Social Icons

Thursday, October 28, 2010

WAANGALIZI WA UCHAGUZI WA UMOJA WA AFRIKA WATUA DAR

Mkuu wa msafara wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Afrika, Dr Ahmad Tejan Kabbah akizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo katika Hoteli ya Movenpick. Kulia ni Tshimanga Mukadi-Mutoke na kushoto ni Matias Matondo wote kutoka Makao Makuu ya AU, Addis Ababa.
Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika(AU) wamewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia mwenendo mzima wa uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na rais nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Waangalizi hao wanaoongozwa na aliyekuwa Rais wa Sierra Leone, Dr Ahmad Tejan Kabbah wamefikia katika Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam na wanatarajia kukaa nchini mpaka Novemba 5, 2010 watakapohitimisha kazi yao na kuzungumza na waandishi wa habari.


Dr Ahmad Tejan Kabbah akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari.


Baadhi ya waangalizi wakimsikiliza Mkuu wa Msafara wao, Dr Kabbah wakati akizungumza na waandishi wa habari leo.


Hoteli ya Movenpick, walipofikia waangalizi hao.

0 comments: