Mbunge wa Mvomero (CCM), Amos Makalla (kushoto) akiwa ameshika kamusi ya kiingereza, aliyopewa na Meneja wa Taasisi ya Misaada ya Elimu nchini Uingereza (School Aid ) Martha Ware. Makalla alikwenda makao makuu ya taasisi hiyo, Uingereza kuishukuru kwa misaada ya kontena la vitabu vya masomo ya sayansi kwa shule za sekondari na kompyuta, iliyotoa kwenda Jimbo la Mvomero. Ware ameahidi kusaidia zaidi elimu Mvomero na kutembelea jimbo hilo siku za usoni.
Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla akifurahia mkoba wa nembo ya School Aid aliyopewa na Meneja wa taasisi hiyo, Martha Ware. Makalla yupo nchini Uingereza na akiwa huko, amefanikisha misaada ya vitabu ya sayansi na kompyuta kwa shule 21 za sekondari Jimbo la Mvomero, Morogoro.
0 comments:
Post a Comment