Social Icons

Friday, October 29, 2010

AMINI: PENZI NA LINAH, KWANGU.....


WIKI hii kupitia MATEJA20 namleta kwenu kijana kutoka Tanzania House of Talent ‘THT,’ Amini Mwinyimkuu Mpili. Mshkaji alizaliwa 1986 katika Hospitali ya Mwananyamala Kinondoni jijini Dar es Salaam akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto saba wa mzee Mwinyimkuu.
Alianza safari ya masomo 1997 katika Shule ya Msingi Kinondoni na kuhitimu mwaka 2003. Kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake hakuendelea na masomo ya sekondari.
Hata hivyo mwishoni mwa mwaka 2003 aliamua kusoma English Course mtaani kwao kwa ‘teacher’ mmoja aliyemtaja kwa jina la Chris kwa muda wa miezi sita kisha kujiingiza kwenye muziki.
Bila kuremba,ungana nami ili uweze kujua mawili matatu kuhusu msanii huyu.
TQ:Unaweza kuniambia ni nani hasa aliyekushawishi ukaamua kujikita kwenye ‘game’ la muziki wa Bongo?
AMINI:Aah! Kiukweli naweza kusema aliyenishawishi ni kaka yangu Bahati Mwinyimkuu ambaye tangu nikiwa mdogo yeye alikuwa akiimba na kwa ujumla familia yetu wote ni wanamuziki.
TQ: Je, ni nani aliyekushika mkono kukupeleka THT?
AMINI: Aliyenipeleka THT ni dada mmoja anaitwa Vumi. Tulikutana Studio ya Royal Production ambako nilienda kwaajili ya kurekodi wimbo wangu ulioitwa Kino na baada ya kunikuta nikiingiza sauti studio hapo alipenda jinsi nilivyokuwa nikiimba na kunishika mkono moja kwa moja hadi THT na nikakubaliwa.
TQ:Ulipotia timu THT kwa mara ya kwanza ni mazingira yapi magumu ambayo ulikutana nayo? Pili, wimbo wako wa kwanza ukiwa hapo uliitwaje.
AMINI:Kiukweli mazingira magumu ya kwanza ilikuwa ni Interview na mazoezi tuliyokuwa tukiyafanya na ukizingatia nilikuwa bado sijazowea. Kuhusu wimbo wa kwanza ulitambulika kwa jina la SO SOO ambao niliufanyia katika studio ya Jupiter Zanzibar.
TQ: Je, kwa sasa bado unamilikiwa na THT au unafanya kazi kivyako?
AMINI: Bado niko chini ya THT na hata kama ukihitaji shoo kwangu siwezi kwenda bila mawasiliano na bosi wangu Ruge.
TQ: Vipi kuhusu maisha yako ya kimapenzi?
AMINI:Kwasasa niko singo ila nina mpenzi wangu ambaye tunapendana na kuheshimiana sana. Huyu ni msanii mwenzangu ambaye anaitwa Estelinah Sanga ‘Linah’.
TQ: Je, Linah ulianza naye uhusiano ukiwa THT au kabla?
AMINI:Linah nilianza naye uhusiano kabla sijaingia THT maana kabla sijaingia THT nilikuwa nikiishi Kimara ambako yeye pia alikuwa akiishi.
TQ: Hebu niambie ukifanikiwa kuingia katika maisha ya ndoa na Linah, ungependa mpate watoto wangapi?
AMINI: Hilo kwasasa ziwezi kulizungmzia maana siku zote Mungu ndiye anayepanga hivyo anatarajia majaaliwa ya Mungu.

Linah.
TQ:Umesema uko na Lina na mnapendana sana, je mnapokuwa faragha unafurahi zaidi anapokufanyia nini?
AMINI: Kusema kweli ninapokuwa na mpenzi wangu huwa nafurahi sana akiniambia neno lolote la kudumisha uhusiano wetu tena kwa kauli ya mahaba.
TQ:Tangu jina lako limekuwa kubwa ni usumbufu gani unaokutana nao kutoka kwa mashabiki zako hasa wa kike?
AMINI:Katika mazuri naweza kusema mara nyingi huwa napigiwa simu na wasichana wakiniambia wanapenda sauti na uimbaji wangu, ingawa wengi wao wamekuwa wakianza na gia hiyo na mwisho wake wanaingiza suala la mapenzi jambo ambalo ninaweza kusema ni la kawaida kwa msanii yoyote anayekubalika duniani.
TQ:Tangu umehiti kwenye ‘game’ nikitu gani kipya ambacho wategemee mashabiki kutoka kwako?
AMINI:Wanatakiwa kujua kuwa soon nitatoa albamu yangu mwenyewe ambayo itakuwa n jumla ya nyimbo 10 ingawa jina la albamu bado sijachagua.
TQ:Nini ushauri wako kwa mashabiki na wasanii wenzako?
AMINI: Ushauri wangu kwa wasanii ni kwamba lazima tuwe na heshima kwa kila mtu maana naamini kwa kufanya hivyo tutaweza kutimiza malengo yetu kwa game hii ya Kibongo bongo. Mashabiki nao nawashauri watuunge mkono kwa kununua kazi zetu.
Endelea kucheki Tenquestion za mastar wa Kibongo kupitia Mateja20 kila siku ya ijumaa.

0 comments: