Ndugu Zangu,
” HAYO malumbano ni ya kwao, sisi hatuyajui, wala hatutaki kuyajua.
Tunashughulika na kutekeleza Ilani tu… maneno maneno kama hayo
hayatuhusu”. Anasema John Chiligati, Katibu Mwenezi wa CCM.( NIPASHE,
Jumapili, Machi 27, 2011)
Simba anapozeeka na kukaribia kufa huanza kupoteza uwezo wa kuona,
kunusa na hata kusikia. Lakini, kuna moja ambalo simba ana hakika
nalo, kuwa ameacha simba watoto. Kizazi cha simba kitaendelea.
Chiligati anasema hayajui yanayotokea ndani ya UVCCM na malumbano
yanayoendelea. Hapa kuna mawili; kama ni kweli hayajui ni tatizo, na
kama anayajua na kuamua kutingisha mabega na kujifanya hayaoni wala
kuyasikia ni tatizo kubwa zaidi. Kwa vile, Umoja wa Vijana wa Chama ni
moja ya viungo muhimu kwenye mwili wa chama.
Maana, katika maisha haya ya kisiasa, vijana ndio nguzo na uhai wa
chama chochote kiwacho. Inakuwaje basi, chama kinachozeeka
kinapozungukwa na ’vijana wazee’? Uhai wa chama hicho utakuwa
hatarini. Na hilo ni Neno La Leo. ( Hii ni sehemu ya makala yangu,
RAIA MWEMA, leo Jumatano)
0 comments:
Post a Comment