Social Icons

Tuesday, July 13, 2010

MATONYA KURUDI DAR KWA KISHINDO! -globalpublishers reports

Matonya akiwa mtaani.

Na Dunsata Shekidele,Morogoro.
OMBA omba maarufu nchini, Anthony Matonya, ambaye kwa sasa ameweka maskani katika mitaa ya Morogoro mjini, amesema kwamba yuko kwenye mchakato wa kurudi jijini Dar es salaam baada ya kuona wakazi wa mkoa huo wamemzowea sana kiasi cha kumkejeli badala ya kumsaidia.

Matonya aliyasema hayo leo asubuhi ofisini kwake barabara ya madaraka eneo la Msikiti wa Jamatini alipofanya mahojiano maalumu na mwandishi wetu juu ya mustakabali wa maisha aliyokuwa akiishi jijini Dar es salaam na yale anayoishi mkoani hapa.

"Swali zuli sana umeniuliza, ukweli maisha ya hapa Morogoro kwa sasa nayaona ni magumu, hilo linatokana na watu wengi wa hapa kiunizoea na kunipita bila kunipa chochote huku wakisema kwamba hawanisaidi kwa kuwa mimi ni maarufu nchini kuliko wao, hivyo hali hiyo ya umaarufu wa kijinga inanigharimu katika kipato changu. kwa sababu hiyo, niko kwenye mchakato wa kurejea jiji Dar es salaam, nadhani kwa sasa kumepoa kidogo tofauti na wakati ule wa serikali ya Makamba,"alisema Matonya.


Matonya akikinga kopo lake kupokea kitu kidogo kutoka kwa mpita njia

matonya akiwa kazini, huku wapita njia wakimshangaa

0 comments: