Thursday, March 31, 2011
DOTNATA AFANYA KUFURU AVUTA `HUMMER`
MSANII matawi ya juu katika tasnia ya filamu Bongo, Husna Mohamed Posh ‘Dotnata’ amefanya kufuru baada ya kutoa ‘burungutu’ kununua‘mkoko’ wa kifahari aina ya Hummer, Amani Jipya limeinyaka.
Akizungumza na gazeti hili muda mfupi baada ya kukamilisha taratibu mbalimbali za kuukomboa mkoko huo kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam, Dotnata alisema kuwa ametumia kiasi cha shilingi za kibongo Milioni 270 kununua ‘mchuma’ huo kutoka katika tawi la kiwanda cha magari hayo huko Detroit, nchini Marekani.
“Kila mtu atasema lake lakini ni kweli nimenunua gari hili kutoka Marekani na nimetumia kiasi cha shilingi milioni 270 mpaka linafika hapa,” alisema Dotnata.
Akiendelea zaidi, msanii huyo mwenye heshima kubwa ndani ya tasnia ya filamu za Kibongo alianika kuwa watu wasimuelewe vibaya kwa kununua gari hilo amefanya hivyo akiwa na lengo la kulikodisha kwenye kwenye sherehe mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili kupunguza makali ya maisha na siyo kutanua nalo kwa matanuzi yasiyo na lazima.
KAMATI YA BUNGE YAITWISHA SERIKALI MZIGO WA DOWANS
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya mahesabu ya Mashirika ya Umma Zitto Kabwe.
Agizo hilo la POAC lilitolewa jana katika kikao cha pamoja baina ya Kamati hiyo na makatibu wakuu wa Wizara za Fedha na Uchumi na Nishati na Madini na watendaji wa Tanesco.
Juzi, Kamati hiyo ilishindwa kuthibitisha deni hilo la zaidi ya Sh96 bilioni kutokana na kukosekana kwa ufafanuzi wa uhalali wake na nani anastahili kuilipa kati ya Serikali na Tanesco.Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha juzi zililidokeza gazeti hili kuwa tangu kutolewa kwa hukumu iliyotaka Dowans ilipwe fidia kutokana na mkataba wake wa kuzalisha umeme kuvunjwa kiholela, Serikali na Tanesco wamekuwa wakitupiana mpira wa nani anayepaswa kulipa deni hilo.
“Kamati imeshindwa kuthibitisha uhalali wa deni hili na tumewataka makatibu wakuu kufika kesho (Jumatano) ili waweze kutupa ufafanuzi kabla ya kutoa uamuzi,” aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Murtaza Mangungu, aliwaambia waandishi wa habari.
Baada ya mahojiano ya muda baina ya viongozi hao wa Serikali na Tanesco, Kamati hiyo iliitaka Serikali kuilipa Dowans ikiwa mahakama itatoa hukumu ya deni hilo kulipwa.Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe alisema jana kuwa kwa mujibu wa vitabu vilivyotolewa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), deni la Dowans lilitakiwa kuingizwa kwenye vitabu vya Serikali na si Tanesco.
"... Kwa sababu wao (Serikali) ndiyo walioingia mkataba na kampuni hiyo (Dowans) ya kuwalipa gharama za ununuzi wa umeme," alisema Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema). Zitto alisema Serikali ilipinga suala hilo na Katibu Mkuu (Hazina) alimwandikia CAG, Februari 9, mwaka huu kuwa Tanesco inapaswa kulipa deni hilo. Tanesco nayo iliandika barua ya kupinga kulipa deni hilo jambo ambalo lilisababisha CAG kukataa kusaini vitabu hivyo.
"Ripoti ya CAG iliyotolewa kwenye kamati hii imeonyesha kuwa deni hili linapaswa kuonekana kwenye vitabu vya Serikali na si Tanesco kwa sababu wao (Serikali), ndiyo walioingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya kuzalisha umeme. Hivyo deni lake halipaswi kulipwa na Tanesco. Utata huo ulimfanya CAG aombe mwongozo," alieleza Zitto jana.
Kwa mujibu wa Zitto, baada ya malumbano hayo, POAC iliomba kukutana na makatibu wakuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi; na Nishati na Madini ili wajadili suala hilo na kufikia muafaka."Muafaka ni kuwa deni hilo linapaswa kuonekana kwenye vitabu vya Serikali hivyo wao ndiyo wenye jukumu la kulipa deni hilo ikiwa mahakama itatoa hukumu ya kulipwa," alisema Zitto.
Alisema Tanesco haiwezi kulipa deni hilo kwa sababu wao siyo walioingia mkataba na Dowans... "Tanesco haiwezi kubebeshwa mzigo usiowahusu, badala yake Serikali itawajibika yenyewe katika suala hilo ikiwa hukumu yake itatoka."Zitto alisema Tanesco linajiendesha kwa hasara kila mwaka na hiyo inatokana na wadaiwa kushindwa kulipa madeni yao ipasavyo, hivyo kulibebesha mzigo wa kulipa deni kubwa kama la Dowans ni sawa na kulifilisi au kuliua kabisa.
"Mwaka jana, Tanesco lilipata hasara ya Sh5 bilioni. Hii inatokana na sababu mbalimbali, ikiwamo ya wadaiwa wao kushindwa kulipa madeni yao. Jambo hilo limesababisha shirika lijiendeshe kwa hasara na kutokana na hali hiyo, hawawezi kubebeshwa mzigo huo wa Dowans," aliongeza.
Sakata la malipo kwa kampuni ya Dowans limeibua mjadala mkubwa miongoni mwa jamii hasa ya wasomi, wanasiasa na watu mbalimbali baadhi yao kupinga na wengine kukubaliana nayo.
Mjadala ulipamba moto baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema kueleza kuwa Serikali haina pingamizi na malipo hayo na kwamba tayari imewaagiza wahusika kutekeleza mara moja.
Kauli hiyo ya Werema na ile iliyotolewa na Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani kuunga mkono malipo hayo ziliwafanya wanaharakati wa haki za binadamu kufungua kesi mahakamani kupinga malipo hayo.
Wednesday, March 30, 2011
NENO LA LEO: SIMBA MZEE ANAPOKARIBIA KUFA...
Ndugu Zangu,
” HAYO malumbano ni ya kwao, sisi hatuyajui, wala hatutaki kuyajua.
Tunashughulika na kutekeleza Ilani tu… maneno maneno kama hayo
hayatuhusu”. Anasema John Chiligati, Katibu Mwenezi wa CCM.( NIPASHE,
Jumapili, Machi 27, 2011)
Simba anapozeeka na kukaribia kufa huanza kupoteza uwezo wa kuona,
kunusa na hata kusikia. Lakini, kuna moja ambalo simba ana hakika
nalo, kuwa ameacha simba watoto. Kizazi cha simba kitaendelea.
Chiligati anasema hayajui yanayotokea ndani ya UVCCM na malumbano
yanayoendelea. Hapa kuna mawili; kama ni kweli hayajui ni tatizo, na
kama anayajua na kuamua kutingisha mabega na kujifanya hayaoni wala
kuyasikia ni tatizo kubwa zaidi. Kwa vile, Umoja wa Vijana wa Chama ni
moja ya viungo muhimu kwenye mwili wa chama.
Maana, katika maisha haya ya kisiasa, vijana ndio nguzo na uhai wa
chama chochote kiwacho. Inakuwaje basi, chama kinachozeeka
kinapozungukwa na ’vijana wazee’? Uhai wa chama hicho utakuwa
hatarini. Na hilo ni Neno La Leo. ( Hii ni sehemu ya makala yangu,
RAIA MWEMA, leo Jumatano)
TUTAKUKUMBUKA DAIMA HAIKA
Haika Robert Masue (32) hatunaye tena. Amefariki Jumamosi Machi 26, mwaka huu katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam baada ya kushikwa na shinikizo la damu la ghafla. Amefariki ikiwa ni wiki chache zimepita tangu ajifungue mtoto. Haikal, ambaye alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya wakala wa bima ya Agin Insurance Brokers, atakumbukwa kwa uchapakazi wake na pengo lake litachukua miaka mingi kuliziba, kwani utendaji wake wa kazi ulikuwa hauna mfano. Global Publishers inaweza kuthibitisha hilo kwa sababu alikuwa akihudumia magari ya kampuni na ya viongozi wake kwa ufanisi wa hali ya juu, alikuwa anaweka kumbukumbu vizuri na hakuna wakati alipitisha tarehe za Bima. Haikal anatarajiwa kuzikwa leo Moshi. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Mungu ailaze roho yake mahali pema - Amin
...wakitoa jeneza kutoka nyumbani kwa wazazi wa marehemu, Kitunda, Ukonga.
...kanisa la Kilithuri la Gongo la Mboto kulikofanyika ibada
...waombolezaji wakiwa kanisani. Katika ni mama wa marehemu
...waombolezaji wakimuaga marehemu
...wakiingiza jeneza kwenye basi tayari kwa safari ya kuelekea Moshi kwa maziko.
HUYU NDIYE BWANAMDOGO ALIYEOTESHWA KUTIBU MAGONJWA SUGU MBEYA
Dogo, anakwenda kwa jina la Jafar Welino, anaumri wa miaka kumi na saba (17), kama unakumbuka juzi kati alijitangaza naye kuoteshwa kutibu magonjwa matano sugu huko Mbeya.
HAPPY BIRTHDAY UNIQUEENTZ
April 1 mwaka huu rafiki yangu na mmiliki wa
www.uniqueentertz.blogspot.com
Mr Magese,anatarajia kufanya sherehe ya kutimiza mwaka mmoja tangua aanzishe blog yake hiyo.
Hivyo basi Mateja20, inamtakakia kila lakheri katika kazi zake za kulisongesha grudumu hilo.
Naye kwa upnde wake Magese, alikuwa na haya ya kusema,
"Nawashukuru watizamaji wote kwa kunipa kampani yakutosha kwa mwaka mmoja uliopita pia mwenyezi mungu kunipa nguvu na uhai wakuwapa mavituz ya ukweli,taerhe 1 april tunatimiza mwaka mmoja. www.uniqueentertz.blogspot.com".
MWINGINE AJITOKEZA KUTOA KIKOMBE TABORA
Baadhi ya wananchi wakilamba kikombe kwa Bibi Tabora.
BENDI YA MASHUJAA KUTAMBULISHA WAPYA
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa Mgahawa wa Hadees, Meneja wa bendi hiyo, Mujibu Hamis, alisema kuwa maandalizi ya onyesho la utambulisho wa wanamuziki limekamilika kwa asilimia 99 na aslimia moja ikibaki kuwa ni onyesho lenyewe litakalofanyika katika Ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho.
“Tumejiandaa vilivyo kuwaonyesha mashabiki wa muziki wa dansi ujio mpya wa bendi yetu iliyokuwa kimya kwa ajili ya kujipanga ili kuweza kwenda na wakati katika jukwaa la ushindani la Muziki wa dansi, na pia tumejitahidi kuongeza wanamuziki katika kila idara kuanzia waimbaji hadi wanenguaji ili kuweza kutoa burudani iliyokamilika kwa mashabiki wetu” alisema Mujibu.
Aliwataja wanamuziki hao wapya wanajiunga na bendi hiyo kuwani pamoja na, Kajo anayetoka katika Kundi la Boziboziana, Jimmy Adol kutoka kwa Koffee Olomide, Profa Kariakoo kutoka Kinshasa, Kama Simba Komilion, kutoka kwa Felix Wazekwa.Wengine ni Rapa mahiri Sauti ya Radi, Kelvin, Salma Shaban ‘Teketeke’ Mariam Lelapel na Corando wote kutoka bendi ya Diamondi Musica.
Katika onyesho hilo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa bendi inayoongozwa na vijana watatu ‘Mapacha 3’, bendi yenye umri wa mwaka mmoja tangu ilipoanzishwa na kuweza kujizolea sifa kem kem baada ya kutwaa Tuzo mbili katika Kili Music Awards 2010, ambazo ni Tuzo ya Wimbo Bora wa bendi wa 2010 pamojana Tuzo ya Rapa bora wa bendi wa mwaka 2010.
HARUSI TRADE FAIR 2011, MAMBO MOTOMOTO
PR&MEDIA Manager of Mustafa Hassanali, Mfaume Shaban speaks during the Press Conference as Mustafa Hassanali (centre) and Hamis Omary, Marketing Manager of Mustafa Hassanali listens in Dar es salaam today.
YANGA WAIGALAGAZA AZAM FC
TIMU ya soka ya Yanga mapema leop, imejiweka kwenye nafasi nzuri, baada ya kuigonga tmu ya Azam FC mabao 2-1 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Yanga inatalajia tena kukigonga na watetezi wa kombe hilo Simba SC hivi karibuni.
Katika mechi hiyo iliyokuwa na upinzani wa hali ya juu, iliwachukua wauza koni ‘Lambalamba’ Azam FC dakika mbili tu kucheka na nyavu za Yanga, baada ya John Boko ‘Adebayor’ kutupia wavuni shuti kali.
Dakika ya 9, Mrisho Ngassa alipiga shuti kali lakini likadakwa na kipa Ivan Knezevic, kabla ya Yanga kujibu kwa shuti kali la Davis Mwape lililogonga mwamba dakika ya 12, huku Jerry Tegete naye akikosa mabao ya wazi matatu kutokana na kupiga mpira fyongo.
Dakika ya 41 Gerson Tegete alijipanga sawa na kupachika bao la kusawazisha baada ya kumpiga chenga kipa na beki wa Azam, huku mwamuzi wa mchezo huo Said Ndege, akimzawadia kadi ya Jano Tegete.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, timu hizo zilitoka Uwanjani zikiwa zinasale ya 1-1.
Baada ya kulejea Uwanjani kwa ungwe ya pili, Tegete tena alipokea mpira na kupachika bao la pili kwa kichwa akitumia vema pasi ya Mwape na kumtoka kipa Nyonzikuru.
Tuesday, March 29, 2011
BAADA YA KUTEMWA TIMU YA TAIFA, MACHAKU AIBUKIA MCHANGANI
IKIWA ni siku chache zimepita toka Kocha Mkuu wa Taifa Stars Jan Poulsen kumtema mshambuliaji wa timu ya Mtibwa Sugar, Salum Machaku 'Sharobaro' katika kikosi chake kilichopambana na Afrika ya Kati kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Afrika uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam na stars kuibuka na ushindi wa bao 2-1, mchezaji huyo jana jioni alinaswa na mtandao huu akicheza ligi ya mchangani katika uwanja wa shule ya msingi Mwembesongo akiichezea timu ya Mikocheni inayomilikiwa na wapiga debe wa stendi kuu ya mabasi ya Msamvu, Morogoro.
Hata hivyo 'staa' huyo licha ya kucheza kwa nguvu zake zote katika mchezo huo alimaliza dakika 90 bila kuifungia bao timu yake hiyo baada ya kubanwa vilivyo na 'Machalii' wa timu ya Black People yenye maskani yake ndani ya kilabu cha kuuza pombe za kienyeji kiitwacho Kaloleni cha Mji Mpya, ambapo katika mchezo huo wa ligi ya kugombea jezi inayojulikana kwa jina la 'Mwembesongo Cup' iliyoandaliwa na wadau wawili wa soka wa mkoani hapa, Daudi Juliani na Master Mage timu hizo zilitoka suluhu.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika mwandishi wetu alizungumza na mchezaji huyo ambapo alidai kwamba kwa sasa yupo mkoani hapa kwa matatizo ya kifamilia na kwamba kuonekana katika ligi hiyo ni moja ya mazoezi.
20% AFANYIWA SHEREHE YA NGUVU NA AFANDE SELE
JANA usiku nyumbani kwa "Mfalme wa vina" nchini, Seleman Msindi 'Afande Sele', palikuwa hapatoshi baada ya msanii huyo kumuandalia sherehe ya kumpongeza msanii mwenzake, Abbas Hamis Kinzasa, maarufu kwa jina la 20% ambaye alifanikiwa kuvunja rekodi ya kutwaa tuzo tano kwa mpigo wakati wa utoaji tuzo za muziki za Kili Music Awards 2011 zilizofanyika Machi 26,wikiendi iliyopita katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Wakati shoo hiyo inafanyika, 20% alikuwa Tabora kwenye moja ya shoo zake ambapo baada ya kumaliza shoo hiyo, Afande Sele alimtaka msanii huyo ashuke mjini hapa kwa lengo la kumfanyia sherehe ya kumpongeza.
Sherehe hiyo ilifanyika kwenye nyumba ya Afande Sele iliyopo pande za Misufini mjini hapa ambapo masela kibao walifurika nyumbani kwa msanii huyo wakinywa na kula usiku kucha.
Katika hali iliyoonyesha kwamba Afande Sele alifurahia kupita kiasi kitendo cha rafiki yake kuibuka kidedea, alijisahau na kutoka kwenye hadhara akiwa amevaa ndala mguu wa kushoto wakati mguu wa kulia akiwa amevaa kiatu cha wazi kitendo kilichowavunja mbavu wageni waliofika kujumuika nao.
Mtandao huu ulimshuhudia mfalme huyo akiwa anakula kilaji kwa staili yake pakiwa "pametapakaa" bia na konyagi za kumwaga.
Monday, March 28, 2011
AMOSI MAKALLA ALIVYOING'ARISHA MVOMERO UINGEREZA
Mbunge wa Mvomero (CCM), Amos Makalla (kushoto) akiwa ameshika kamusi ya kiingereza, aliyopewa na Meneja wa Taasisi ya Misaada ya Elimu nchini Uingereza (School Aid ) Martha Ware. Makalla alikwenda makao makuu ya taasisi hiyo, Uingereza kuishukuru kwa misaada ya kontena la vitabu vya masomo ya sayansi kwa shule za sekondari na kompyuta, iliyotoa kwenda Jimbo la Mvomero. Ware ameahidi kusaidia zaidi elimu Mvomero na kutembelea jimbo hilo siku za usoni.
ZANZIBAR HEROES YAPIGWA TAFU
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu, kampuni ya Future Century Ltd, Helene Masanja wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuisaidia timu ya soka ya Zanzibar, Zanzibar Heroes iliyofanyika mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki. Future Century ndiyo iliyoratibu hafla hiyo ya uchangishaji ambapo jumla ya shilingi 67,981,000 na dola za kimarekani 17,900 zilichangishwa.
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Future Century Ltd, Helene Masanja (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadhamini na wageni mashuhuri waliohudhuria hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuisaidia timu ya soka ya Zanzibar, Zanzibar Heroes iliyofanyika mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki. Future Century ndiyo iliyoratibu hafla hiyo ya uchangishaji ambapo Jumla ya shilingi 67,981,000 na dola za kimarekani 17,900 zilichangishwa.
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein (katikati) Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Future Century Ltd, Helene Masanja (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya soka za Zanzibar Heroes, pamoja na baadhi ya wageni wengine mashuhuri wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuisaidia timu hiyo iliyofanyika mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.
ZANZIBAR HEROES FUNDRAISING GALA
The Zanzibar Heroes Fundraising Gala Dinner was held at the beautiful Zanzibar Beach Resort on 26th March, 2011 with his Excellency, Hon. Dr. Ali Mohammed Shein as the guest of honour. The event was a major success with different dignitaries; Speaker House of Representatives, the Regional Commissioner, Major of Mjini Magharib, Chief Justice of Zanzibar, Ministry of Information, Culture, Tourism and Sports, Minister of Infrastructure and communication, Ministry of Agriculture and Natural Resources, Ministry of President Office without portfolio, Minister of Commerce, Industry and Trade to mention a few.
The venue was filled with a vibrant ambiance where sponsors banners where in full display. The sponsors where; Zan Air, Zanzibar Ports Cooperation, People’s Bank of Zanzibar, Zanzibar Insurance Cooperation, SuperSports Africa, Multi-Choice Tanzania, United Petroleum, Zantel, Zanzibar Beach Resort, Zantel, General Agency Limited, New Africa, Affordable Housing, Explore Zanzibar and Vayle Springs Limited.
The CEO, Helene Masanja lead the way to greet the Hon. Dr. Shein followed by the sponsors CEO’s/ Managing Director who were seated together at the high table. The dignified guests seated at the high table were; the Hon. Dr. Ali Mohammed Shein, the Minister of Information, Culture, Tourism and Sports; Abdliahi Jihad Hassan, CEO of Future Century Limited; Helene Masanja, the Regional Commissioner; Abdallah Mwinyi Hamisi, CEO of General Agency Limited; Anvar Rajpar, CEO of Zan Air; Carls Sailsbury, CCO of Zantel: Nahaat Mahfoudh.
The guests were greeted with an opening dance by the Marimba Group and welcomed into the Karume Hall- Zanzibar Beach Resort and more entertainment was from the talented Kazumuska Band which entertained the guests to the late hours of the night. The MC, Taji Liundi motivated the guests to pledge and encouraged bidders to raise funds for the Zanzibar Heroes.
Martha Enock, the project manager of Future Century Sports Limited used their annual presentation of the events and initiatives planned in 2011 as a platform to engage guests and potential sponsors at the initial stages to enable proper planning to accommodate the team.
The National Coach also provided a compelling speech to motivate the guests and potential sponsors to invest in Zanzibar football. The president’s speech also addressed the guests and was proud to be a patron of the Zanzibar Heroes. Hon. Dr. Shein was seen to be in a fantastic mood and he assisted Taji Liundi in the auction and seemed to better at inspiring guests to bid!
Each guest that pledged was given the opportunity to shake hands with the president and had photos taken. Amongst the pledges was Tsh 5,000,000 by Azam Football Club, Tsh 6,000,000 by Carl Salisbury, USD 4,000,000 by Zanzibar Ports Cooperation, and USD 4,000,000 by the People’s Bank of Zanzibar which totalled totalled to Tsh 39,981,000 and USD 8,300.
The auction raised Tsh 28,000,000 and USD 500; where Abubakar Bakhresa bid for jersey signed by the president at the event for Tsh 10,000,000, jersey signed by the Zanzibar Heroes was taken by the Zanzibar Ports Cooperation at Tsh 2,000,000, the PVR Decoder donated by Multi-Choice Tanzania was bid by People’s Bank of Zanzibar at Tsh 2,000,000.
The camera donate by Afforadable Housing was in fact taken by Afforadable Housing at USD 500. The two portraits of the President of Zanzibar, that was signed during the dinner were taken by Zanzibar Beach Resort and Zanibar Ports Cooperation at Tsh 8,000,000 each. Amongst donations in kind include free housing by Ahmada Yahya Wakili for the National Coach Housing at a value of USD 9,600. The total amount of raised during the event was Tsh 67,981,000 and USD 17,900.
MIRIAM LUKINDO ATAMBULISHA VIDEO YA ALBAMU YAKE
Tunu Pinda akiingia ndani ya ukumbi wa Blue Pearl huku akisalimiana na mke wa Waziri Mkuu wa zamani, Bi Regina Lowassa.
MWIMBAJI wa nyimbo za Injili nchini, Miriam Lukindo, jana alitambulisha video ya albamu yake ijulikanayo kama “Ni Asubuhi” kwa baadhi ya viongozi wa serikali na wabunge katika ukumbi wa Blue Pearl, jijini Dar es Salaam. Uzinduzi kamili wa video hiyo utafanyika tarehe 10 Aprili mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond, pia jijini Dar es Salaam.Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, aliyekuwa mgeni rasmi.
Mama Tunu Pinda (wa kwanza kushoto) akiwa na Miriam Lukindo (katikati), kulia ni Bi Regina Lowassa.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Vicky Kamata (kushoto), akifuatilia hafla hiyo.
Miriam Lukindo akiwajibika kwenye jukwaa.
Wageni katika hafla hiyo wakiserebuka na wimbo wa Miriam Lukindo unaoitwa ‘Amen’.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Martha Mlacha (kulia), akicheza kwa hamasa.
Tunu Pinda akiitambulisha rasmi albamu ya “Ni Asubuhi”.
Regina Lowassa akipakua msosi katika hafla hiyo.
WAZIRI MAIGE NA TERESYA NAO WAPATA KIKOMBE KWA BABU
Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige akipata kikombe cha Babu Ambilikile Mwasapile.
SERIKALI YAIPA DOLE DAWA YA BABU
TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU BABU HUKO SAMUNGE LOLIONDO.
TAARIFA YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII KUPITIA TAASISI ZAKE ZA UTAFITI KUHUSU DAWA YA MCHUNGAJI MSTAAFU AMBILIKILE MASAPILA WA SAMUNGE- LOLIONDO, AMBAZO NI: MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA), TAASISI YA UTAFITI WA DAWA ASILI YA CHUO KIKUU CHA AFYA YA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI, (MUHAS) MKEMI MKUU WA SERIKALI (CGC), TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU (NIMR)
Taarifa ziliifikia serikali kuwa, Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, anatibu magonjwa sugu kwa kutumia dawa aliyooteshwa na Mwenyezi Mungu. Inasemekana kuwa, mchungaji alianza tiba hii tangu mwezi Agosti 2010, lakini watu wengi walianza kumiminika kwenda huko Samunge, kuanzia mwishoni mwa mwezi wa pili, mwaka huu wa 2011.
Kufuatia taarifa hii, serikali iliielekeza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa, ufanyike haraka uchunguzi kuhusu dawa hii na itoe ushauri Serikalini ipasavyo. Baada ya kupokea maagizo hayo, wizara iliteua wataalamu kutoka taasisi zake tukiwemo sisi, TFDA, NIMR, Muhimbili kwa maana ya MUHAS, Mkemia Mkuu na tulijumuisha wataalamu wa hapa wizarani, ili kuifanya kazi hiyo muhimu, akiwemo Msajili wa Tiba Asili na Mbadala.
Hapo Machi 7 mwaka huu, sisi TFDA na wenzetu wanasayansi tulifanya safari kwenda Samunge kuonana na kufanya mazungumzo na Mchungaji mstaafu AmbilikileMasapila. Sisi TFDA na wataalam wenzangu wote, tunamshukuru sana mchungaji mstaafu, kwa ushirikiano na msaada mkubwa aliotupa sisi watafiti wote. kwa kuwa, tulifanya mazungumzo kwa masaa kadhaa kuhusu dawa hiyo jinsi alivyoanza, pia, alituonyesha mti unaotumika na alitupa sehemu mbali mbali za mti huo, kwa uchunguzi zaidi. Kadhalika, alituonyesha jinsi anavyotayarisha dawa hiyo na kutupatia sampuli yake iliyokwishategenezwa, tayari kwa matumizi. Sisi TFDA na wataalamu wenzetu tuliondoka nayo, kwa ajili ya uchunguzi zaidi, kwenye maabara zetu.
Baada ya kurejea kituoni Dar es Salaam, kazi ya utafiti wa dawa hiyo ilianza:
Jambo la kwanza kama watafiti, ilikuwa ni kuangalia na kuhakikisha usalama wa dawa ya Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila kwa watu. Uchunguzi uliofanyika, umetoa matokeo ambayo tumeridhika kuwa, dawa kwa kipimo anachotumia Mchungaji mstaafu AmbilikileMasapila, haina madhara yoyote yanayotambulika kwa sasa, kwa matumizi ya binaadamu.
Kazi inayofuata kwetu sisi watafiti baada ya matokeo haya, ni kuchunguza na kubaini, kama kweli dawa hii inatibu magonjwa hayo matano (5), kama anavyoeielezea yeye Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila. Uchunguzi huu utakapo kamilika, matokeo yake yatatolewa mara moja kwa wananchi wote!.
Hata hivyo, ninaomba kuwatahadharisha kuwa, hatua hii ya uchunguzi, si ya muda mfupi. Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za kisayansi duniani, tafiti za namna hii zina mchakato unaohitaji muda wa kutosha kukamilisha hatua zake mbali mbali, na pia, kufikia viwango na vigezo vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa. Tunafanya hivyo kwa kuzingatia kuwa, dawa hii ni kwa ajili ya matumizi ya binadamu, na inafuatiliwa na wananchi wetu na mataifa mbalimbali.
Sambamba na utafiti katika hatua hii, pia tunafanya uchambuzi wa kisayansi, katika maabara zetu, kwa sampuli tuliyoichukua kwa Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa kuangalia mambo mengine mawili muhimu kama ifuatavyo:
1. Kwa hatua tuliyofikia na taarifa tulizo nazo za dawa hii mpaka sasa, tumeandaa na tunakamilisha taratibu, ili tuweze kufuatilia maendeleo ya kiafya ya wagonjwa 200, ambao wamekubali kwa ridhaa yao wenyewe, kushiriki katika utafiti huu, ili kuona maendeleo yao kiafya, baada ya kunywa dawa ya Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa maradhi walionayo. Hatua hii, inafuata vigezo vyote vya Kitaifa na Kimataifa.
2. Pia tumeweka utaratibu madhubuti, wa kufuatilia matumizi ya mti huu, kama “mmea tiba”, katika sehemu nyingine za nchi yetu, kwani tuna taarifa kuwa, makabila mbali mbali yamekuwa yakitumia mti huu kama tiba. Makabila hayo ni pamoja na; Wagogo, Wamasai, Wabarbaig na Wasonjo kule Samunge.
Kwa niaba ya watafiti na wataalam wenzangu, ninaomba nimalize kwa kusema kwa muhtasari kuwa;:
1. Sisi sote tumeridhishwa kuwa, dawa anayotoa Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, haina madhara yeyote yanayotambulika kwa sasa kwa matumizi ya binadamu. jambo hili mwazoni lilitia wasiwasi Serikali, Wataalam mbalimbali na wananchi kwa ujumla.
2. Kazi hiyo ya utafiti inaendelea ili kubaini magonjwa inayotibu,
3. Katika hatua hii, ninapenda kuwashukuru wataalamu wenzangu wote wa kikosi kazi cha wataalam wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya mkuu wa wilaya, Ngorongoro na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha na wananchi wote kwa kufanikisha zoezi hili mpaka sasa.
4. Pia sisi tunamshukuru sana Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, kwa ushirikiano alioutoa, kwa timu ya watafiti waliofika kumuona, kuanzia siku ya kwanza mpaka leo hii..
Mwisho ninachukua fursa hii, kuwaomba wananchi wawe na subira katika kipindi hiki ili watupe nafasi tuweze kufanya kazi hii ya utafiti na uchambuzi zaidi, kwa utulivu na umakini wa juu kwani duniani kote, tafiti za aina hii, hazina njia ya mkato, nasi tunaahidi kwamba, tutatoa taarifa ya kina mara utafiti utakapo kamilika.
Asanteni na Ninawashukuru kwa kunisikiliza!
MAPACHA 3 WANADI TUZO ZAO KWA MASHABIKI
Baba wa Kalala Junior wa pili kutoka kulia, Komando Hamza Kalala, akiongea jambo kuhusiana na tuzo za wanae.
Mwanamuziki wa bendi hiyo Kalala Junior (kulia), akiwa amenyanyua juu moja ya kadi aliyozawadiwa na mashabiki zake, kushoto kwake ni Jose Mara na Khald Chokora wakiwa na maua mkononi pamoja na tuzo hizo.
Baadhi ya wapenzi wa bendi hiyo wakiwapongeza Mapacha Watatu kwa kutwaa tuzo hizo.
Meneja wa Bendi hiyo, Khamis Dakota, akifurahia kutwaa tuzo hiyo.
Kimwana Manywere 2007, Husna Idd 'Sajenti' (kulia), akifuatilia mchakato mzima wa kunadi tuzo za Mapacha Watatu na rafiki yake.
Sajenti akifuatilia kwa makini Swagger za bendi hiyo.
BENDI ya Muziki wa dansi Bongo, inayoundwa na vichwa vitatu Khald Chuma 'Chokoraa', Joseph Michael 'Jose Mara, na Junior Hamza 'Kalala Junior', maarufu kwa jina la Mapacha Watatu, Usiku wa kuamkia leo, waliweza kunadi tuzo walizotunukiwa na Kili Music Awards, jumamosi iliyopita ndani ya Ukumbi wa Diamond Jublee.
Ishu hiyo ya kunadi tuzo zao ilifanyika katika Ukumbi wa Mzalendo Pub ndani ya Jengo la Millenium Tower, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ambapo bendi hiyo hufanya shoo zake kila siku ya jumapili.
Bendi hiyo ilijinyakulia tuzo ya Wimbo Bora wa Kiswahili na Rapa Bora kwa upande wa bendi ambayo alitwaa kiongozi wa bendi hiyo Khald Chuma 'Chokoraa'.