Social Icons

Thursday, June 10, 2010

ZAIN YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA JIVUNIE SMS


Kampuni ya Simu za Mkononi ya Zain leo imekabidhi jumla ya shilingi milioni moja (1,000,000) kwa washindi wawili wa Promosheni ya Jivunie SMS.Washindi waliokabidhiwa zawadi zao za pesa taslimu leo ni wale waishio jijini Dar es Salaam, wakati washindi waishio nje ya jiji la Dar es Salaam watakabidhiwa zawadi zao hivi karibuni.

Akiwataja washindi waliojizolea kitita cha laki tano kila mmoja, Meneja Masoko wa Zain Tanzania Constantine Magavilla, alisema ni Mashimba Mashimba mkazi wa Tabata Kisiwani jijini Dar es salaam na Philipo Masonda, Osole David Gilina na Godwin Joseph.

Meneja Masoko wa Zain Tanzania, Constantine Magavilla (kulia) akimkabidhi kitita cha sh.500,000/= Philipo Masonda ndani ya makao makuu ya ofisi za Zain Morocco jijini Dar es Salaam.


Mshindi wa Jivunie SMS Mashimba Mashimba akipokea kitita kiasi chake kutoka kwa Constantine Magavilla makao makuu ya Zain Morocco jijini Dar es Salaam



Washindi wote wawili wakiwa wameshikilia pesa zao kwa tabasam muda mfupi baada ya kukabidhiwa.



0 comments: