Social Icons

Tuesday, March 29, 2011

20% AFANYIWA SHEREHE YA NGUVU NA AFANDE SELE

Seleman Msindi 'Afande Sele' (kulia), akiwa na msanii mwenzake, Abbas Hamis Kinzasa '20%' (kushoto) wakijichana.

JANA usiku nyumbani kwa "Mfalme wa vina" nchini, Seleman Msindi 'Afande Sele', palikuwa hapatoshi baada ya msanii huyo kumuandalia sherehe ya kumpongeza msanii mwenzake, Abbas Hamis Kinzasa, maarufu kwa jina la 20% ambaye alifanikiwa kuvunja rekodi ya kutwaa tuzo tano kwa mpigo wakati wa utoaji tuzo za muziki za Kili Music Awards 2011 zilizofanyika Machi 26,wikiendi iliyopita katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Wakati shoo hiyo inafanyika, 20% alikuwa Tabora kwenye moja ya shoo zake ambapo baada ya kumaliza shoo hiyo, Afande Sele alimtaka msanii huyo ashuke mjini hapa kwa lengo la kumfanyia sherehe ya kumpongeza.

Sherehe hiyo ilifanyika kwenye nyumba ya Afande Sele iliyopo pande za Misufini mjini hapa ambapo masela kibao walifurika nyumbani kwa msanii huyo wakinywa na kula usiku kucha.

Katika hali iliyoonyesha kwamba Afande Sele alifurahia kupita kiasi kitendo cha rafiki yake kuibuka kidedea, alijisahau na kutoka kwenye hadhara akiwa amevaa ndala mguu wa kushoto wakati mguu wa kulia akiwa amevaa kiatu cha wazi kitendo kilichowavunja mbavu wageni waliofika kujumuika nao.

Mtandao huu ulimshuhudia mfalme huyo akiwa anakula kilaji kwa staili yake pakiwa "pametapakaa" bia na konyagi za kumwaga.

0 comments: