Mwendesha pikipiki akiwa amezungukwa na watu baada ya kuanguka na kuumia vibaya sehemu mbalimbali za mwilini.
MWENDESHA pikipiki ambaye jina lake halikufahamika leo asubuhi amenusurika kufa baada ya kugongwa na gari aina ya Suzuki ambalo hutumiwa kuwafundishia madereva wanafunzi lililokuwa limeandikwa Victory Driving Mbezi Makonde na namba za simu 0754 594050. Ajali hiyo ilitokea eneo la Mlimani City katika Barabara ya Sam Nujoma ambapo gari hilo lilimparamia mwendesha pikipiki baada ya kulikwepa gari jingine lililokuwa likija mbele. Hadi kamera yetu inaondoka kwenye tukio, polisi walikuwa bado hawajafika na Wasamaria wema walilazimika kumpeleka majeruhi huyo hospitali.
Pikipiki iliyohusika katika ajali hiyo.
Baadhi ya watu wakishuhudia ajali hiyo.
Suzuki iliyosababisha ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment