Miongoni mwa wasanii na filamu zilizong’ara, ni filamu ya Ndoto za Elibidi kutoka Nchini Kenya, iliyotungwa na Kamau wa Ndung'u na Nick_Reding ambayo ilinyakua jumla ya tuzo nne, wakati msanii Yvone Cherry Monalisa alikuwa msanii pekee wa kibongo aliyenyakua tuzo ya mwigizaji Bora.
Tuzo nyingine zilizotolewa ni pamoja na Themba (Best Feature Film-Golden Dhow), Imani (Best Feature Film –Silver Dhow), The Gift (Filamu fupi bora), Pumzi (Special Jury Prize), Motherland( Best Documentary), Ndoto za Elibidi (Verona Award), Soul Boy (SIGNIS award), A step into darkness (SIGNIS Award) na My City on fire (East African Talent Award) kutoka Uganda.
Wengine ni Shungu (Sembene Ousmane Award), The gardener and his 21 flowers (Sembene Ousmane Award), My Policy (Chairman Award), Nani (Best Tanzanian Film), wakati tuzo ya Lifetime Achievement ikienda kwa Profesa Elias Eliezer Jengo na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo ambaye aliondoka na tuzo ya ZIFF Ambassador.
Kamau wa Ndung’u na Nick Reding wakifurahia tuzo waliyoipata kutokana na filamu yao ya Ndoto za Elibidi.
Mzee Chilo naye alikuwepo eneo la tukio, hapa akiwa amechill na Monalisa.
Mtunzi wa filamu ya Shungu akipokea tuzo yake.
Wanuri Kahiu kutoka Kenya tuzo baada ya filamu yake ya pumzi kuibuka kidedea.
Wasanii wa filamu wa kibongo waliohudhuria kwenye tamasha la ZIFF wakiwa jukwaani.
Mtunzi wa filamu ya Nani, Sajni Srivastava akiifurahia tuzo yake.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo ndiye aliyekuwa mgeni rasmi.
Mtunzi wa filamu ya My City on Fire, Dennis Onen akiifurahia tuzo aliyoipata.