Social Icons

Tuesday, May 31, 2011

WANAFUNZI WA TOSAMA IRINGA WATAWANYWA KWA MABOMU


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Tosamaganga, wakiandamana kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa, huku wakiongozwa na Askari Polisi wa kutuliza ghasia kabla ya kuanza kuzuiliwa.


WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Tosamaganga wilayani Iringa jana waliandamana katika maandamano ya amani kuelekea ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa kuwasilisha malalamiko yao dhidi ya uongozi wa shule hiyo.



Lakini wakati wakiwa katika maandamano hayo Askari wa kutuliza ghasi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatawanya wanafunzi hao zaidi ya 1000 wa shule hiyo kama njia ya kuwazuia kuandamana.


Tukio la mapambano kati ya FFU na wanafunzi hao lilianza majira ya saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana kwa polisi kufukuzana na wanafunzi hao kuwarudisha kwa mabomu shuleni pasipo mafanikio baada ya idadi kubwa ya wanafunzi kukimbilia porini na wengi wao kujificha katika nyumba za wenyeji wa maeneo hayo.


Kabla ya polisi kufikia hatua hiyo ya kuwatawanya wanafunzi hao waliwaeleza waandishi wa habari kuwa sababu ya wao kufanya mgomo wa kutoingia madarasani na kutaka kuandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Iringa umetokana na uongozi mbovu wa shule hiyo usiozingatia haki za binadamu.


Waliwataja walimu wengine zaidi ya 6 wakiwemo wa kike (majina tunayo) ambao wamekuwa wakiwadharirisha kwa kuwapekua sehemu za siri hadharani na kupokonya simu zao kwa faida yao .


Aidha walidai kuwa chakula wanacholishwa shuleni hapo hakina ubora kama wanaoelezwa wazazi huku wakimtaka mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa kutolea ufafanuzi juu ya bajeti inayotengwa maalum kwa ajili ya shuleni hiyo kwa chakula.

Hivi ndivyo wanafunzi hao walivyoanza kutawanywa, hapa wakitimua mbio kila mmoja akijaribu kuokoa maisha yake baada ya askari kuanza kuachia mabomu ya machozi.
Hapa wakiingi msituni kujificha huku kila mmoja akiwa na mwelekeo wake.

Picha na Francis Godwin, Iringa

0 comments: