Social Icons

Friday, May 27, 2011

MISS UNIVERSE KUPATIKANA LEO


SHINDANO la kumsaka Miss Universe Tanzania linafanyika leo kwenye ukumbi wa Golden Tulip Hotel jijini Dar es Salaam, ambapo mshindi wa taji hilo, atapata sh. Milioni 3.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communication, Maria Sarungi, alisema jana kuwa maandalizi yote yamekwisha kamilika na wanatarajia kuwa na mashindano yenye ushindani wa hali ya juu.
Maria alisema kuwa warembo wote wana morali ya hali ya juu tayari kupambana kwani zawadi za mwaka ni kubwa kulinganisha na miaka ya nyuma.
Alisema kuwa ukilinganisha na miaka iliyopita mwaka huu warembo watafaidika sana hususani kielimu kama ilivyo lengo kuu la mashindano haya ambapo elimu ni nyanja mojawapo ya kumwinua mwanamke.
Mbali na fedha taslimu wamejitokeza wadhamini mbalimbali katika kutoa zawadi kwa washindi.
Maria alisema kuwa mbali ya kuvaa taji, kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil, Miss Universe Tanzania pia ataoata nafasi ya kusoma nchini Marekani .

Mrembo huyo atasomea masuala ya uzalishaji habari, filamu na mengineyo katika chuo cha New York Film Academy na vilevile atakuwa balozi wa nia njema wa Vodacom, Jamii forums mtandao maarufu wa kijamii watatoa simu aina ya Blackberry Bold.

Mshindi wa pili atapata sh. Milioni 1 ambapo wa tatu atazawadiwa sh. 500,000 na wa tatu na wa nne watapata 250,000.
Warembo watakaoshika nafasi kuanza ya sita mpaka 10 watapata sh. 100,000 na waliobaki sh. 50,000.
Ppia Shear Illusion imetoa zawadi ya thamani ya shilingi 75,000/= kwa kila mshiriki na pia atatoa kifurushi cha vipodozi na nywele kwa mshindi wa Miss Universe Tanzania yenye thamani ya shilingi 350,000.
Kampuni ya ndege ya Precision air wao wametoa tiketi tatu za ndege kwa mshindi ambapo zitamsafirisha popote ndani ya nchi akiwa kwenye shughuli zake za kijamii, Mercy G beauty parlour wametoa ofa ya huduma mbalimbali za urembo kwa mshindi ikiwemo utunzaji wa kucha nywele na mengineyo kwa kipindi chote cha mwaka mzima.
Institute of Entrepreneurship Development with Youth and Women (MTI base/ILO SIYD) watatoa zawadi kwa Mrembo mwenye mahusiano mema (Miss Congeniality) ambapo mshindi atapiga professional portfolio yenye thamani ya dola za kimarekani 1000 pia watatoa zawadi kwa Miss Entrepreneurial Mindset ambapo mshindi atapata mafunzo ya kuanzisha biashara bure yenye thamani ya dola za kimarekani 1500 pia akiweza kuandaa vizuri mchanganuo wa biashara watamsaidia kumuunganisha na benki kwa ajili ya kupata mkopo wa biashara.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania imedhaniwa na Vodacom pamoja na Golden Tulip, Chanel Ten, Magic FM, The Citizen, Le Grande Casino, Coca Cola, Dar Life, Jamii Forums, MH Gallery, Dodoma Hotel, Tripple A, Vayle Springs, New York Film Academy, Shear Illusion, Mercy G, na Precision Air.

0 comments: