Social Icons

Tuesday, May 31, 2011

MEYA SONGEA MBARON


Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Bi. Mariamu Mwakambaya Dizumba.

Na Stephano Mango,Songea.
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Songea Bi. Mariamu Mwakambaya Dizumba kwa tuhuma za kumtishia kumuua mwandishi wa habari
wa kujitegemea anayeandikia gazeti la Nipashe mkoani Ruvuma Bw. Gideon Mwakanosya.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma
Bw. Michael Kamuhanda alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa Dizumba lilitokea jana majira
ya saa za asubuhi mara tu baada ya kutoka safari yake ya Msumbiji.

Alisema kuwa Mwakanosya alitoa taarifa kituo kikubwa cha polisi kuwa Bi. Dizumba alimtolea
lugha za matusi na vitisho vikiwemo vya kumkamia kumuua na kumtaka awe anaandika habari za
Halmashauli na sio habari zinazomuhusu yeye na mume wake.

Alifafanua kuwa Mwakanosya alitoa taarifa ya tukio hilo yenye SO/RB/3553/2011 na baada ya
kuendelea kutishiwa alifungua kesi yenye namba SO/IR/2590/2011 katika kituo kikuu cha
polisi Songea na kwamba jeshi lake linaendelea kufanya upelelezi ikiwa ni pamoja na
kukusanya ushahidi wa pande zote mbili.

Kamuhanda alieleza zaidi kuwa upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa kwenye ofisi ya
Mwanasheria wa Serikali kanda ya Songea kwa hatua zaidi za kisheria ili mtuhumiwa
afikishwe mahakamani.

0 comments: