Baada ya Mchungaji Mwasapila wa Loliondo,Dogo wa Mbeya sasa kuna Bibi ameibuka toka Tabora,Magreth Mutalemwa (40) mwenye Mume na watoto wanne anayeishi Urban Quarter,Uzunguni-Tabora,naye anadaiwa kutoa kikombe cha dozi kwa shs 500,ambacho Kinawatibu magonjwa wale wote wenye kusumbuliwa na magonjwa mbali mbali
Bibi ameanza tangu tarehe 21/March/2011,baada ya kudaiwa kuoteshwa kabla ya tarehe 21 na kuidharau ndoto ile alianza kupata matatizo lakini baada ya kuanza kufanya yale aliyotakiwa kufanya matatizo yakaisha ndio mpaka leo anatibu watu
“Ndio mimewasikia Mchungaji Mwasapila, Babu dogo wa Mbeya na ninavyoona mimi huu ni uwezo wa Mwenyezi Mungu tu,kwani katika uoteshwaji wangu nakumbuka sauti iliniambia tupo watatu na tumetunukiwa roho safi kufanya shuhuli hii ya kutoa tiba.Kwa hiyo naamini hao ni wawili na mimi ni wa tatu na ndio tuliotunukiwa” alifunguka Bibi Magreth Mutalemwa toka Urban Quarter,Uzunguni-Tabora
0 comments:
Post a Comment