Ni tukio la kuhuzunisha lililobeba majonzi tele ambapo staa wa Kundi la Orijino Komedi, Joseph Shamba ‘Vengu’, amekumbwa na mkasa mzito ambao umesababisha mashuhuda watoe kauli ya kutemea mate chini.
Staa huyo ambaye ‘hufiti’ zaidi anapoigiza kama demu, alikutwa akiwa hana fahamu, umbali wa mita chache kutoka Klabu ya Sun Cirro, Sinza, alfajiri ya Jumapili iliyopita.
Ishu nzima inasimuliwa na mashuhuda kuwa usiku wa kuamkia Jumapili, Vengu ambaye inadaiwa ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa, alionekana akifakamia pombe kwa staili ya ‘kata mti panda mti’ au ukipenda unaweza kuita ‘bandika bandua’.
Alifafanua kwamba wakati Vengu anatia ‘maguu’ kwenye baa hiyo alionekana na majeraha mdomoni ambayo haikueleweka yalitokana na nini, ingawa zilikuwepo hisia kwamba alifanyiwa mchezo mbaya.
“Si unajua tena wikiendi, kila mtu na hamsini zake lakini alfajiri watu ndiyo wakashtukia kumbe jamaa aliangusha gari kwenye kona moja hivi ambayo ilimsababishia kutoonekana haraka,” alisema ‘sosi’ wetu na kuongeza:
“Ile alfajiri katika kumsaidia ndiyo tukamhifadhi kwa huyo msamaria mwema.”
“Nilipompigia simu Masanja kumpa taarifa alionesha kukasirishwa na kukemea tabia za mwenzake halafu akakata simu. Baadaye meneja wa kundi lao, Seki (Sekioni David), alikuja kumchukua,” alisema msamaria mwema huyo.
Kutokana na kupitiwa usingizi akiwa anaendesha, Vengu alisababisha foleni kwenye Barabara ya Shekilango, Bamaga, Dar, hivyo madereva wengine kumpigia honi mfululizo lakini hakuzinduka.
Baadaye, watu walilizunguka gari la Vengu na walipomuona, Seki alipigiwa simu ambaye alifika haraka na kuvunja kioo cha gari, akachomoa ‘loki’ na kuliendesha.
KWETU SISI
Tunamtaka Vengu kubadilika haraka iwezekanavyo kutoka kwenye tabia aliyo nayo ya ulevi wa kupindukia. Pia anahitaji kujitambua kuwa yeye ni msanii ambaye ni kioo cha jamii, hivyo anapaswa kuwa mfano wa kuigwa.