Social Icons

Tuesday, May 31, 2011

WANAFUNZI WA TOSAMA IRINGA WATAWANYWA KWA MABOMU


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Tosamaganga, wakiandamana kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa, huku wakiongozwa na Askari Polisi wa kutuliza ghasia kabla ya kuanza kuzuiliwa.


WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Tosamaganga wilayani Iringa jana waliandamana katika maandamano ya amani kuelekea ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa kuwasilisha malalamiko yao dhidi ya uongozi wa shule hiyo.



Lakini wakati wakiwa katika maandamano hayo Askari wa kutuliza ghasi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatawanya wanafunzi hao zaidi ya 1000 wa shule hiyo kama njia ya kuwazuia kuandamana.


Tukio la mapambano kati ya FFU na wanafunzi hao lilianza majira ya saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana kwa polisi kufukuzana na wanafunzi hao kuwarudisha kwa mabomu shuleni pasipo mafanikio baada ya idadi kubwa ya wanafunzi kukimbilia porini na wengi wao kujificha katika nyumba za wenyeji wa maeneo hayo.


Kabla ya polisi kufikia hatua hiyo ya kuwatawanya wanafunzi hao waliwaeleza waandishi wa habari kuwa sababu ya wao kufanya mgomo wa kutoingia madarasani na kutaka kuandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Iringa umetokana na uongozi mbovu wa shule hiyo usiozingatia haki za binadamu.


Waliwataja walimu wengine zaidi ya 6 wakiwemo wa kike (majina tunayo) ambao wamekuwa wakiwadharirisha kwa kuwapekua sehemu za siri hadharani na kupokonya simu zao kwa faida yao .


Aidha walidai kuwa chakula wanacholishwa shuleni hapo hakina ubora kama wanaoelezwa wazazi huku wakimtaka mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa kutolea ufafanuzi juu ya bajeti inayotengwa maalum kwa ajili ya shuleni hiyo kwa chakula.

Hivi ndivyo wanafunzi hao walivyoanza kutawanywa, hapa wakitimua mbio kila mmoja akijaribu kuokoa maisha yake baada ya askari kuanza kuachia mabomu ya machozi.
Hapa wakiingi msituni kujificha huku kila mmoja akiwa na mwelekeo wake.

Picha na Francis Godwin, Iringa

MASHABIKI WA MAN U WAJIFARIJI NA MSIMU WA DHAHABU WA SERENGETI



Mashabiki wa timu ya Man U ya uingereza wameibuka kidedea na kuwa mabingwa wa Tamasha la Mabingwa wa Mwendelezo wa Msimu wa Dhahabu na Serengeti Soccer Bonanza Mkoani Tanga, wakishangilia na kuinua kombe lao juu baada ya kushinda katika mchezo dhidi yao na timu ya mashabiki wa Barcelona mkoani humo na hatimaye timu hiyo ikamalizia hasira zake kwa wapinzani wao hao Barcelona kwa kuwabamiza kwa mikwaju ya penati tatu kwa moja baada ya kutoka suluhu katika dakika za 90 kumalizika bila kufungana kwenye bonanza lililofanyika leo kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Meneja mauzo wa Kampuni ya Serengeti Breweries mkoani Tanga, Faki Mohamed,(mwenye kofia) akikabidhi kombe kwa Nahodha wa timu ya mashabiki wa Manchester United, Julius Silasi, baada ya timu hiyo kuibamiza Barcelona katika mchezo wa fainali za Mwendelezo wa Msimu Dhahabu na Serengeti Soccer Bonanza. Kulia ni mratibu wa Bonanza hilo, Shafii Dauda (katikati) ni Meneja Mauzo wa Kanda Patrick Kisaka na Peter Ngassa.

MEYA SONGEA MBARON


Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Bi. Mariamu Mwakambaya Dizumba.

Na Stephano Mango,Songea.
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Songea Bi. Mariamu Mwakambaya Dizumba kwa tuhuma za kumtishia kumuua mwandishi wa habari
wa kujitegemea anayeandikia gazeti la Nipashe mkoani Ruvuma Bw. Gideon Mwakanosya.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma
Bw. Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa Dizumba lilitokea jana majira
ya saa za asubuhi mara tu baada ya kutoka safari yake ya Msumbiji.

Alisema kuwa Mwakanosya alitoa taarifa kituo kikubwa cha polisi kuwa Bi. Dizumba alimtolea
lugha za matusi na vitisho vikiwemo vya kumkamia kumuua na kumtaka awe anaandika habari za
Halmashauli na sio habari zinazomuhusu yeye na mume wake.

Alifafanua kuwa Mwakanosya alitoa taarifa ya tukio hilo yenye SO/RB/3553/2011 na baada ya
kuendelea kutishiwa alifungua kesi yenye namba SO/IR/2590/2011 katika kituo kikuu cha
polisi Songea na kwamba jeshi lake linaendelea kufanya upelelezi ikiwa ni pamoja na
kukusanya ushahidi wa pande zote mbili.

Kamuhanda alieleza zaidi kuwa upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa kwenye ofisi ya
Mwanasheria wa Serikali kanda ya Songea kwa hatua zaidi za kisheria ili mtuhumiwa
afikishwe mahakamani.

Banda la TA Reading latingisha ndani Ya Reading Carnival

Banda la TA Reading lilikuwa hivi.
Naibu Balozi wa Tanzania Uingereza, Chabaka Kilumanga (wa tatu kulia) akiwa na wadau wa Reading wakati wa Carnival.

URBAN PULSE CREATIVE inawaletea picha za matukio ya Reading Carnival iliyofanyika jana Jumatatu ambapo ilikuwa ni siku ya 'Bank Holiday'. Kwa mara ya kwanza TA Reading ikishirikiana na TANZ UK waliandaa banda la Kitanzania kwa kupika chakula cha Kitanzania na kuuza kwa wadau mbalimbali waliojitokeza kutembelea banda la TA ikiwa ni mojawapo ya mradi wa kuchangia mfuko wa TA Reading. Mgeni rasmi alikuwa Mh. Naibu Balozi wa Tanzania Uingereza, Chabaka Kilumanga aliyeambatana na Afisa wa Ubalozini Amosi Msanjila. Kwa ujumla banda ka Kitanzania lilitia fora kuliko mabanda yote mengine ya mataifa mbalimbali.
Zifuatazo ni picha zaidi za tukio hilo:

Afisa wa Ubalozi, Amosi Msanjila (kulia) akiwa na mpwa wake ndani ya Carnival.


Dello akiandaa kuku wa kuchoma.


Mdau Paul Onyango kutoka Bongo Fleva (kushoto) akiwa na wadau wa Reading.


Mh. Naibu Balozi Kilumanga (kulia) akijitayarisha kuchukua msosi.


Mpaka watasha walipagawa na banda la Kibongo.


Timu ya Urban Pulse ndani ya banda la TA Reading.


Wadau wa Reading wakila pozi ndani ya banda na TA Reading wakiwa na Berry Black (mwenye sweta nyekundu).


Nyomi iliyokuwepo pande hizo.

Asanteni

URBAN PULSE CREATIVE

GARI LAGONGA BAJAJ

Baadhi ya mashuhuda wa ajali waliofika mahali pa tukio.

Mmoja wa abiria waliokuwa katika Bajaj akikagua madhara ya ajali hiyo.

DEVERA mmoja wa Bajaj ambaye jina lake halikufahamika, alinusurika kufa juzi Jumapili maeneo ya Kawe, jijini Dar es Salaam, baada ya kugongwa na gari ambalo dereva wake alikimbia kwenda kusikojulikana akidhani ameua. Hata hivyo, dereva huyo na abiria wake hawakuumia sana kwani waliweza kushirikiana kulifukuza gari hilo kwa miguu japo hawakufanikiwa. Bajaj hiyo iliharibika sehemu kadhaa.

TAFAKARI YANGU JUU YA TAIFA LANGU

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgv_PXqInhyphenhyphen1Hs6cAyy_QvEJwaYkcIpzPo9E5YMBLExIjvHfxNYcejh7AMi1dRhAQbaT4FjT6EolclMwjJRuU0bor1ZPAIoBvg9WucGoOc0AXg1ZRHJXMWLETLCUwGnCfc9-yQW2uQz/s1600/Tanzania-flag.jpg

NIWASALIMIE NDUGU NA JAMAA KWA UJUMLA WENU NA NITOE SHUKRANI ZANGU KWA MOLA WANGU KWA KUNIPATIA FURSA HII TUKUFU YA KUANDIKA HAYA MACHACHE. TANZANIA NI TAIFA LILILO NA WINGI WA MABONDE, MITO, MAZIWA NA HATA MILIMA PIA, KAMA HIYO HAITOSHI TUMEBARIKIWA SANA KATIKA ARDHI YETU ILIYOJAA RUTUBA NA HATA MADINI YALIYOTAPAKAA KILA KONA.

HIVYO TUNA KILA SABABU YA KUJIVUNIA TAIFA HILI KIHISTORIA NA KIJIOGRAFIA PIA. LAKINI KUNA MSEMO WA KISWAHILI UNASEMA: "UKIMSIFIA MGEMA BASI TEMBO HULITIA MAJI", MSEMO HUU NAUFANANISHA NA TASWIRA AU MTAZAMO WANGU JUU YA TAIFA HILI NA UONGOZI WAKE .

TUMEPATA SIFA NYINGI ZA NDANI NA NJE YA NCHI YETU KIASI WENGI WALITAMANI KUWA NI MIONGONI MWETU KULINGANA NA SIFA BORA ZA TAIFA HILI. LAKINI WAPO WALIOONA SIFA HIZI SI KITU KWAO NA KUAMUA KULITIA DOA NA KASORO NYINGI ZISIZO NA FAIDA WALA THAMANI. KATIKA TAIFA WAMEHARIBU RASILIMARI NA SASA WANALIHARIBU TAIFA NAO NI HAWA WANAOITWA MAFISADI HAWA NI WATU WASIO NA UCHUNGU NA TAIFA HILI HATA KIDOGO NI WATU WALIOJAA UNAFIKI NA URAFI WA MALI HUKU WAKISAHAU KUWA HAPA DUNIANI WALIKUJA WATUPU NA WATAONDOKA WATUPU.

SERIKALI AMBAYO NI SHINA MAMA LA TAIFA LENYE KUSIMAMIA HAKI NA USTAWI WA TAIFA LEO NDIO IMEKUWA KIPAUMBELE KATIKA KUHARIBU MISINGI ILIOWEKWA NA WAASISI WA TAIFA HILI. NAKUMBUKA SHUJAA MWAKYEMBE NA KAMATI YAKE JINSI ILIVYOLIPUA UFISADI BUNGENI. MIMI KAMA MTANZANIA NILIFARIJIKA NA KUONA SASA TAIFA LINAAMKA KUTOKA KATIKA USINGIZI MZITO, NA KILICHOKUJA KUTOKEA SIKUAMINI MASIKIO YANGU NA KUNIFANYA NIONDOE IMANI NA SERIKALI ILIOKO KWA KUSHINDWA KUWAJIBIKA IPASAVYO.

LEO HII BAADHI YA WALIOTAJWA KATIKA KASHFA ZILE BADO NI WATUMISHI WA SERIKALI NA HATA SERIKALI HAIJATOA TAMKO LOLOTE JUU YA HAWA WATU KILA SIKU IMEKUWA IKIWAZUGA WANANCHI HUKU IKIWAACHA MAFISADI WAKIZIDI KUVIMBA VICHWA NA KUITAFUNA NCHI KWA MRIJA.

TANZANIA NI ILE ILE YA WENYE NACHO, WASIONACHO WATABAKI KUWA CHINI KILA SIKU. HII NI AIBU SANA

BADO TUNADHIHIRISHA UKARIBU NA 'MAPATNA' WETU WATATU AMABAYO NI UJINGA, UMASKINI NA MARADHI HAWA NDIO WATU TULIOKUBALI KUFUNGA NAO PINGU ZA MAISHA HUKU TUKIMUACHA ELIMU, MAISHA BORA NA UTAJIRI WAENDEZAO INASIKITISHA SANA!.

LEO MMERIPOTIWA NA MAGAZETI MKIPONGEZWA KWA KUSIMAMIA KESI YENU DHIDI YA EPA SAWA TUNAKUBALI ILA EPA NI ZAIDI YA RICHMOND? AU NI ZAIDI KAGODA? AMA NI ZAIDI YA DOWANS? AU NI ZAIDI YA MGODI WA KUFUA MAKAA YA MAWE KULE KIWILA? AU NI ZAIDI YA ULE UNUNUZI WA KIBABAISHAJI WA RADA YA MABILIONI YA WALIPA KODI WA TAIFA? NO! USHINDI WA EPA SI WAKUJIVUNIA TENA MNYAMAZE NA MKAE KIMYA TUMECHOSHWA NA TABIA ZENU ZA KUTUFANYA WATOTO, HAO WATUHUMIWA WA EPA NI KWA SABABU HAKUNA SURA YA WAZIRI? AU KWA KUWA HAWAKUWA HATA KATIKA SEKRETALIETI YA CHAMA FULANI? NDIO MMEAMUA KUWAWEKA MSALABANI NA KUWABEBESHA MZIGO WA MAOVU YENU ? MUNGU HAPENDI!

VYAMA VYA UPINZANI

SIAMINI KAMA NI NJAA AMA MNA HAJA YA KULIKOMBOA TAIFA, KWA DHATI NAIKUMBUKA ZANZIBAR YA KUANZIA MWAKA 2000 HADI KIPINDI CHA KAMPENI YA MWAKA 2010 MLISIMAMA NA KUONYESHA UPINZANI ULIOKOMAA ILA CHA AJABU SASA HIVI MMEKUWA KIMYAA. JE? ZILE HAKI ZA WANYONGE MLIZOKUWA MKIAHIDI KUZISHUGULIKIA NDO ZIMESHATIMIZWA? HAYO MAISHA BORA KWA WAZANZIBAR YAMESHAPATIKANA? SINA MAJIBU YA MASWALI HAYA ILA KAMA MNATAKA MADARAKA KWA URAFI WA MALI BASI SIASA SI MAHALI PAKE KWANI MTASABABISHA MAAFA MAKUBWA SANA MSITUMIE WANANCHI KAMA MITAJI YA MAFANIKIO YENU. NA NYIE WENGINE HUKO BARA NIMEWAONA TARIME MKIPIGA KELELE KILA KONA YA NCHI YA TANZANIA ANGALIENI YASIJE YAKAWAFIKA YA MSETO. BAADAE UPINZANI UKAFA KISHA MKAANZA KUKAA PAMOJA MKILA VINONO MKINYWA NA KUFURAHI HUKU BADO MKITUACHA SISI WALALA HOI NA NJAA ZETU. TAFUTENI AMANI YA KUDUMU, TAFUTENI MAISHA BORA YA KUDUMU, JIFUNZENI KUTENDA HAKI NA SI KULINDANA NA TAMBUENI HAZINA MNAYOIPANDA SASA NI FAIDA YENU YA BAADAE.

HODI IKULU

KUNA KIPINDI NILISOMA HABARI KUTOKA KTK MAGAZETI KUHUSU MTANDAO WA KIJASUSI TOKA MAREKANI ULIOINGIA NCHINI NA KUBAINI UOZO UNAOFANYIKA IKULU, NA IKASEMEKANA KUWA IKULU NDIYO INAZUIA UTEKELEZAJI WA KUWASHUGHULIKIA MAFISADI HAO. HILI NINALIUNGA MKONO KWA ASILIMIA MIA MOJA KUWA NDIVYO ILIVYO IKULU INAWALINDA TENA KWA HALI NA MALI. HILI NILIONA KUPITIA KITUO KIMOJA CHA HABARI, KIONGOZI MMOJA AKIMNADI MTUHUMIWA AMBAYE MWEZI MMOJA KABLA YA UCHAGUZI ALIKUWA NA KESI YA KUJIBU MAHAKANI. PILI, TUHUMA ILIYOSIMAMIWA NA AKINA MWAKYEMBE INA MAZINGIRA YA USHAHIDI ULIO HAI WA VIELELEZO. TATU, SERIKALI ILIDAIWA KUTAKA KULIPA MABILIONI YA DOLA KWA KAMPUNI YA DOWANS KAMA FIDIA HUKU IKIJUA KABISA DOWANS HAISTAHILI KULIPWA. NILISOMA RIPOTI YA KUTOKA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU WALIHAINISHA VIFUNGU SABA VILIVYOKIUKWA KATIKA SHITAKA HILO LAKINI SERIKALI YETU ILIKUWA TAYARI KULIPA DENI KWA MADAI KUWA HILO DENI HALIKWEPEKI. KWA NINI? HATUJUI NA HATA ALIPOKUJA HUYO ANAEJIITA MMILIKI WA KAMPUNI HIYO HAKUNA JIPYA ALILOKUJA NALO KWANI HATUKUSIKIA LOLOTE WALILOLIONGEA.

SASA HAKUNA NJIA, IKULU INAWEZA KUKWEPA UKWELI HUU HATUTAKI IFIKE IWE KAMA LIBYA ETI TUKALALAMIKE KWA WAHISANI WAJE WATUTANDIKE NA MALI ZETU WABEBE KISA TUMESHINDWA KUJIONGOZA! HAPANA, SERIKALI BADILIKENI JENGENI MIFUMO YENYE MISAADA KWA WANANCHI WENU, HAKUNA GENI KAMA UFISADI HATA NCHI ZILIZOENDELEA BADO ZILIUPITIA ILA HAUKUUZIDI HUU WA KWETU. FANYA KWA KUJIFUNZA ISIFANYE KWA KUUWA VIONGOZI WALIO MATAJIRI WA MALI NA MASKINI WA UFAHAMU HATUWATAKI NA NDIO SERIKALI INAYOWAKUMBATIA WASIO NA UZALENDO WALITAKIWA KUNYONGWA HADHARANI BILA AIBU WIMBO WA TAIFA UNAPIGWA HAWAISI CHOCHOTE KWA SABABU NI WANAFIKI HAWANA UZALENDO WAMEKAA KWA MASLAHI YAO BINAFSI

TAHADHARI BINAFSI

MIMI NI RAIA MWEMA NA MENYE KUPENDA HAKI YA WENGI ILA KWA KUYASEMA HAYA MSIJE MKASHANGAA MKISIKIA KWAMBA SIPO DUNIANI KWANI KUNA KATABIA WANAKO HAWA JAMAA ,WAKIONA WANAKOSOLEWA TU BASI WATAHAKIKISHA HUONEKANI WATAKUONDOA TU IWE KWA AJALI AMA KUVAMIWA NA MAJAMBAZI NA PENGINE HATA KWA SUMU YA CHAKULA HAYA NI MAMBO YALIYO WAZI NA WANAYOFANYA.

SOKOINE NA NYERERE MAGUFULI NA MWAKYEMBE

MAJINA HAYA KILA YAKITAJWA MABADILIKO AMA FARAJA NDANI YA NAFSI HUTOKEA, NIMEWAWEKA KWANI NI WATU WANAOPAMBANA NA WASIOOGOPA KITU ZAIDI YA SHERIA INAYOWAONGOZA HAKUNA ASIYEMJUA NYERERE KWA UHODARI WAKE WA KULINDA RASILIMALI NA KUTETEA WANYONGE, SOKOINE HAKUPENDA WATUMISHI WAZENBE NA WASIO WAADILIFU, MAGUFULI INGAWA HUKO NYUMA ALIYUMBA KWA KASHFA AMBAZO BAADAE ALIBADILIKA NA KUWA MFANO WA KUIGWA NA WENGINE NI MTU MWENYE MISIMAMO NA MCHAPAKAZI WA UKWELI. MWAKYEMBE HUYU NI SIMBA WA VITA HAOGOPI NA WALA HATISHIKI NA LOLOTE LILE, NINAWAPONGEZA KWA UCHAPAKAZI WENU HODARI INGAWA MABOSI WENU WANAWAKATISHA TAMAA ILA IKO SIKU NANYI MTAKUWA WAAMUZI MAANA WATU WANAWAKUBALI NA WANAWAONA. SITA NAE HAYUKO NYUMA.

HITIMISHO

MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD

SPECIAL OFFERS FROM TILBURY
NEXT FROM TILBURY WILL NOW BE ON SATURDAY 25/06/2011
NEXT FROM SHEERNESS WILL BE ON WEDNESDAY 12/06/2011
WEEKLY SERVICES FOR CONTAINER VESSELS CMA-CGM, MAERSK, ZIM, DELMAS, &MSC SHIPPING LINES

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS

WAZEE WA KAZI

UNIT 21 HARBOUR HOUSE


COLD HARBOUR LANE
RAINHAM
RM13 9YA
TEL: 01708550434
MOBILE:07903828119 (CHRIS LUKOSI),
07950689243 (SIMON LOUIS(MOHSIN)
FAX: 01708550434
WE SHIP ALL TYPES OF CARGO TO AFRICA AT UNBEATABLE RATES, i.e CONTAINERS, TRUCKS, CARS, MACHINES ETC.WE ALSO SELL USED VEHICLES & MACHINERY FROM UK.
KARIBU/WELCOME!!!!
JOIN US ON FACEBOOK

NEW PRICE CUTS AS USUAL
CAR(SALOON)TO DAR OR MOMBASA from TILBURY now £720
4X4 TO DAR OR MOMBASA from TILBURY now £800 only
.

FOR MORE INFORMATION PLEASE VISIT OUR WEBSITE
WWW.SERENGETIFREIGHT.CO.UK
email us info@serengetifreight.co.uk
serengetifreight@yahoo.co.uk

WHY PAY TOO MUCH?
SEE HOW WE CAN SAVE YOUR MONEY!
BEI ZETU TUMEZIANIKA HADHARANI HATUNA CHA KUFICHA
WALA HAZINA KIGUGUMIZI
WE CAN BEAT ANY QUOTES, YOU NAME IT!

Saturday, May 28, 2011

VIMWANA 10 WATINGA FAINALI YA KIMWANA MANYWELE TWANGA PEPETA

Baadhi ya washiriki wa kinyang’anyiro hicho, wakiwajibika stejini.

HATUA ya nusu fainali ya kumsaka Kimwana Manywele Twanga Pepeta 2011, usiku wa kuamkia leo imefana vilivyo ndani ya Club Sun Cirro Shekilango, Dar es Salaam.
Katika mchujo huo, vimwana 10 wamechaguliwa kuingia fainali inayotarajiwa kufanyika Juni 17, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar.
Tukio hilo lilipambwa na burudani kabambe kutoka kwa Bendi ya The African Stars International ‘Twanga Pepeta’ na Kundi la Off-Side Trick.



Waimbaji wa Twanga Pepeta wakipamba shindano hilo kwa kuimba.


Msanii wa Kundi la Off-Side Trick, (kushoto), akikamua kwenye shindano hilo sambamba na mnenguaji wao.


Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka (kushoto) akiwa kwenye pozi na wageni waalikwa.



Mwimbaji mahiri wa Twanga Pepeta, Charles Gabriel ‘Chalz Baba’ ‘akirap’ kwa staili yake.


Asha Baraka (kushoto), akiteta jambo na mratibu wa shindano hilo, Maimartha Jesse.


Baadhi ya majaji wa shindano hilo wakiwa ‘bize’ na kazi yao.


Mashabiki waliohudhuria shindano hilo wakishuhudia kwa makini.


Mnenguaji wa Twanga Pepeta, Lilian Tungaraza ‘Internet’ akizungusha nyonga muda mfupi baada ya kuombwa kucheza pamoja na Kundi la Off-Side Trick.


Maimartha (kulia), akimkaribisha Asha Baraka azungumze machache kabla ya washindi kutajwa.


Vimwana Manywele Twanga Pepeta waliofuzu kuingia fainali wakiwa kwenye pozi la pamoja na baadhi ya viongozi wa shindano hilo.


Wanenguaji wa kike wa bendi hiyo, wakiwajibika jukwaani.

MREMBO 'UNIVERSE' APATIKANA

Baadhi ya washiriki wakicheza kabla ya kuanza kwa shindano hilo.

Usiku wa leo, Jumamosi kulifanyika Shindano la kutafuta Mrembo ‘Miss Universe’ lililochukua nafasi ndani ya Hoteli ya Golden Tulip iliopo Masaki jijini Dar es Salaam.


Mshindi wa kwanza Nelly Kamwelu (katikati) akiwa na mshindi wa pili Neema Kilango (kushoto) na mshindi wa tatu Yakoba Asenga mara baada ya kutangazwa matokeo.


Warembo ambao walifanikiwa kuingia katika tano bora wakipozi ili wapate picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa kuingia katika nafasi hiyo.


Warembo waliofanikiwa kuingia katika tatu bora wakiwa wameshikilia mataji ya maua.


Mwanamuziki wa kizazi kipya Ambwene Yesaya ‘AY’ akipozi na mshindi Nelly Kamwelu.

Big Brother Amplified


Washiriki wa Big Brother Amplified, Weza wa Angola (aliyebebwa) na Wendall wa Zimbabwe wakionyesha moja ya staili tatu za kucheza muziki.


Karen wa Nigeria akionyesha umahiri wa kucheza muziki ikiwa ni sehemu mojawapo ya majukumu ya washiriki.

Habari/ Picha:M-net's Big brother Amplified

Friday, May 27, 2011

JE, HII NI SAWA KWA JINSIA MOJA?

..Sajenti na Mary (kulia) wakilishana keki kistaili..

Mpiga Tumba wa Bendi ya African Stars Intenational 'Twanga Pepeta' MCD, akipata kipande chake

...ni utamu tu wa keki jamani

....kula mtoto wangu kipande kidogo


...Gitaa Cake.....

MISS UNIVERSE KUPATIKANA LEO


SHINDANO la kumsaka Miss Universe Tanzania linafanyika leo kwenye ukumbi wa Golden Tulip Hotel jijini Dar es Salaam, ambapo mshindi wa taji hilo, atapata sh. Milioni 3.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communication, Maria Sarungi, alisema jana kuwa maandalizi yote yamekwisha kamilika na wanatarajia kuwa na mashindano yenye ushindani wa hali ya juu.
Maria alisema kuwa warembo wote wana morali ya hali ya juu tayari kupambana kwani zawadi za mwaka ni kubwa kulinganisha na miaka ya nyuma.
Alisema kuwa ukilinganisha na miaka iliyopita mwaka huu warembo watafaidika sana hususani kielimu kama ilivyo lengo kuu la mashindano haya ambapo elimu ni nyanja mojawapo ya kumwinua mwanamke.
Mbali na fedha taslimu wamejitokeza wadhamini mbalimbali katika kutoa zawadi kwa washindi.
Maria alisema kuwa mbali ya kuvaa taji, kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil, Miss Universe Tanzania pia ataoata nafasi ya kusoma nchini Marekani .

Mrembo huyo atasomea masuala ya uzalishaji habari, filamu na mengineyo katika chuo cha New York Film Academy na vilevile atakuwa balozi wa nia njema wa Vodacom, Jamii forums mtandao maarufu wa kijamii watatoa simu aina ya Blackberry Bold.

Mshindi wa pili atapata sh. Milioni 1 ambapo wa tatu atazawadiwa sh. 500,000 na wa tatu na wa nne watapata 250,000.
Warembo watakaoshika nafasi kuanza ya sita mpaka 10 watapata sh. 100,000 na waliobaki sh. 50,000.
Ppia Shear Illusion imetoa zawadi ya thamani ya shilingi 75,000/= kwa kila mshiriki na pia atatoa kifurushi cha vipodozi na nywele kwa mshindi wa Miss Universe Tanzania yenye thamani ya shilingi 350,000.
Kampuni ya ndege ya Precision air wao wametoa tiketi tatu za ndege kwa mshindi ambapo zitamsafirisha popote ndani ya nchi akiwa kwenye shughuli zake za kijamii, Mercy G beauty parlour wametoa ofa ya huduma mbalimbali za urembo kwa mshindi ikiwemo utunzaji wa kucha nywele na mengineyo kwa kipindi chote cha mwaka mzima.
Institute of Entrepreneurship Development with Youth and Women (MTI base/ILO SIYD) watatoa zawadi kwa Mrembo mwenye mahusiano mema (Miss Congeniality) ambapo mshindi atapiga professional portfolio yenye thamani ya dola za kimarekani 1000 pia watatoa zawadi kwa Miss Entrepreneurial Mindset ambapo mshindi atapata mafunzo ya kuanzisha biashara bure yenye thamani ya dola za kimarekani 1500 pia akiweza kuandaa vizuri mchanganuo wa biashara watamsaidia kumuunganisha na benki kwa ajili ya kupata mkopo wa biashara.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania imedhaniwa na Vodacom pamoja na Golden Tulip, Chanel Ten, Magic FM, The Citizen, Le Grande Casino, Coca Cola, Dar Life, Jamii Forums, MH Gallery, Dodoma Hotel, Tripple A, Vayle Springs, New York Film Academy, Shear Illusion, Mercy G, na Precision Air.

WASHINDI WA PROMOSHENI YA TUSKER MILIONI 500 WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO


MKURUGENZI
Mauzo na Masoko wa Bia ya Tusker,Segun Macaulay (watatu kushoto)akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. milioni 1, Mathias Martin, mkazi wa Yombo baada ya kujishindia katika promosheni ya Tusker Milioni 500 kwa mashabiki, inayochezeshwa na kampuni ya SBL kupitia bia ya Tusker ambayo itaendelea hadi mwezi July kwa watumiaji wa bia ya Tusker kujishindia zawadi mbalimbali za fedha. Wanaoshuhudia tukio hilo (kulia) ni John Warange na Rittah Mchaki meneja wa kinywaji cha Tusker (kushoto). Hafla ya kukabidhi zawadi hizo imefanyika Chang'ombe katika kiwanda cha (SBL)jana.
Trophin Marcel, akikabidhiwa zawadi ya mfano wa hundi.




John Shirima, akikabidhia zawadi ya mfano wa hundi.


Baraka Simon, akikabidhiwa zawadi ya mfano wa hundi.

IDD AZZAN AMSHUKIA SHYROSE


Mbunge wa kinondoni Idd Azzan

Mbunge wa jimbo la Kinondoni Idd azzan, aliesimamishwa miezi 18 kushiriki shughuli za chama baada ya kushindwa kuthibitisha kauli yake nae kaibuka kumlipua shyrose bhanji kuwa katika uchaguzi mkuu uliopita shrose alitoa sapoti kubwa sana kwa chama cha CHADEMA ila hakupewa adhabu.
Mbali na hayo Idd Azzan wiki iliyopita alipigwa zengwe na moja ya vigogo hao wa CCM kuwa eti ni pusha mzee wa mapouda..!
Siasa za kulipuana ndiyo umekuwa mtindo mpya wakukomoana wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama cha mapinduzi(CCM).

DAH!! TUNDU LISSU ACHEZEA KICHAPO!










Tundu Lissu akionyesha shati lake analodai kuchaniwa na polisi baada ya kumpa kichapo akiwa nje ya Mahakama ya Wilaya ya Tarime, baada ya kupata dhamana jana. Picha na Anthony Mayunga


MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, na wenzake saba ambao juzi walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime na kusomewa mashtaka matatu ya kuingia eneo la hospitali bila kibali, kufanya mkutano na kuzuia watu kufanya kazi, wamepata dhamana lakini wamezuiwa kutembelea maeneo ya Nyamongo hadi kesi inayowakabili itakapokwisha.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo, Yusto Roboroga alitoa uamuzi huo akisema ni kwa mujibu wa kifungu cha Sheria Namba 148 cha Makosa ya Jinai, kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ambacho kinatoa haki kwa watuhumiwa kupata dhamana. Alitoa uamuzi huo baada ya kupitia pingamizi lililowekwa na upande wa mashtaka kutaka wasipewe dhamana. Hata hivyo, alisema: “Washtakiwa wanazuiwa kutembelea maeneo ya Nyamongo mpaka kesi hiyo itakapokuwa imekwisha."

Hakimu Ruboroga alitaja masharti ya dhamana hiyo kuwa ni kusaini mkataba wa dhamana wa Sh5 milioni kwa wadhamini wawili wanaoaminika. Kwa wasio wakazi wa Tarime, alisema watatakiwa kupeleka mahakamani hati za mali isiyohamishika. Washtakiwa wote walikidhi masharti na kuachiwa kwa dhamana hadi Juni 26, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Saturday, May 21, 2011

SHEIKH YAHYA KUZIKWA JIONI HII

Maziko ya Sheikh Yahya aliyefariki dunia jana, yanatarajiwa kufanyika jioni hii katika makaburi ya Tambaza, yaliyoko jirani na Muhimbili Primary school jijini Dar es salaam na Makamu wa Rais, Dk. Ghalib Bilal (pichani kushoto) anatarajiwa kumuwakilisha Rais Kikwete katika msiba huo. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck said.


Mtoto wa marehemu, Hassan Yahya Hussein (wa pili kushoto), akiwa na viongozi wa serikali msibani leo mchana


Mchungaji Anthony Lusekelo ' Mzee wa Upako' akitoa rambirambi msibani mapema leo.


...sehemu ya waombolezaji upande wa kina mama


...sehemu ya waombolezaji upande wa kina baba


.aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Omar Mahita naye ni miongoni mwa viongozi mbalimbali waliohudhuria mazishi ya sheikh yahya nyumbani kwa marehemu Mwembe Chai, jijini Dar es salaam.