Social Icons

Friday, June 18, 2010

RBP NA TWIGA STARS WALIVYOADHIMISHA SIKU YA 'MTOTO WA AFRIKA’

KAMPUNI ya RBP & Industrial Technology .T. Limited chini ya Rais wake Bi Rahma A. Al-Kharoosi Jumatano wiki hii ilijumuika na watoto zaidi ya mia moja kutoka vituo mbalimbali vya yatima hapa nchini katika kusherehekea Siku ya Mtoto wa Afrika katika ufukwe wa South Beach, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Akiongea katika hafla hiyo Al-Kharoosi alisema ameamua kuwakutanisha watoto katika ufukwe huo ili waweze kufurahi na kucheza pamoja kutokana na mapenzi yake makubwa kwa watoto.

Rahma ambaye pia ni mlezi mkuu wa timu ya wanawake ya taifa (Twiga Stars) aliongeza kwamba siku hiyo ya Mtoto wa Afrika ilikuwa siku nzuri kwake kukaa na timu hiyo kabla ya mchakato mpya wa kwenda kuwania fainali za Kombe la Afrika zitakazofanyika Afrika Kusini mwezi wa kumi mwaka huu.


Rahma A.Al-Kharoosi (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars katika ufukwe wa South Beach katika Siku ya Mtoto wa Afrika


Mpipga picha wetu Musa Mateja (kushoto) akiwa katika pozi na mwanamitindo maarufu nchini,
Fidelina Iranga


Mwandaaji wa hafla hiyo, Al-Kharoosi (wa pili kushoto) akifurahia jambo na watoto yatima; wengine ni baadhi ya walezi wa watoto hao


Baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo na walimu wa watoto waliohudhuria sherehe hizo wakiwa kwenye picha ya pamoja.



Meneja mkuu wa RBP & Industrial Technology.T. Limited, Ibrahim Khatrush (kushoto), akiwa na kaka yake, Mohamed Khatrush, ambaye ni meneja wa kampuni ya London Mine Camp iliyo chini ya kampuni hiyo.


Mmoja wa watoto yatima akilishwa chakula na Bi Al-Kharoosi katika sherehe hizo.


Nahodha wa Twiga Stars, Sophia Edward Mwasikili, akiongea na waandishi wa habari siku hiyo.


Ibrahim Khatrus mwenye miwani akijipatia chakula.


Rais wa Kampuni hiyo naye hakuwa nyuma kujichukulia msosi mahali hapo.


Rais wa RBP akipiga ‘cheers’ na mmoja wa watoto yatima.



Fideline Iranga akijaribu kupekuwa habari kwenye kompyuta yake na rafiki yake, aliyejulikana kwa jina moja la Martin.


Bi Al-Kharoosi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya timu nzima iliyokuwepo katika hafla hiyo.



Sophia Edward (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mlezi wa timu hiyo, Bi Rahma Al-Kharoosi, na wa mwisho kulia ni mmoja wa wachezaji wa timu hiyo.







0 comments: