Social Icons

Thursday, July 15, 2010

MAUJI KWENYE BAA MCHANA KWEUPE!

Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Sadam ameauwa kwa kupigwa risasi mchana wa leo katika baa maarufu ya Angels' Park iliyoko Ilala Sharief Shamba jijini Dar es salaam!! Kijana huyo inadaiwa kuuawa na mmiliki wa bar hiyo baada ya kundi la vijana wengi, akiwemo marehemu, kuvamia kwa lengo la kumpiga mwenye baa ili kulipiza kisasi! Mtandao huu umeeleza na mashuhuda kuwa, sakata lilianzia jana baada ya vijana wasiojulikana kudaiwa kumkaba mteja mmoja wa baa hiyo akiwa chooni na vijana hao kukamatwa na kuplekwa polisi ambako walishikiliwa hadi leo. Imedaiwa kuwa baada ya kuona wenzao wanasota rumande, pengine kwa sababu ya mmiliki wa huyo, waliamua kumfuata ili kulipiza kisasi kwa kumfanyia.

Wakiwa kundi huku wameshika silaha mbalimbali vikiwemo visu, vijana hao walivamia baa hiyo na kuanza kumpiga mwenye baa na kumchoma kisu ambacho bahati nzuri hakikumdhuru sana. Kuona hali hiyo, mwenye baa alitoa bastola yake, akapiga hewani ili kuwatisha, lakini waliendelea kumfuata na kumshambulia huku wakiharibu mali za baa hiyo, likiwemo gari lake lililovunjwa kioo cha nyuma. Awali vijana wawili walipigwa risasi na kujeruhiwa na marehemu aliendelea kumfuata mwenye baa na ndipo alipopigwa risasi na kufa papo hapo!

...sehemu ya watu waliojazana kushuhudia tukio hilo la aina yake kuwahi kutokea mitaa ya Ilala!

...jamaa wakibeba maiti ya Sadam kuingiza kwenye gari la polisi

...

...gari la mwenye baa lililovunjwa vioo na vijana hao wakati wakivamia baa hiyo


0 comments: