Mtanange wa kumsaka mrembo wa jimbo la Miss Kinondoni 2010/11 jana ulimalizika katika ukumbi wa MlimaniCity ambapo mrembo aliyekuwa amevaa namba ya ushiriki 4 Alice Lushiku ndiye aliyetwaa taji hilo huku namba mbili ikinyakuliwa na Irene Hezeron na Amisuu Umari akikamilisha safu ya tatu bora kwa nafasi hiyo.
Warembo waliyokuwa wakiwania taji hilo wakiwa mbele ya watazamaji.
Mkufunzi wa warembo Joketi Mwegelo (kulia), akimpatia swali la kujibu Alice Lushiku ambalo alijibu vizuri na kumuongezea ‘point’ za ushindi.
Miss Kinondoni aliyemaliza muda wake, Lulu Abraham (kulia) akimvisha taji kwa mmliki mpya wa taji hilo, Alice baada ya kuwabwaga wenzake 10 na kutangazwa mshindi.
Wanenguaji wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’ wakiwajibika stejini katika kinyang’anyiro hicho.
Miss Kinondoni 2010 Alice Lushiku (katikati) akiwa kwenye pozi la pamoja na warembo wenzake waliyoshika nafasi za juu (kushoto)ni Irene Hezeron aliyeshika namba mbili mwishoni kulia ni Amisuu Umari aliyeshika namba tatu.
0 comments:
Post a Comment