Social Icons

Thursday, March 31, 2011

DOTNATA AFANYA KUFURU AVUTA `HUMMER`



MSANII matawi ya juu katika tasnia ya filamu Bongo, Husna Mohamed Posh ‘Dotnata’ amefanya kufuru baada ya kutoa ‘burungutu’ kununua‘mkoko’ wa kifahari aina ya Hummer, Amani Jipya limeinyaka.

Akizungumza na gazeti hili muda mfupi baada ya kukamilisha taratibu mbalimbali za kuukomboa mkoko huo kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam, Dotnata alisema kuwa ametumia kiasi cha shilingi za kibongo Milioni 270 kununua ‘mchuma’ huo kutoka katika tawi la kiwanda cha magari hayo huko Detroit, nchini Marekani.

“Kila mtu atasema lake lakini ni kweli nimenunua gari hili kutoka Marekani na nimetumia kiasi cha shilingi milioni 270 mpaka linafika hapa,” alisema Dotnata.

Akiendelea zaidi, msanii huyo mwenye heshima kubwa ndani ya tasnia ya filamu za Kibongo alianika kuwa watu wasimuelewe vibaya kwa kununua gari hilo amefanya hivyo akiwa na lengo la kulikodisha kwenye kwenye sherehe mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili kupunguza makali ya maisha na siyo kutanua nalo kwa matanuzi yasiyo na lazima.

“Leo natarajia kukamilisha usajili hivyo mwishoni mwa wiki hii litakuwa barabarani lakini sitalitumuia kwa matanuzi kama ambavyo watu wanaweza kufikiria, nimepanga kulikodisha kwenye sherehe na hafla mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili linisaidie kujikwamua, ” alimaliza Dotnata.

0 comments: