Jerry (kushoto) akiingia na wakili wa utetezi, Majura Magafu.
...Akisindikizwa na mkewe, Jennifer John, kuingia chumba cha hukumu.
MTANGAZAJI maarufu wa televisheni na radio nchini, Jerry Murro, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kupokea rushwa, leo ameachiwa huru na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Frank Moshi, baada ya mahakama hiyo kubaini mapungufu yalikuwemo upande wa mashitaka kwenye mwenendo mzima wa kesi hiyo. Akikubaliana na hoja za upande wa utetezi, aliwaachilia huru pia wenzake wawili ambao ni Edmund Kapama na Deogratius Mgasa.
Mshitakiwa namba tatu katika kesi hiyo, Edmund Kapama, akielekea chumba cha hukumu.
Jerry akitoka na mkewe kwa furaha baada ya kuachiwa huru.
…Akionyesha ishara ya dole baada ya kuachiwa huru.
…Akiongea na wanahabari baada ya kuachiwa huru.
Mapaparazi wakimzingira (Jerry) kumpa pole na kumhoji.
Jerry akiondoka mahakamani na mkewe.
0 comments:
Post a Comment