Afisa Viwango wa Tigo, Pamela Shellukindo (kulia), akifafanua juu ya shindano hilo, na mfanyakazi mwenzake wa idara hiyo Benedict Mponzi.
Benedict Mponzi akijibu moja ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwajibika kwenye kikao hicho.
KAMPUNI YA mawasiliano ya simu za mkononi Tanzania, Tigo, leo, Novemba 30, imetangaza shindano lenye ujumbe wa ‘Zamu Yako Kushinda’ itayoendeshwa ndani ya siku 82 ambapo mshindi wa kwanza atazawadiwa 4,000,000.
Haya yalielezwa na maofisa wa Tigo, Pamela Shellukindo na Benedict Mponzi katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Kwa mujjibu wa maofisa hao, mshindi wa pili atajinyakulia kompyuta aina ya ‘Laptop’ mpya kutoka kampuni ya Samsung.
Tigo imeamua kuanzisha shindano hilo ili kuwapa changamoto wateja wake na kutoa nafasi za kushindi kwa wale wa malipo ya kabla na ya baadaye ambao walishiriki katika shindano lililopita.
Washiriki wanatakiwa kutuma ujumbe mfupi kuanzia saa sita kamili usiku wa tarehe 30/11/2011 mpaka saa 11: 59 usiku wa tarehe 19/12/2012.
Ili kushiriki, unatakiwa kutuma neno ‘Tigo’ kwenda namba 15571, kila meseji itagharimu kiasi cha shilingi 450, na wanaotakiwa kushiriki ni wale wote wenye umri wa miaka 18 tu.
0 comments:
Post a Comment