Saturday, October 30, 2010
SIKILIZA HOTUBA YA MH. MKAPA LEO JANGWANI
THEA AFUNDWA USIKU WA KUAMKIA LEO
FIVE STAR YAZINDUA MWACHE ANENG'NEKE
Wanamuziki wa Five Star wakiwajibika jukwaani
Katika uzinduzi huo mwanamuziki mkogwe wa miondoko hiyo Bi. Kidude kutoka Zanzibar na kundi lake ndio alikuwa wa kwanza kupanda jukwaani na kuwaburudisha mashabiki.
Shabiki ambaye alivaa kinguo kifupi naye akionyesha manjonjo yake
Bi Kidude akiimba wimbo maarufu wa Ahmada Umelewa.
Mtangazaji wa Redio ya Time Fm, Hadija Shaibu ‘Dida’ akitaniana na Bi Kidude.
Bi Kidude akisunda pesa zake ambazo ametunzwa na mashabiki wake.
Friday, October 29, 2010
MATEJA20 NA PICHA ZA MATUKIO TOFAUTI...
Shumileta na mambo ya Red Bull siku chache baada ya kutangaza kuachana na 'Gambe' hapa alikuwa nje ya Club Bilicanas Posta Dar, juzikati.
Baby Boy akijalibu kuunda Swagger.
Mzee wa Pamba akionyesha vijisenti vyake ndani ya Club Bilicanas.
Mnenguaji wa Bendi ya African Stars International 'Twanga Pepeta' akiwa amezimika muda mfupi baada ya kushuka jukwaani ndani ya ukumbi wa Club Bilicanas.
Rehema Chalamilla Ray C wa ( pili kulia) akila Bata na marafiki zake ambao majina yao hayakutamburika mara moja katika kiwanja cha Samaki Samaki Mlimani City jijini Dar juzikati, wa pili 'kulia' ni Jerald Lucas Reporter wa magazeti ya Ijumaa.
Ray C katika pozi.
DK, SHEIN USO KWA USO NA DK. BILAL AIRPORT
AMINI: PENZI NA LINAH, KWANGU.....
WIKI hii kupitia MATEJA20 namleta kwenu kijana kutoka Tanzania House of Talent ‘THT,’ Amini Mwinyimkuu Mpili. Mshkaji alizaliwa 1986 katika Hospitali ya Mwananyamala Kinondoni jijini Dar es Salaam akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto saba wa mzee Mwinyimkuu.
Alianza safari ya masomo 1997 katika Shule ya Msingi Kinondoni na kuhitimu mwaka 2003. Kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake hakuendelea na masomo ya sekondari.
Hata hivyo mwishoni mwa mwaka 2003 aliamua kusoma English Course mtaani kwao kwa ‘teacher’ mmoja aliyemtaja kwa jina la Chris kwa muda wa miezi sita kisha kujiingiza kwenye muziki.
Bila kuremba,ungana nami ili uweze kujua mawili matatu kuhusu msanii huyu.
TQ:Unaweza kuniambia ni nani hasa aliyekushawishi ukaamua kujikita kwenye ‘game’ la muziki wa Bongo?
AMINI:Aah! Kiukweli naweza kusema aliyenishawishi ni kaka yangu Bahati Mwinyimkuu ambaye tangu nikiwa mdogo yeye alikuwa akiimba na kwa ujumla familia yetu wote ni wanamuziki.
TQ: Je, ni nani aliyekushika mkono kukupeleka THT?
AMINI: Aliyenipeleka THT ni dada mmoja anaitwa Vumi. Tulikutana Studio ya Royal Production ambako nilienda kwaajili ya kurekodi wimbo wangu ulioitwa Kino na baada ya kunikuta nikiingiza sauti studio hapo alipenda jinsi nilivyokuwa nikiimba na kunishika mkono moja kwa moja hadi THT na nikakubaliwa.
TQ:Ulipotia timu THT kwa mara ya kwanza ni mazingira yapi magumu ambayo ulikutana nayo? Pili, wimbo wako wa kwanza ukiwa hapo uliitwaje.
AMINI:Kiukweli mazingira magumu ya kwanza ilikuwa ni Interview na mazoezi tuliyokuwa tukiyafanya na ukizingatia nilikuwa bado sijazowea. Kuhusu wimbo wa kwanza ulitambulika kwa jina la SO SOO ambao niliufanyia katika studio ya Jupiter Zanzibar.
TQ: Je, kwa sasa bado unamilikiwa na THT au unafanya kazi kivyako?
AMINI: Bado niko chini ya THT na hata kama ukihitaji shoo kwangu siwezi kwenda bila mawasiliano na bosi wangu Ruge.
TQ: Vipi kuhusu maisha yako ya kimapenzi?
AMINI:Kwasasa niko singo ila nina mpenzi wangu ambaye tunapendana na kuheshimiana sana. Huyu ni msanii mwenzangu ambaye anaitwa Estelinah Sanga ‘Linah’.
TQ: Je, Linah ulianza naye uhusiano ukiwa THT au kabla?
AMINI:Linah nilianza naye uhusiano kabla sijaingia THT maana kabla sijaingia THT nilikuwa nikiishi Kimara ambako yeye pia alikuwa akiishi.
TQ: Hebu niambie ukifanikiwa kuingia katika maisha ya ndoa na Linah, ungependa mpate watoto wangapi?
AMINI: Hilo kwasasa ziwezi kulizungmzia maana siku zote Mungu ndiye anayepanga hivyo anatarajia majaaliwa ya Mungu.
AMINI: Kusema kweli ninapokuwa na mpenzi wangu huwa nafurahi sana akiniambia neno lolote la kudumisha uhusiano wetu tena kwa kauli ya mahaba.
TQ:Tangu jina lako limekuwa kubwa ni usumbufu gani unaokutana nao kutoka kwa mashabiki zako hasa wa kike?
AMINI:Katika mazuri naweza kusema mara nyingi huwa napigiwa simu na wasichana wakiniambia wanapenda sauti na uimbaji wangu, ingawa wengi wao wamekuwa wakianza na gia hiyo na mwisho wake wanaingiza suala la mapenzi jambo ambalo ninaweza kusema ni la kawaida kwa msanii yoyote anayekubalika duniani.
TQ:Tangu umehiti kwenye ‘game’ nikitu gani kipya ambacho wategemee mashabiki kutoka kwako?
AMINI:Wanatakiwa kujua kuwa soon nitatoa albamu yangu mwenyewe ambayo itakuwa n jumla ya nyimbo 10 ingawa jina la albamu bado sijachagua.
TQ:Nini ushauri wako kwa mashabiki na wasanii wenzako?
AMINI: Ushauri wangu kwa wasanii ni kwamba lazima tuwe na heshima kwa kila mtu maana naamini kwa kufanya hivyo tutaweza kutimiza malengo yetu kwa game hii ya Kibongo bongo. Mashabiki nao nawashauri watuunge mkono kwa kununua kazi zetu.
Endelea kucheki Tenquestion za mastar wa Kibongo kupitia Mateja20 kila siku ya ijumaa.
Thursday, October 28, 2010
WAANGALIZI WA UCHAGUZI WA UMOJA WA AFRIKA WATUA DAR
Waangalizi hao wanaoongozwa na aliyekuwa Rais wa Sierra Leone, Dr Ahmad Tejan Kabbah wamefikia katika Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam na wanatarajia kukaa nchini mpaka Novemba 5, 2010 watakapohitimisha kazi yao na kuzungumza na waandishi wa habari.
Dr Ahmad Tejan Kabbah akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari.
Baadhi ya waangalizi wakimsikiliza Mkuu wa Msafara wao, Dr Kabbah wakati akizungumza na waandishi wa habari leo.
KIPOFU AIBUKA KIDEDEA NA TIGO KWALUZA
Jackson Mmbando (kushoto), akimkabidhi kitika cha shilingi milioni moja, Musa Zuberi, baada ya kushinda mchezo huo. Anayeshuhudia ni afisa wa Huduma za Wateja wa kampuni hiyo Nasra Msuya.
Sehemu ya wateja wakisubiri waitwe majina yao kwa ajili ya kuchukua “mkwanja” wao.
WATANZANIA TUPIGE KURA
WATANZANIA TUPIGE KURA
Tanzanian Reality Show - Lujwangana Household
DREVA WA 'BODABODA' ANUSURIKA KIFO
Pikipiki iliyohusika katika ajali hiyo.
Baadhi ya watu wakishuhudia ajali hiyo.
KAZI ZETU, VIBURUDISHO VYETU, IMANI YETU
KITAMBO kidogo, kabla utandawazi haujaingia nchini, maisha yalikuwa yanakwenda ‘kibubu-bubu’ kiasi kwamba mtu aliweza kufanya tukio la kushangaza mahali fulani lakini lisisikike popote.
Lakini kwa dunia ya leo, hilo haliwezekani, kwani kama utapigwa kofi kimyakimya na mkeo ndani ya nyumba, si ajabu kesho jambo hilo ukalikuta gazetini! Ndivyo maisha ya sasa yalivyo.
Kumekuwa na kawaida moja ya watu kupitia sehemu kadhaa za viburudisho baada ya kazi zao kwa ajili ya kupumzisha akili na kuchangamsha damu, lakini ndani ya hayo yote kuna jambo ambalo limekuwa likiwachanganya wengi na kuwaacha kwenye maswali lukuki yasiyo na majibu.
Hili ni lile linalohusu aina ya burudani wanayokutana nayo pindi wanapoamua kuwa ‘bize’ na kukonga nyoyo zao kwa vinywaji katika ‘viwanja’ mbalimbali vya starehe.
Siku hizi, si ajabu kuingia kwenye baa au sehemu fulani ya kinywaji na kukutana na sauti kubwa ya muziki wa Injili ukiporomoshwa eneo hilo ilihali si mahala pake sahihi.
Hii imekuwa ikiwachanganya watu wengi ambao wanaingia maeneo hayo kujiachia, lakini sasa cha ajabu watu hao wakiwa bado hawajakolea ‘ulabu’ huanza kuhoji kwa maswali mfululizo kuhusu hatua hiyo ya kupigiwa muziki wa Injili ambao kwa asilimia mia moja unamtukuza Mungu.
“Wewee! Mbona unatuwekea nyimbo za dini hapa kwani tuko kanisani? Acheni mambo hayo jamani la sivyo tutaondoka!” watu husikika wakisema maneno hayo kila mara.
Lakini dakika chache baadaye, pale kinywaji kinapokuwa kimeshakolea haohao waliokuwa wakiponda kwa kelele ndiyo wanakuwa mstari wa mbele kuziomba ama kuinuka kwenda kucheza hasa pale DJ anapoamua kuzipa nafasi nyimbo hizo. Hakika hii ni ajabu!
Haya, lakini hayo ni yao na starehe zao. Turudi kwenye mada ya msingi. Suala la upigwaji wa nyimbo za dini kwenye sehemu za starehe kama baa na kadhalika ni kutokuelewa maana halisi ya muziki huo. Au, je, hiyo ndiyo sehemu sahihi kwa ajili ya kuwakomboa waliopotea?
Hakuna hakika kamili. Hata hivyo, mnaojua maana mtatuambia, lakini kwetu sisi tunaona kama ni hali ya kutokuthaminiwa kwa muziki wenyewe. Mbona hatujawahi kusikia kaswida ikipigwa sehemu kama hizo?
Kumbukeni lengo si kurushiana kashfa na lugha chafu, tunachokitafuta ni maana halisi na ukweli juu ya uhalali wa kupigwa kwa nyimbo hizo sehemu ambazo lugha kutoka Maandiko Matakatifu inasisitiza kwamba ni haramu.
Wednesday, October 27, 2010
MPOTO ATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA
MSANII ‘first class’ katika miondoko ya mashairi nchini, Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba, ametoa misaada kwenye kituo cha watoto yatima na wasio na makao maalumu, CHAKUWAMA Orphanage Centre, kilichoko Sinza-Mori, jijini Dar es Salaam ambacho kinamilikiwa na Mama Hadija.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mpoto alisema ameamua kuwasaidia watu hao akiamini kuwa ni jamii yake kwani yeye pia ni yatima na siku ya leo ni siku ya kuzaliwa kwake inayoambatana na tarehe ya kifo cha mama yake mzazi.
“Nimeamua kutoa misaada kwani ni sehemu ya kutambua uwepo wa kundi hili muhimu, hata mimi ni mwenzao kwani sina wazazi na kwa kuwa leo ni siku ya kuzaliwa kwangu na ni siku ambayo mama yangu mzazi alifariki. Hivyo katika hili sina cha kuongeza zaidi ya kuwatia moyo na Mungu atawalinda,” alisema Mpoto.
Mpoto ni msanii aliyepata mafanikio makubwa kutokana na mashairi yake na sasa ameweza kutengeneza bendi yake binafsi inayofahamika kwa jina la ‘Mjomba Band’ yenye makazi yake Kinondoni-Mkwajuni jijini Dar.
….Mpoto akiingia ndani ya mjengo wa watoto yatima.
….Akiongea Mama Hadija mmliki wa kituo hicho.
...Mama Hadija akimsikiliza Mpoto.
…. Akipokea misaada ya chakula na mafuta.
...Mpoto akitoa shukrani kwa Mama Hadija.
….Akijiandaa kuimba nao wimbo wa ‘Mjomba’.
....Tayari wimbo wa ‘Mjomba’ umeanza.
...DJ Choka naye alikuwepo.
...Ubao wa kituo hicho.
...Wimbo umekolea.
...Mjomba akiongea na waandishi wa habari.
...Mama Hadija akijibu maswali ya waandishi wa habari.
…..Akifurahi na watoto.