa enzi za ‘ Chama Kushika Hatamu Zote’. Dunia Imebadilika. Angalia picha za matukio

Saturday, January 29, 2011

MISS UTALII TANZANIA YAWADIA

Washiriki wa Shindano la miss utalii wakifanya mazoezi ya viungo katika fukwe za Coco Beach jijini Dar es Salaam.

Warembo hao wakiwa kwenye pozi la kujiandaa kucheza mpira wa miguu.
Warembo wakicheza mpira katika moja ya mazoezi yao.

WAKATI Fainali za Taifa za Shindano la Miss Utalii Tanzania zimepangwa kufanyika usiku wa Februari 5,mwaka huu Mrembo atakayenyakua taji laTaifa la Miss Utalii mwaka huu ataondoka na faida kubwa ya zawadi ya mkataba wenye thamani ya shilingi milioni mia moja na hamsini.

Taarifa iliyotolewa na Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo imeeleza kuwa, shindano la mwaka huu litafanyika kwenye hoteli ya kitalii ya Kiromo View Resort iliyopo umbali wa kilometa kumi tu toka Bagamoyo mjini ambapo pia kutakuwa na burudani kadhaa zitakazosindikiza usiku huo adhimu na ya kihistoria katika tasnia nzima ya urembo na utalii hapa Tanzania.
Akaendelea kusema; washiriki wote wa fainali za Miss Utalii Tanzania 2010/11 wako katika hali nzuri kiafya na kisaikolojia kwa ajili ya shindano na kufafanua kuwa mbali ya kitita hicho kwa Malkia wa mwaka huu, warembo wengine wataweza kujitwalia mataji yatakayowakilisha hifadhi za taifa 16 zilizo chini ya mamlaka ya hifadhi za Taifa (TANAPA).
Kadhalika, Chipungahelo amesema kuwa mbali ya mataji ya hifadhi, pia, kutakuwa na tuzo zingine toka baadhi ya makampuni na taasisi zilizodhamini shindano hili ili kuyawakilisha katika suala zima la kuutangaza utalii kupitia hifadhi za taifa na utamaduni wa Mtanzania na hivyo kuongeza hamasa zaidi kwa washiriki ambao nao wameonesha kujawa shauku ya kufanya vema.

“Fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2010/11, zitakuwa tukio kubwa zaidi la kitaifa la kitamaduni na urembo nchini, ambalo kishindo chake kitaleta mageuzi makubwa katika sanaa ya urembo nchini, barani Afrika na duniani kwa ujumla. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa mara ya kwanza dunia itashuhudia idadi kubwa ya warembo wakiwa jukwaa moja wakitangaza na kuonesha utamaduni kupitia mavazi ya asili, ya kitalii, ya mitindo, ya ubunifu. Pia, warembo hao wataonesha vipaji vya kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za asili za mikoa au kanda wanazowakilisha,’ amesema Rais wa Miss Utalii Tanzania.
Aidha, amewataja wadhamini wakuu wa shindano la taifa la Miss Utalii 2010/11 ni Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,Business Times Limited, Kiromo View Resort na Sahara Media Group Limited,inayomiliki kituo cha runinga cha Star TV, Radio Free Africa, Kiss FM na gazeti la Msanii Afrika. Wengine ni Zizzou Fashion, Alaisy Travel, Auckland Tours, Tintona TankStation, Tesco Furniture, Mlonge By Makai Enterprises,Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Coco Beach.
Warembo hao wameanza ziara rasmi za kutembelea na kutangaza vivutio vya utalii ,kwa kutembelea maeneo ya kihistoria yaliyopo Mkoani Pwani,ambapo juzi walitembelea Maeneo ya Kihistoria yaliyopo wilayani Bagamoyo ikiwemo Magofu ya Kaole,wakiongozwa na katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo. Aidha jana warembo wote 60 walitembelea na kutangaza Fukwe za Bahari ya Hindi zilizoko mkoani Dar Es Salaam wakiongozwa na Mbunge wa Kinondoni Mh, Idd Azan. wakiwa katika Fukwe wa Coco Beach warembo hao wakiwa wamegawanywa katika timu nne za mpira wa miguu walishindana kusakata kabumbu la Ufukweni hali iliyopelekea kuwa kivutio kikubwa na kusababisha ufukwe huo kufurika mamia ya watu wakishuhudia warembo hao wakionyesha vipaji vya hali ya juu ya kusakata kandanda.
michuano baina ya timu hizo za warembo zilizopewa majina ya hifadhi za Taifa ulikuwa mkubwa na kuamsha shangwe za mara kwa mara kwa wapenzi waliojazana kushuhudia mechi hizo. katika mchezo wa kwanza timu ya soka ya warembo wa Ngorongoro iliweza kuibwaga timu ya soka ya Selous kwa mabao 4-2 wakati katika mchezo wa pili ambao ulizikutanisha timu za Serengeti National Park dhidi ya Maunt Kilimanjaro na matokeo timu ya Mlima Kilimanjaro kuibuka kwa ushindi wa mabao 3-1. Mbunge wa Kinondoni Mh, Idd Azan kwa kufurahishwa na viwango vilivyoonyeshwa na timu hizo za warembo wa miss Utalii Tanzania 2010- 2011 ambao tarehe 5 mwezi wa pili watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Utalii Tanzania 2010- 2011 katika Hotel ya Kitalii ya Kiromo Bagamoyo, alinunua kila goli kwa shilingi elfu kumi(10,000) hivyo aliweza kutoa shilingi laki moja kwa magoli kumi yaliyofungwa. naye mfanyabiashara maarufu nchini Zizzou Fashion alitoa seti nne za jezi kwa warembo wote 60.

TUNZO ZA MUZIKI WA INJILI ZA LINDIMA

Balozi wa ZindukaProfesa Jay, akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu Tamasha la Tuzo za wasanii wa mziki wa Injili linalotarajiwa kufanyika februali 27 Kulia ni Mratibu wa Tamasha hilo, Haris Kapiga.

TANZANIA Gospel Promoters (TGMP) kwa mara nyingine tena baada ya miaka mitano kupita wameandaa tamasha la Tunzo za Muziki wa Injili (Gospel Music Awards) lililopangwa kufanyika Februari 27 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo asubuhi katika mkutano na waandishi wa habari Mratibu wa Tamsha hilo Haris Kapinga kutoka Kampuni ya Clouds Media Haris Kapinga alisema tamasha hilo litatumika kuwapongeza na kufanya tathmini ya jumla kwa wasanii binafsi na tasnia nzima huku Tunzo mbalimbali zitatolewa.
Tunzo hizo ni wimbo bora wa mwaka, mwandishi bora wa mwaka, mwimbaji bora wa kike wa mwaka, mwimbaji bora wa mwaka wa kiume, kundi bora, msanii bora wa muiziki wa Injili wa mwaka na mwimbaji anayechipukia katika uimbaji wa nyimbo za Injili.
Wimbo wa mwaka, video bora, Mtayarishishaji bora wa mziki wa video wa mwaka , Mtayarishaji bora wa muziki, Tunzo ya Jumuiya, Kwaya bora ya Akapela,Kwaya bora inayotumia ala, bendi bora ya muziki wa Injili, Kwaya bora inayotumia ala ya Piano.
“Jinsi watu watakavyoweza kupiga kura, kura zitaanza kupigwa Januari 29 mwaka huu na kufikia kilele cha February 12 huku fomu zote zilizopigiwa kura zitatakusanywa Februari 13” alisema Kapinga.
Anaendelea kwa kusema kuwa mdhamini mkuu wa tamasha hilo ni Mradi wa kutokomeza Malaria , Zinduka ambao zaidi ya lengo kuu la kupambana na Malaria inatumia tamasha hili kuwaunganisha viongozi wa dini mbalimbali kwa kuanza na madhehebu ya dini ya Kikristo ili kupeleka ujumbe kuhusiana na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.
Tangu Mradi huo ulipoasisiwa nchini mwaka 2010 umekuwamradi wa kwanza unaofanya kazi kwa kushirikiana na sekta mbalimbali katika jamii ili kusimamia pamoja na kumaliza ugonjwa wa Malaria nchini kote.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa dini ambao ni Sister Mariana Francis kutoka Roman Catholic, Mchungaji David Mwasota ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Makanisa ya Kipentekoste, Mchungaji Solomon na John Gao wa Makanisa ya Anglican, ambao wote kwa pamoja wamewakumbusha wana jamii na kuwahimiza Watanzania katika kujilinda, kuepukana na vifo vinavyoweza kuzuilika.
“Tunaimani kwamba kwa kutumia nguvu ya muziki wa Injili , mwamko na ufahamu kwenye jamii vitaongezeka sana huku jamii na waumini wakiunganisha nguvu ya kupambana na Malaria” alisema Mwasota.

IDADI YA WAGONJWA WA UKOMA YAPUNGUA NCHINI

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hadji Mponda.




SERIKALI imesema hali ya maambukizi na idadi ya wagonjwa wa Ukoma nchini inaendelea kupungua mwaka hadi mwaka kutokana na juhudi mbalimbali zinazochukuliwa kukabiliana na ugonjwa huo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salam na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda wakati akitoa Tamko kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukoma Duniani ambayo kitaifa itafanyika mkoani Lindi.
Amesema idadi ya wagonjwa wa Ukoma imepungua kutoka wagonjwa 35,000 mwaka 1983 hadi kufikia wagonjwa wapatao 2,600 kwa mwaka 2009 huku takwimu za mwaka 2009 zinaonyesha kuwa ,asilimia 11 ya wagonjwa wapya waliogunduliwa tayari walikuwa wamekwishapata ulemavu wa kudumu.
“Wagonjwa wengi wamekuwa wakipata madhara ya ugonjwa wa Ukoma kutokana na kuchelewa kwenda kwenye vituo vya afya kwa uchunguzi na matibabu” Amebainisha.
Ameeleza kuwa takwimu za mwaka 2009 zinaonyesha kuwa hali ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukoma bado ni kubwa katika mikoa ya Lindi wagonjwa 176, Rukwa wagonjwa 376, Dar es salaam wagonjwa 386 na mkoa wa Mtwara ambao una wagonjwa 175.
Amesema kuwa serikali kwa kutambua athari za ugonjwa huo na umuhimu wa kuzuia ulemavu utokanao na ukoma imeweka msisitizo kupitia kauli mbiu ambayo ni “Pambana na Ulemavu Utakanao na Ukoma” ili kuhimiza ushiriki wa jamii nzima katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukoma.
“Ninapenda kuwahimiza wananchi wote kuwa wakiona dalili za ugonjwa wa ukoma ambazo ni baka au mabaka kwenye ngozi yasiyo na hisia ya mguso ambayo huambatana na ganzi kwenye mikono na miguu wawahi kwenye vituo vya tiba kwa ajili ya uchunguzi na kupatiwa matibabu sahihi ya ugonjwa wa ukoma ambayo hutolewa bila malipo”
Dkt. Mponda ameongeza kuwa serikali imekuwa ikiwahudumia waathirika wa ugonjwa wa ukoma ikiwemo kugharimia jozi za viatu maalum 7000 kila mwaka kwa wale walioathiriwa na ukoma bila malipo ili kuzuia athari na kupunguza ulemavu utokanao na kuharibiwa kwa mishipa ya fahamu, huduma za marekebisho ambazo ni pamoja na huduma za upasuaji, viungo bandia, magongo na viti mwendo .
Aidha ametoa wito kwa jamii kutowanyanyapaa wala kuwatenga wagonjwa wa ukoma kutokana na mila potofu na ukosefu wa uelewa kuhusu ugonjwa huo huku akisisitiza kuwa mtu ambaye yupo kwenye matibabu hata kama ana ulemavu hawezi tena kuambukiza ugonjwa huo na anastahili kuishi katika jamii.

Kwa upande wake Meneja wa Programu ya kupambana na Ugonjwa wa Ukoma nchini Dkt.Said Egwaga amefafanua kuwa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea kupambana na ugonjwa huo huku akibainisha kuwa dawa za matibabu kwa ajili ya wagonjwa zinapatikana tofauti na miaka ya nyuma ambapo wagonjwa waliwekwa kwenye kambi maalum.
“Miaka ya nyuma hakukuwa na tiba ya ukoma tulikuwa na kambi maalum kwa ajili ya waathirika lakini sasa wagonjwa wa ukoma hawapelekwi tena kwenye kambi isipokuwa hupewa dawa ambazo huzitumia majumbani mwao”
Ameongeza kuwa Wizara kupitia kitengo cha Ustawi wa jamii imekuwa ikiwaangalia waathirika wa ukoma wakiwemo walemavu kwa kuwapatia misaada ikiwemo ujenzi wa makazi yao na kuwasaidia katika shughuli za kilimo.
Siku ya Ukoma Duniani iliasisiwa takribani miaka 56 iliyopita kwa lengo la kuielimisha jamii kuhusu ugonjwa wa ukoma na huadhimishwa ulimwenguni kote kila jumapili ya mwisho wa mwezi januari kila mwaka.

Aron Msigwa/Habari maelezo

Tanzania committed to the planned tarmac highway around the Serengeti National Park

President Jakaya Kikwete speaks in Davos today


Tanzania has reiterated its position on the planned tarmac highway around the Serengeti National Park to ease transport problems facing poor communities surrounding the Park, saying it will still go ahead and build the road.

However, contrary to what groups lobbying against the planned highway have been claiming, the Government insists the highway will not be built through the Serengeti, which has been acclaimed internationally as the World Heritage Site.

The Government position was articulated yesterday (Thursday, January 27, 2011) by the President of the United Republic of Tanzania, His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete during his bilateral talks with the Managing Director of the World Bank, Ms. Ngozi Ikonjo-Iweala at the margins of the World Economic Forum (WEF), which both the President and Mrs.Ikonjo-Iweala are attending in Davos.

“Contrary to what some people are saying, and to the rumors being circulated everywhere, my Government has never decided to build a tarmac road through the Serengeti,” President Kikwete told Ms Ikonjo-Iweala.

President Kikwete told the World Bank Managing Director that the Government plan seeks to severely reduce the length of the current road passing through the Serengenti National Park.

He said that currently a 220-kilometre unpaved road was running through the Serengeti and that the Government want to reduce it to only 54 kilometres that will pass through the National Park and those 54 kilometers will remain unpaved.

“Currently, 220 kilometers of road are passing through Serengeti National Park, right in the middle of the Park. And there is huge traffic crossing the park with large lorries and huge buses. We are unhappy with this situation. We want to reduce the length of road going through the Serengenti to only 54 kilometers passing mainly through the northern tip of the Park,” said President Kikwete.

He added: “This planned highway will meet three major objectives. One, is to reduce the flow of traffic passing the Park. Second, is to reduce the length of the road running through the Serengeti and third is to empower those poor communities living just outside the Serengeti to have a reliable road going through their area.”

“Some of the accusations against the Tanzania Government on this issue are quite absurd. People sit in Dar es Salaam and listen to all these people and institutions which are paid to say bad things about the Government, said the President and added:

“ Tanzania has the most impeccable record in conservation in the world. About 20 per cent of our land has been under conservation since our independence in 1961. We are a leading nation in conservation in the world. How, then can we make decisions that would destroy the Serengeti? We would be the last people to destroy the Serengeti.”

President Kikwete has advised those who are interested in getting accurate facts about Government plans on the road supporting poor communities surrounding the Serengeti National Party to talk to the right people.

“We have a responsibility to our people. They need a road and we will deliver it to them while fully preserving our beloved Serengeti National Park,” said President Kikwete in relation to the long-running campaign against this road mainly by non-governmental organizations (NGO’s) and some conservation groups.

Friday, January 28, 2011

MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA ISRAEL NAIROBI

Waziri wa Ujenzi Dr. John Magufuli (kulia) akizungumza na Balozi wa Umoja wa Ulaya (European Union) Tim CLARKE wakati alipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni jijini Dar es Salaam ambapo walizungumzia masuala mbalimbali ya miradi ya barabara inayogharamiwa na Jumuiya ya Ulaya. (EU) hususani maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mandela.Picha na Hisani ya Kitengo cha Habari na Mawasiliano- Wizara ya UJENZI.
Waziri wa Ujenzi Dr. John Magufuli akiongea na Balozi wa Israel kwa nchi za Afrika Mashariki ambae ofisi yake ipo Nairobi Kenya Jacob Keidar hivi karibuni alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.Mazungumzo hayo hususani Israel kujenga nyumba nafuu nchini Tanzania kwa gharama nafuu kwa ajili ya wafanyakazi Serikalini pamoja na Taasisisi.
SHIRIKA LA NDEGE LA QATAR LAPANUA WIGO NA KUBORESHA HUDUMA ZAKE AFRIKA MASHARIKI

Safari za mara kwa mara za nchini Kenya na Tanzania na nyongeza ya safari 12 kwa wiki, kwenda Nairobi mara mbili Kwa siku, safari tano zaidi kwa Dar es Salaam.

Shirika la ndege la Qatar leo limetangaza kupanua mtandao wake wa Afrika Mashariki kwa kuongeza safari 12 zaidi kupitia miji mikuu miwili – Dar es Salaam na Nairobi.

Mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam, hivi sasa una huduma kila siku, kupata nyongeza ya safari nne kwa wiki kutoka mwezi Januari. Safari za nyongeza kuanzia Februari 14 zitachukua mzunguko hadi wiki 12 za huduma.

Safari za kila siku kutoka Nairobi kwenda Doha zimeongezeka hadi kufikia safari 12 kwa wiki. Kuanzia tarehe 3 mwezi Januari safari za nyongeza mbili zitachukua nafasi hadi mara mbili kwa siku.

Safari zote zinatolewa na ndege aina ya A320 zikiwa na viti 12 vya daraja la pili na viti 132 daraja la tatu.

Bara la Afrika ni mojawapo ya soko kubwa la Shirika la ndege la Qatar kwa idadi ya vituo linavyohudumia na mji pekee kutengeneza zaidi ya asilimia10 ya mtandao wa kimataifa wa shirika hilo.

Shirika la ndege la Qatar hivi sasa linasafiri katika miji 14 Afrika, ikiwemo Alexandria, Aljeria, Misri, Luxor, Casablanca, Cape Town, Johannesburg, Khartoum, Lagos, Nairobi, Dar Es Salaam, Shelisheli, Tripoli na Tunisia.

Kutoka kila mji, Shirika linatoa ofa kwa kupitia kiungo chake cha Doha kufikia vituo vingi kwenye mtandao wake Ulaya, Mashariki ya kati, Asia kusini na kaskazini pamoja na Amerika ya kusini.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ndege la Qatar Bw. Akbar Al Baker alisema "Tunayo furaha kutambulisha upatikanaji wa safari za nyongeza kwa Afrika na kutoa ofa kubwa ya kwa abiria kuchagua ndege kutoka na kwenda kwenye miji.

“Kama sehemu ya mkakati wa ukuaji wetu, tunaendelea kupiga hatua mbele katika safari za mara kwa mara, katika vituo ambapo ni hatua madhubuti kuongeza ukuaji wetu katika nyanja za biashara na Utalii.

“Safari ya Dar es Salaam limefanya vizuri zaidi kwa kipindi cha miaka mine iliyopita ambapo ilizinduliwa mwezi Januari mwaka 2007”

“Mara kwa mara tumekuwa tukihudumia Nairobi tangu mwezi Novemba mwaka 2005 na hii imekua moja ya historia ya mafanikio makubwa Afrika, kwa hiyo tunayofuraha kuwapatia abiria wetu nafasi zaidi kwa kuongeza safari hadi kufikia mara mbili kwa siku,” aliongeza.

Zaidi ya miezi minne ijayo, ukuaji wa shirika utalenga Ulaya likiwa na vituo vipya vinne vitakavyotambulishwa– Budapest (Januari 17), Bucharest (Januari 17), Brussels (Januari 31), na Stuttgart (Machi 6), kabla ya kuzindua kituo chake cha 100 kwa mji wa Syria wa Aleppo tarehe 6 Aprili.

Hivi karibuni shirika linaendesha safari zake za ndege 93 katika vituo vikubwa vya biashara kupitia Ulaya, Mashariki ya kati, Afrika, Asia Pacific, Amerika ya kaskazini na Kusini. Kituo kipya kilichoongezwa ni Meditterrania ya Ufaransa tarehe 24 mwezi Novemba.

Kufikia mwaka 2013 Shirika la ndege Qatar linapanga kutoa huduma katika vituo 120 ulimwenguni likiwa na lengo la wastani wa ndege 120 kwa kipindi cha miaka mitatu.

Ratiba ya safari mpya za Afrika Mashariki

DAR ES SALAAM - DOHA
Jumatutu, Jumatano, Alhamisi na Jumapili – kuanzia Januari 2
Kuondoka Dar Es Salaam QR547 saa 1815, kufika Doha saa2350
kuondoka Doha QR546 at 1120 saa, kufika Dar Es Salaam saa 1715

Jumamosi – kuanzia Februari 14
Kuondoka Dar Es Salaam QR547 saa 1815, kufika Doha saa 2350
Kuondoka Doha QR546 saa 1120, kufika Dar Es Salaam saa1715

NAIROBI - DOHA
Jumatatu, jumatano, Alhamis, Jumamosi na Jumapili
Kuondoka Nairobi QR535 saa 1850, kufika Doha saa 2345
KUondoka Doha QR534 saa 1230, kufika Nairobi saa 1750

Jumanne na Ijumaa – kuanzia Januari 2
Kuondoka Nairobi QR535 saa 1850, kufika Doha saa 2345
Kuondoka Doha QR534 saa 1230, kufika Nairobi saa 1750

2O% ATUNUKIWA GITAA NA PRODUCER WAKE

MWANDAAJI wa muziki, John Water (kushoto) akimkabidhi zawadi ya Gitaa aina ya Aucustic lenye thamani ya Sh. 200, 000, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abas Hamis ’20%, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa msanii huyo anayeendelea kufanya vizuri katika anga za muziki wa Bongo Flava. Makabidhiano hayo yalifanyika jana kwenye Duka la City Music Sound lililopo Mtaa wa Uhuru Dar es Salaam.

Msanii huyo 20% akijaribu kupiga gitaa lake baada ya kukabidhiwa.

Picha: Sufianimafoto blog.

AIRTEL, KUKUTANISHA MAKAPUNI ZAIDI YA 40, KWENYE BONANZA LAO LA FEBRUARI 12 MWAKA HUU

Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino wa Kampuni ya Airtel Tanzania Beatrice Singano (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tamasha la Wanahabari linalotarajiwa kufanywa na kampuni hiyo Februari 12 mwaka huu, Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Mutta Muganyizi.
KAMPUNI ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania imeandaa Tamasha la waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari litakalofanyika Februari 12 mwaka huu katika viwanja vya Posta na Simu Kijitonyama, Dar es Salaam.
Hatua hii ya Airtel ni katika kutambua umuhimu wa tasnia ya habari nchini lakini pia ni hatua ya kuimarisha uhusiano wa kikazi baina ya pande hizi mbili zinazotegemeana katika utendaji wao wa kila siku.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano alisema hatua hiyo ni ya kuimarisha ushirikiano baina ya pande mbili hizo na kwamba bonanza hilo litaziwezesha pande mbili husika kufahamiana zaidi.
Alisema wanahabari wamekuwa na mchango mkubwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii na kwamba Airtel wameona ni kitendo cha uungwana kwao kuonyesha thamani waliyonayo wanahabari kwa kukutana na kuburudika kwa pamoja kupitia michezo.
“Ni kawaida katika kila mwisho au mwanzoni wa mwaka kufanya tathimini ya jumla ya pale tulipo na wapi tunakwenda lakini pia huwa tunakitumia kipindi hiki kukaa na kufurahi kwa pamoja na watu wenye majukumu tofauti katika kulijenga taifa ambapo miongoni mwao ni nyinyi wanahabari,” alisema.
Aliongeza kuwa pamoja na burudani tofauti pia kutakuwa na michezo mbalimbali ya kubahatisha ambapo wanahabari wataweza kujishindia zawadi tofauti kutoka Airtel.
Kampuni ya Capital- Plus International (CPI) ndio waratibu wa tamasha hili ambapo Mratibu Mawazo Waziri aliitaja michezo itakayohusika kuwa ni pamoja na mpira wa miguu ikihusisha timu ya watu saba kila upande, pete,kuvuta kamba na kuruka kwa magunia ambapo katika burudani kutakuwa na mashindano ya kuimba na kucheza dansi.
Alisema taratibu nyingine kuelekea katika tamasha hilo zitaendelea kutolewa kadri siku zitakavyosonga ambapo aliahidi wanahabari kupata burudani ya kipekee katika tamasha hili la aina yake katika medani ya Habari.
“Airtel chini ya uratibu wetu imedhamiria kuwapa wanahabari burudani ya kipekee kwani mchango wenu kwao pia umekuwa wa kipekee,” alisema Waziri.

DOWANS YAWASILISHA OMBI LA USAJILI MAHAKAMA KUU

Kampuni ya Dowans leo imewasilisha rasmi maombi ya madai ya usajili wa TUZO katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam na kusajiliwa kwa kupewa namba ya usajili nane ya mwaka huu.

Kampuni ya Dowans ilishinda kesi ya madai dhidi ya TANESCO katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na kuamuliwa TANESCO kumlipa Dowans Sh Bilioni 94.

Naibu msajili mwandamizi wa mahakama hiyo Mh. Salvatory Mwongole,ameiambia Globu ya Jamii kwamba maombi hayo yameifikia mahakama hiyo januari 25 mwaka huu na yamewasilishwa na wakili wa kampuni hiyo hapa nchini kutoka kampuni ya uwakili ya Kennedy Fungamtama.

Mh. Mwongole amesema maombi hayo yamekwishapangiwa jaji lakini kulingana na unyeti wa suala hilo jina la jaji linahifadhiwa kwa sababu ndio kwanza ameteuliwa kushughulikia maombi ya usajili huo na jalada halijamfikia.

Alisema maombi hayo ya usajili yameombwa na kampuni ya Dowans Holdings S.A na Dowans Tanzania dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kwa mujibu wa sheria TUZO hiyo haitasajiliwa hadi mahakama itoe nafasi kwa mdaiwa kuwasilisha pingamizi kupinga usajili wa Tuzo hiyo kama anaona haifai kusajiliwa, na kama hana pingamizi itasajiliwa kama imekidhi sheria na mdaiwa kulazimika kulipa fedha hizo.

Wadau wengine pia wana nafasi ya kuwasilisha maombi yao kama wanadhani usajili wa TUZO hiyo haustahili nayo pia yatapokelewa, Mahakama ikishasikiliza kama kuna mapingamizi itatoa maamuzi kama ni kuisajili au la.

REDSUN,JOH MAKINI,BELL 9 NA BEKA KUKAMUA USIKU WA VERSITY NITE NEW MAISHA CLUB

Msanii Swabri Mohamed (Redsun) kutoka nchini Kenya akifafanua jambo mapema leo asubuhi kuhusiana na shoo yao kabambe ya Versity Nite ambayo itawakutanisha wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu itakayofanyika leo usiku ndani ya New Club Maisha,jijini Dar.Redsun ameahidi kufanya kamuzi kubwa kwenye shoo hiyo.
Msanii wa kizazi kipya Bakari Hassan (Beka Boy) akizungumza na vyombo vya habari mapema leo asubuhi ambaye pia atashiriki kwenye shoo ya Versity Nite itakayofanyika usiku leo ndani ya New Club Maisha,kushoto kwake ni Msanii kutoka nchini Kenya,Swabri Mohamed (Redsun) akifurahia maelezo ya Beka Boy.ukiachilia wasanii hawa,wengine ni Joh Makini pamoja Belle 9 ambao kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao hawakuweza kutoka katika mkutano huo na wanahabari.

MWANAMUZIKI WA MSONDO AFARIKI DUNIA


Malik enzi za uhai wake.
Mwanamuziki wa Bendi ya Msondo Music, Hamis Malik maarufu kama Super Malik, leo asubuhi amefia Hospitali ya Anglikan iliyopo Buguruni Malapa jijini Dar baada ya kukimbizwa hapo alipopatwa na homa kali.



Malik (kulia) akiwajibika jukwaani na wanamuziki wenzake wa bendi hiyo.

MIYEYUSHO NA FUNDI KUKAMUANA KESHO


Bondia Juma Fundi (kushoto) akipimwa afya kabla mpambano.
MABONDIA Francis Miyeyusho na Juma Fundi, kesho wanatarajia kupambana katika mchezo wa raundi 10 utakaofanyika katika Ukumbi wa Amana Vijana Social Jijini Dar es Salaam. Leo mchana paparazi wetu aliwanasa mabondia hao ukumbini hapo wakiwa kwenye hatua za mwisho za mpambano huo ikiwemo kupima afya zao.



Francis Miyeyusho (kushoto) na Fundi wakitunishiana misuli.

Promota wa pambano hilo, Kaike Siraj (katikati) akiwainua mikono juu mabondia hao kuwatakia mchezo mwema.

Aliyewahi kuwa mshindi wa Shindano la Bongo Star Search (BSS),Jumanne Idd naye alinaswa eneo la tukio na kudai atawatumbuiza mashabiki kabla ya mpambano huo.

HAYA NDO' MALEZI BORA YA BABA NA MAMA

USTADHI mmoja (pichani) jana mchana analinaswa na kamera yetu mjini Morogoro akiwa amembeba mtoto wake mgongoni na upande wa kitenge akiwa anaendesha baiskeli kuelekea sehemu ambayo haikufahamika.

Hii inaonyesha jinsi jukumu la kutunza mtoto linavyotakiwa kuwa la wazazi wote – baba na mama.



POLISI WAPUNGUZIWA MSOSI

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, (IGP) Said Mwema.

SERIKALI imeondoa posho ya upepelezi na nyumba kwa askari polisi bila maelezo katika mishahara ya miezi ya Desemba 2010 na Januari mwaka huu, Mwananchi limebaini.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa, posho hizo zitaendelea kukatwa kwani baadhi ya askari waliokwishapata mshahara wa Januari, wamesema fedha hizo hazipo.

Baadhi ya askari polisi walilithibitishia Mwananchi kuhusu kukatwa kwa mishahara yao, huku taasisi husika za serikali ambazo ni polisi makao makuu na hazina, wakirushiana mpira kuhusu suala hilo.

"Ni kweli tumekatwa posho zetu zote na tatizo hilo limeanza mwezi huu," askari mmoja wa mkoani Ruvuma alilieleza gazeti hili.

Askari mwingine aliyefika kwenye ofisi za gazeti hili jana alisema anasikitishwa na hatua hiyo kwani imeharibu bajeti yote aliyoiweka kwa mwezi Januari.

"Haya mambo ya ajabu sana, watu wamekatwa posho tena bila maelezo, wanataka askari sasa waanze kuwabambikia raia kesi ili kujiongezea kipato?"alisema.

Polisi huyo alidai kuwa katika mshahara wake wa mwezi Desemba mwaka jana, alikatwa Sh150,000 jambo ambalo limemfanya akope kwa ajili ya kuwapeleka watoto shule.

"Kukatwa posho bila maelezo ni ngumu sana na kimsingi hii inatupa shida kubwa kuzoea mazingira mapya, inaonekana hawa watu wanakata pesa zetu ili wawalipe Dowans (kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyozua zogo kutokana na mkataba tata),"alisema.

Hata hivyo kukatwa kwa fedha hiyo kumeibua utata hasa baada ya uongozi wa jeshi la polisi kutupiana mpira na Wizara ya Fedha walipotakiwa kutoa maelezo kuhusu suala hilo.

Wakati polisi ikisema yenyewe haihusiki na malipo ya askari wake, Wizara ya fedha na uchimi ilisesema inaandaa malipo ya wafanyakazi kulingana na maelekezo ya mwajiri husika.

Msemaji wa polisi, Advera Senso aliliambia gazeti hili jana kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo kwani malipo ya polisi yanafanywa na Wizara ya Fedha (Hazina).

“Hilo suala ungewauliza watu wa Wizara ya Fedha kwa sababu sisi sio watu tunaotoa mishahara,”alisema Senso na kuongeza kuwa wao huandaa malipo kisha kuyapeleka hazina kwa ajili ya malipo.

Naye Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ingiahedi Mduma, alisema kuwa wizara haihusiki na suala la kupanga mishahara ya watu.

"Tunacholipa wafanyakazi ni maagizo yanayotoka kwa mwajiri," alisema Mduma.

Kwa mujibu wa Mduma jeshi la polisi haliko chini ya Wizara ya Fedha bali Ofisi ya Rais - Manejimenti ya Utumishi wa Umma, kwa hiyo mishahara inayopangwa kutoka Utumishi, ndiyo inayolipwa na Hazina.

“Sisi ni kama mawakala tu suala la kulipa mishahara linatokana na mipango iliyotolewa na Utumishi na Jeshi hilo, kwa hiyo hatuwezi kubadilisha chochote tunacholetewa,”alisema.

Lakini Mduma alidokeza kuwa kuna uwezekano wa baadhi ya polisi ambao hawajalipwa fedha za pango kuwa tayari wamepewa nyumba za kuishi.

“Inategemea kama hao polisi hawajalipwa inawezekana tayari wamegawiwa nyumba kwa hiyo kile kiasi walichokuwa wanapewa kwa ajili ya makazi kimefutwa,"alisema na kuongeza:

"Au fedha za pango walizokuwa wakilipwa walikuwa wakilipwa kwa makosa. Kama ni hivyo basi, itabidi wakatwe kwa muda wote ule waliokuwa wakiingiziwa fedha hizo, hadi deni litakapomalizika.”

Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo jana, Kamishna wa Utawala na Rasilimali wa Jeshi la polisi, Clodwig Mtweve alisema anahitaji muda kulifuatilia.

Alisema, "Ndio kwanza umeniambia, sasa ngoja niwasiliane na kitengo cha mishahara nijue tatizo ni nini." Mtweve aliahidi kuwa atatoa maelezo ya suala hilo leo.

Alipotafutwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Nahodha hakuweza kupatikana na baadaye katika mawasiliano ya simu haikupatikana, lakini msaidizi wake alisema kuwa waziri alikuwa safarini Indonesia kufuatilia shughuli za uanzishwaji mradi wa vitambulisho vya taifa.


Polisi ni miongoni mwa kada za watumishi wa umma ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikilalamikia mishahara midogo, huku malipo hayo yakielezwa kuwa kichocheo cha kukithiri kwa vitendo vya rushwa ndani ya chombo hicho cha usalama wa raia.

Ripoti ya utafiti uliofanywa na Tasisi ya Wanaharakati wa Maendeleeo barani Afrika (ForDIA) na kutolewa Januari 18, mwaka huu inaonyesha kuwa Idara ya Polisi ni kinara wa rushwa ikizitangulia idara nyingine za serikali ambazo ni Afya na Mahakama.


Kwa mujibu Fordia, polisi inaongoza kwa kupokea rushwa, huku sekta za Afya, Mahakama, Elimu, Tanesco na idara za leseni na ushuru zikitajwa pia kuwa na kiwango kikubwa cha rushwa.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Bubelwa Kaiza alisema “polisi ndio vinara wa rushwa kwa sasa”.

Alisema utafiti huo unaonyesha kuwa polisi wanaongozwa kwa asilimia 81.9 kwa kupokea na kutoa rushwa. “Polisi imeendelea kushika nafasi ya kwanza baada ya kuongoza idara nyingine kwa kuwa na asilimia 85.3 mwaka jana kutoka nafasi ya pili ya asilimia 75.8 waliyokuwa wakiishikilia mwaka 2009,’’alisema Bubelwa.

Kwa mujibu wa Fordia utafiti huo ulifanyika katika mikoa 11 ya Tanzania ambayo ni Dar es salaam, Tanga, Kagera, Manyara, Rukwa, Tabora, Kilimanjaro, Mwanza, Mara, Pwani na Mtwara.

Utafiti huo pia umejumuisha serikali za mitaa 47 katika wilaya tofauti nchini na kulishirikisha watu mbalimbali wapatao 1,122 ambao waliulizwa maswali, lengo likiwa kujua kinara wa rushwa nchini.

Kati ya watu hao 1,122 waliohojiwa wanaume walikuwa 646 na wanawake 476. Hata hivyo watu walioweza kutoa majibu walikuwa 367, ambapo wanaume walikuwa 248 na wanawake 119, huku Bubelwa akieleza kuwa watu waliohojiwa ni wanaoishi mijini na vijijini.

Alisema sula la umri lilizingatiwa katika kuwahoji watu ambapo, waliohojiwa wote walizidi miaka 18, hivyo utafiti huo kuhusisha vijana, wazee na watu wenye umri wa kawaida.

Alifafanua kuwa walipata majibu na maoni mbali mbali kutoka kwa wananchi kuhusu suala la polisi ambapo walielezwa kuwa watu hukamatwa kwa uonevu na hulazimika kutoa 'kitu kidogo' (rushwa), ili waachiwe hata kama hawakuwa na makosa, ambapo pia watu wenye makosa wanapofikishwa polisi huachiwa baada ya muda mfupi kutokana na kutoa kitu kidogo.

Alisema lengo la utafiti huo ambao ulifanyika kwa nchi nzima ilikuwa ni kuanzisha majadiliano ili kuonyesha uelewa kwa wananchi na kuipa changamoto serikali juu ya mapambano ya rushwa.

CHANZO: MWANANCHI

Wednesday, January 26, 2011

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA SEMINA YA WABUNGE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipeana mikono na na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda katika Ukumbi wa mikutano Ubungo Plaza alikoenda kufungua Semina elekezi ya siku 10 kwa Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akifunguwa Semina Elekezi ya siku 10 kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoanza leo katika ukumbi wa Hoteli ya Ubungo Plaza Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipunga mkono kuagana na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kufunguwa Semina elekezi ya siku 10 kwa Wabunge hao katika ukumbi wa Hoteli ya Ubungo Plaza leo.

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA RUAHA (University College),WAGOMA

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa chuo cha Ruco wakiwa katika mgomo leo wakishinikiza bodi ya mikopo kuwaingiza fedha zao za kujikimu kiasi cha shilingi 300,000 kama ilivyokuwa katika vyuo vya Mkwawa cha Iringa na UDOM cha Dodoma hivi karibuni.

TWANGA, WANAUME HALISI KUKAMUA SAUTI ZA BUSARA

Msanii Juma Nature akiwa na Kiongozi wa African Stars 'Twanga Pepeta' Lwiza Mbuttu mara tu baada ya mkutano wa waandishi wa habari na waandaji wa tamasha la Sauti Za Busara jijini Dar leo. Sir Nature atakuwepo Sauti za Busara kwa mara ya pili wakati Twanga watakuwa Zenji kwa mara ya kwanza kwenye tamasha hilo. Chini ni video ya Lwiza Mbuttu akiongelea mipango ya Twanga k.

KESI YA MURO YAFIKIA PATAMU

MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Kisutu imepokea pingu, miwani na hati ya upekuzi katika kesi ya kuomba rushwa ya sh milioni 10 inayomkabili aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) Jerry Muro kama kielelezo cha ushahidi katika kesi hiyo.Vielelezo hivyo viliwasilishwa jana mahakamani hapo na Ofisa wa Polisi dwani Nyanda ambaye ni shahidi wa sita katika kesi hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Gabriel Mirumbe.Shahidi huyo aliieleza Mahakama kuwa Januari 29, mwaka 2010 akiwa ofisini kwake alipokea maagizo kutoka kwa mkuu wake wa kazi Kamishina wa Upelelezi Charles Mkumbo akimtaka kufanya upekuzi katika gari yenye namba za usajili T 545 BEH mali ya Jerry Muro.Alidai alishuka kwenda kulifuata gari hilo lililokuwa limepaki kwenye maegesho ya magari ya kituo kikuu cha polisi kati akiwa na mlalamikaji Michael Wage pamoja na mashahidi wengine ili kushuhudia zoezi la upekuzi huo.“Wage aliyekuwa analalamika kutishiwa kuuawa na Muro alikuwepo makusudi ili kuitambua miwani yake aliyodai kuisahau katika gari ya Muro siku aliyokamatwa na pingu aliyodai kutishiwa kufungwa nayo.“Baada ya upekuzi huo vitu vyote vilirekodiwa na kusainiwa na mimi na Muro mwenyewe kama uthibitisho kwamba kweli vitu hivyo vilikutwa garini kwake,” alidai shahidi huyo.Katika kesi hiyo Muro na wenzake Edmund Kapama na Deogratius Mgasa wanadaiwa kuomba rushwa ya Sh milioni 10, kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Michael Wage, Januari 29 mwaka jana.Mwendesha mashitaka wakili Mkuu wa Serikali Boniface Stanslaus alidai kwa jana upande wa mashitaka ulikuwa na shahidi mmoja ambapo wengine watatu waliobaki watatoa ushahidi wao pindi kesi hiyo itakapopangiwa tarehe nyingine. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 7 na 8, mwaka huu itakaposikilizwa tena.