JINI KABULA ATIMULIWA KWA ‘BWANA’KE’
Na Brighton Masalu
NYANGUMI anaye
piga mbizi katika bahari ya filamu za kibongo asiyeishiwa na vimbwanga kila jogoo wanapouaga usiku mmoja, Miriam Nyafulwa Jolwa ‘Jini Kabula’ juzikati alionja chungu ya maisha baada ya kupewa ‘Red card’ nyumbani kwa anayedaiwa ni ‘bwana’ake’ anaye tambulika mjini kwa nomino ya Waukweli, Mateja20 imebugia ushahidi wa kutosha.
Kikianika mwanya mbele ya balozi wa mateja20, chanzo makini cha habari hii ambacho ni rafiki mkubwa wa mkurya huyo, hivi karibuni kilitambaa na sentensi kuwa , Waukweli amemtimulia mbali Kabula baada ya kumhisi anatoka kimapenzi na mdogo wake aliyemtaja kwa jina la Nchumi.
Kikulacho hicho kiliendelea kuachia paragraph moja baada ya nyingine kwamba maisha ya Kabula na Nchumi kwa sasa yamehamia Makumbusho Kijitonyama kwa rafiki yao ambaye anaelea mjini kwa nembo ya U-miss Ruvuma mwaka 2008 -09, Isabella Mpanda.
“Pamoja na kuhamishia kambi huko Waukweli amekuwa akiwawinda kila kukicha ambapo juzikati aliwakuta Kinondoni wasaga lami katika matembezi ya hapo na pale na kujikuta akimpola simu Nchumi, ambapo Kabula aliingilia, na kusababisha eneo hilo kugeuka ‘Libya’ kwa ugomvi mkubwa lakini mwisho wa siku Waukweli alitokomea kitaa na ‘kilongalonga’ hicho” kilihabarisha chanzo chetu na kuongeza:
“Walimuacha X yuho wa Mr. Chuzi na Nchumi wakilalama huku wakiahidi kufuatilia simu yao na asipo itowa watahakikisha nao wanamlia patro ili kumfuanyia kitu ambacho hatakuja kukisahau katika life yake yote,” kilifunika lips .
Mateja20, baada ya kuzinyaka ‘Nyiuzi’ hizo ilipereruka angani katika jiji la Meck Sadick kikiwasaka wahusika ili kujua yapi ni maziwa na lipi ni tui la nazi juu ya udakaua huo ambapo Jini na mwenzake walikiri kupewa ‘go ahead’ na dumejike huyo kutoka nyumbani kwake, lakini cha ajabu ni kwamba bado ana wafanyia ‘Ugadafi’ bila hatia.
“Nashangaa kwake tumemtokea lakini haishi kututafuta sijui anataka tumfanyie nini ili alizishwe na maisha haya maana yeye yuko na mkewe … sasa sijui bado anahitaji nini kwetu maana aliona sisi hatufai tena kuishi nae na tukamtokea sisi hata hatumueliwi kabisa,” alibainisha Jini Kabula huku akikimbiza macho pembeni mwa kamera ya Mateja20.