Social Icons

Sunday, June 13, 2010

TANZANIA MITINDO HOUSE YAZINDUA KITUO CHA KUCHEZEA WATOTO YATIMA

KAMPUNI ya Mitindo House leo iimefanikisha sherehe ya Uzinduzi wa Kituo cha kuchezea watoto yatima iliyofanyika Mwera Manispaa ya Temeke ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Oil &Industurial Technology T.LTD. Rahma A. Al-Kharoosi.

Akiongea katika ufunguzi huo Mwenyekiti wa Mitindo House Khadija Mwanamboka alisema kwamba wamelazimika kufungua kituo hicho kutokana na uhaba mkubwa wa sehemu za kuchezea watoto yatima hapa nchini na vile vile amekuwa akitafuta namna ya kuwakutanisha pamoja watoto hao ili waweze kujumuika na kucheza pamoja.

Naye Rais wa Oil &Industrial Technology T. Limited Rahma Al-Kharoosi alisema kuwa kampuni yake ilmelazimika kudhamini ishu hiyo kutokana na kuguswa kwake siku nyingi na kwamba hadi sasa iko kwenye mchakato wa kuwakutanisha watoto sehemu moja hasa siku ya watoto Duniani ili waweze kula na kufurahi pamoja.

Mgeni Rasmi Rahma Al-Kharoosi (Kushoto) akipokelewa na Mwenyeji wake Khadija Mwanamboka muda mfupi baada ya kuwasili eneo hilo.

Rahma Al-Kharoosi (katikati) akifungua ubao unaoonyesha jina la Kituo hicho kulia kwake anayeshuhudia zoezi hilo ni Meneja wa London Mine Camp Mohamed Khatrush akiwa na baadhi ya watoto na wageni waliohudhulia shughuli hizo.

Khadija Mwanamboka (kushoto) akimpa mkono wa pongezi mgeni Rasmi baada ya kumaliza zoezi la ufunguzi.

Mgeni Rasmi akiwa amekumbatiana na mmoja wa watoto yatima waliokuwepo katika shughuli hizo.

Baadhi ya watoto wakijaribu kuimba na wimbo na mgeni rasimi muda mfupi baada ya kuzindua mpango huo.

Rahma Al-Kharoosi aliyebeba mtoto akibembea na watoto katika moja ya Bembea zilizopo mahari hapo.

Mwenyekiti wa kituo hicho (kulia) akionyesha tano kwa furaha na mgeni rasmi muda mfupi baada ya kuhitimisha zoezi la ufunguzi wa ishu hiyo.

Fiderene Iranga (kushoto)akibadilisha mawili matatu na mmoja wa wageni waarikwa waliyohudhuria uzinduzi huo.

Mgeni rasmi akionyesha aina ya chakula anachokipenda mara baada ya kukaribishwa kupata msosi.

0 comments: