Social Icons

Tuesday, May 31, 2011

TAFAKARI YANGU JUU YA TAIFA LANGU

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgv_PXqInhyphenhyphen1Hs6cAyy_QvEJwaYkcIpzPo9E5YMBLExIjvHfxNYcejh7AMi1dRhAQbaT4FjT6EolclMwjJRuU0bor1ZPAIoBvg9WucGoOc0AXg1ZRHJXMWLETLCUwGnCfc9-yQW2uQz/s1600/Tanzania-flag.jpg

NIWASALIMIE NDUGU NA JAMAA KWA UJUMLA WENU NA NITOE SHUKRANI ZANGU KWA MOLA WANGU KWA KUNIPATIA FURSA HII TUKUFU YA KUANDIKA HAYA MACHACHE. TANZANIA NI TAIFA LILILO NA WINGI WA MABONDE, MITO, MAZIWA NA HATA MILIMA PIA, KAMA HIYO HAITOSHI TUMEBARIKIWA SANA KATIKA ARDHI YETU ILIYOJAA RUTUBA NA HATA MADINI YALIYOTAPAKAA KILA KONA.

HIVYO TUNA KILA SABABU YA KUJIVUNIA TAIFA HILI KIHISTORIA NA KIJIOGRAFIA PIA. LAKINI KUNA MSEMO WA KISWAHILI UNASEMA: "UKIMSIFIA MGEMA BASI TEMBO HULITIA MAJI", MSEMO HUU NAUFANANISHA NA TASWIRA AU MTAZAMO WANGU JUU YA TAIFA HILI NA UONGOZI WAKE .

TUMEPATA SIFA NYINGI ZA NDANI NA NJE YA NCHI YETU KIASI WENGI WALITAMANI KUWA NI MIONGONI MWETU KULINGANA NA SIFA BORA ZA TAIFA HILI. LAKINI WAPO WALIOONA SIFA HIZI SI KITU KWAO NA KUAMUA KULITIA DOA NA KASORO NYINGI ZISIZO NA FAIDA WALA THAMANI. KATIKA TAIFA WAMEHARIBU RASILIMARI NA SASA WANALIHARIBU TAIFA NAO NI HAWA WANAOITWA MAFISADI HAWA NI WATU WASIO NA UCHUNGU NA TAIFA HILI HATA KIDOGO NI WATU WALIOJAA UNAFIKI NA URAFI WA MALI HUKU WAKISAHAU KUWA HAPA DUNIANI WALIKUJA WATUPU NA WATAONDOKA WATUPU.

SERIKALI AMBAYO NI SHINA MAMA LA TAIFA LENYE KUSIMAMIA HAKI NA USTAWI WA TAIFA LEO NDIO IMEKUWA KIPAUMBELE KATIKA KUHARIBU MISINGI ILIOWEKWA NA WAASISI WA TAIFA HILI. NAKUMBUKA SHUJAA MWAKYEMBE NA KAMATI YAKE JINSI ILIVYOLIPUA UFISADI BUNGENI. MIMI KAMA MTANZANIA NILIFARIJIKA NA KUONA SASA TAIFA LINAAMKA KUTOKA KATIKA USINGIZI MZITO, NA KILICHOKUJA KUTOKEA SIKUAMINI MASIKIO YANGU NA KUNIFANYA NIONDOE IMANI NA SERIKALI ILIOKO KWA KUSHINDWA KUWAJIBIKA IPASAVYO.

LEO HII BAADHI YA WALIOTAJWA KATIKA KASHFA ZILE BADO NI WATUMISHI WA SERIKALI NA HATA SERIKALI HAIJATOA TAMKO LOLOTE JUU YA HAWA WATU KILA SIKU IMEKUWA IKIWAZUGA WANANCHI HUKU IKIWAACHA MAFISADI WAKIZIDI KUVIMBA VICHWA NA KUITAFUNA NCHI KWA MRIJA.

TANZANIA NI ILE ILE YA WENYE NACHO, WASIONACHO WATABAKI KUWA CHINI KILA SIKU. HII NI AIBU SANA

BADO TUNADHIHIRISHA UKARIBU NA 'MAPATNA' WETU WATATU AMABAYO NI UJINGA, UMASKINI NA MARADHI HAWA NDIO WATU TULIOKUBALI KUFUNGA NAO PINGU ZA MAISHA HUKU TUKIMUACHA ELIMU, MAISHA BORA NA UTAJIRI WAENDEZAO INASIKITISHA SANA!.

LEO MMERIPOTIWA NA MAGAZETI MKIPONGEZWA KWA KUSIMAMIA KESI YENU DHIDI YA EPA SAWA TUNAKUBALI ILA EPA NI ZAIDI YA RICHMOND? AU NI ZAIDI KAGODA? AMA NI ZAIDI YA DOWANS? AU NI ZAIDI YA MGODI WA KUFUA MAKAA YA MAWE KULE KIWILA? AU NI ZAIDI YA ULE UNUNUZI WA KIBABAISHAJI WA RADA YA MABILIONI YA WALIPA KODI WA TAIFA? NO! USHINDI WA EPA SI WAKUJIVUNIA TENA MNYAMAZE NA MKAE KIMYA TUMECHOSHWA NA TABIA ZENU ZA KUTUFANYA WATOTO, HAO WATUHUMIWA WA EPA NI KWA SABABU HAKUNA SURA YA WAZIRI? AU KWA KUWA HAWAKUWA HATA KATIKA SEKRETALIETI YA CHAMA FULANI? NDIO MMEAMUA KUWAWEKA MSALABANI NA KUWABEBESHA MZIGO WA MAOVU YENU ? MUNGU HAPENDI!

VYAMA VYA UPINZANI

SIAMINI KAMA NI NJAA AMA MNA HAJA YA KULIKOMBOA TAIFA, KWA DHATI NAIKUMBUKA ZANZIBAR YA KUANZIA MWAKA 2000 HADI KIPINDI CHA KAMPENI YA MWAKA 2010 MLISIMAMA NA KUONYESHA UPINZANI ULIOKOMAA ILA CHA AJABU SASA HIVI MMEKUWA KIMYAA. JE? ZILE HAKI ZA WANYONGE MLIZOKUWA MKIAHIDI KUZISHUGULIKIA NDO ZIMESHATIMIZWA? HAYO MAISHA BORA KWA WAZANZIBAR YAMESHAPATIKANA? SINA MAJIBU YA MASWALI HAYA ILA KAMA MNATAKA MADARAKA KWA URAFI WA MALI BASI SIASA SI MAHALI PAKE KWANI MTASABABISHA MAAFA MAKUBWA SANA MSITUMIE WANANCHI KAMA MITAJI YA MAFANIKIO YENU. NA NYIE WENGINE HUKO BARA NIMEWAONA TARIME MKIPIGA KELELE KILA KONA YA NCHI YA TANZANIA ANGALIENI YASIJE YAKAWAFIKA YA MSETO. BAADAE UPINZANI UKAFA KISHA MKAANZA KUKAA PAMOJA MKILA VINONO MKINYWA NA KUFURAHI HUKU BADO MKITUACHA SISI WALALA HOI NA NJAA ZETU. TAFUTENI AMANI YA KUDUMU, TAFUTENI MAISHA BORA YA KUDUMU, JIFUNZENI KUTENDA HAKI NA SI KULINDANA NA TAMBUENI HAZINA MNAYOIPANDA SASA NI FAIDA YENU YA BAADAE.

HODI IKULU

KUNA KIPINDI NILISOMA HABARI KUTOKA KTK MAGAZETI KUHUSU MTANDAO WA KIJASUSI TOKA MAREKANI ULIOINGIA NCHINI NA KUBAINI UOZO UNAOFANYIKA IKULU, NA IKASEMEKANA KUWA IKULU NDIYO INAZUIA UTEKELEZAJI WA KUWASHUGHULIKIA MAFISADI HAO. HILI NINALIUNGA MKONO KWA ASILIMIA MIA MOJA KUWA NDIVYO ILIVYO IKULU INAWALINDA TENA KWA HALI NA MALI. HILI NILIONA KUPITIA KITUO KIMOJA CHA HABARI, KIONGOZI MMOJA AKIMNADI MTUHUMIWA AMBAYE MWEZI MMOJA KABLA YA UCHAGUZI ALIKUWA NA KESI YA KUJIBU MAHAKANI. PILI, TUHUMA ILIYOSIMAMIWA NA AKINA MWAKYEMBE INA MAZINGIRA YA USHAHIDI ULIO HAI WA VIELELEZO. TATU, SERIKALI ILIDAIWA KUTAKA KULIPA MABILIONI YA DOLA KWA KAMPUNI YA DOWANS KAMA FIDIA HUKU IKIJUA KABISA DOWANS HAISTAHILI KULIPWA. NILISOMA RIPOTI YA KUTOKA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU WALIHAINISHA VIFUNGU SABA VILIVYOKIUKWA KATIKA SHITAKA HILO LAKINI SERIKALI YETU ILIKUWA TAYARI KULIPA DENI KWA MADAI KUWA HILO DENI HALIKWEPEKI. KWA NINI? HATUJUI NA HATA ALIPOKUJA HUYO ANAEJIITA MMILIKI WA KAMPUNI HIYO HAKUNA JIPYA ALILOKUJA NALO KWANI HATUKUSIKIA LOLOTE WALILOLIONGEA.

SASA HAKUNA NJIA, IKULU INAWEZA KUKWEPA UKWELI HUU HATUTAKI IFIKE IWE KAMA LIBYA ETI TUKALALAMIKE KWA WAHISANI WAJE WATUTANDIKE NA MALI ZETU WABEBE KISA TUMESHINDWA KUJIONGOZA! HAPANA, SERIKALI BADILIKENI JENGENI MIFUMO YENYE MISAADA KWA WANANCHI WENU, HAKUNA GENI KAMA UFISADI HATA NCHI ZILIZOENDELEA BADO ZILIUPITIA ILA HAUKUUZIDI HUU WA KWETU. FANYA KWA KUJIFUNZA ISIFANYE KWA KUUWA VIONGOZI WALIO MATAJIRI WA MALI NA MASKINI WA UFAHAMU HATUWATAKI NA NDIO SERIKALI INAYOWAKUMBATIA WASIO NA UZALENDO WALITAKIWA KUNYONGWA HADHARANI BILA AIBU WIMBO WA TAIFA UNAPIGWA HAWAISI CHOCHOTE KWA SABABU NI WANAFIKI HAWANA UZALENDO WAMEKAA KWA MASLAHI YAO BINAFSI

TAHADHARI BINAFSI

MIMI NI RAIA MWEMA NA MENYE KUPENDA HAKI YA WENGI ILA KWA KUYASEMA HAYA MSIJE MKASHANGAA MKISIKIA KWAMBA SIPO DUNIANI KWANI KUNA KATABIA WANAKO HAWA JAMAA ,WAKIONA WANAKOSOLEWA TU BASI WATAHAKIKISHA HUONEKANI WATAKUONDOA TU IWE KWA AJALI AMA KUVAMIWA NA MAJAMBAZI NA PENGINE HATA KWA SUMU YA CHAKULA HAYA NI MAMBO YALIYO WAZI NA WANAYOFANYA.

SOKOINE NA NYERERE MAGUFULI NA MWAKYEMBE

MAJINA HAYA KILA YAKITAJWA MABADILIKO AMA FARAJA NDANI YA NAFSI HUTOKEA, NIMEWAWEKA KWANI NI WATU WANAOPAMBANA NA WASIOOGOPA KITU ZAIDI YA SHERIA INAYOWAONGOZA HAKUNA ASIYEMJUA NYERERE KWA UHODARI WAKE WA KULINDA RASILIMALI NA KUTETEA WANYONGE, SOKOINE HAKUPENDA WATUMISHI WAZENBE NA WASIO WAADILIFU, MAGUFULI INGAWA HUKO NYUMA ALIYUMBA KWA KASHFA AMBAZO BAADAE ALIBADILIKA NA KUWA MFANO WA KUIGWA NA WENGINE NI MTU MWENYE MISIMAMO NA MCHAPAKAZI WA UKWELI. MWAKYEMBE HUYU NI SIMBA WA VITA HAOGOPI NA WALA HATISHIKI NA LOLOTE LILE, NINAWAPONGEZA KWA UCHAPAKAZI WENU HODARI INGAWA MABOSI WENU WANAWAKATISHA TAMAA ILA IKO SIKU NANYI MTAKUWA WAAMUZI MAANA WATU WANAWAKUBALI NA WANAWAONA. SITA NAE HAYUKO NYUMA.

HITIMISHO

MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA

0 comments: