Meneja Uhusiano wa Tigo nchini, Jackson Mmbando, akiwaonesha kwenye kompyuta wanahabari na washindi wa shindano hilo (hawapo pichani), vocha zinazotumika katika mchezo huo.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo, leo imeendelea kuwakabidhi zawadi, pesa taslimu na wengine hundi, wateja wake waliojishindia katika mchezo wa kubahatisha wa Kwaruza na Ushinde. Katika mchezo huo, Musa Zuberi, mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam ambaye ni kipofu, baada ya kukwaruza vocha aliyonunua ameibuka na ushindi wa shilingi milioni moja.
Jackson Mmbando (kushoto), akimkabidhi kitika cha shilingi milioni moja, Musa Zuberi, baada ya kushinda mchezo huo. Anayeshuhudia ni afisa wa Huduma za Wateja wa kampuni hiyo Nasra Msuya.
Sehemu ya wateja wakisubiri waitwe majina yao kwa ajili ya kuchukua “mkwanja” wao.
Baadhi ya washindi wakiwa na furaha baada ya kukabidhiwa pesa zao.
0 comments:
Post a Comment