Social Icons

Thursday, June 10, 2010

ADAMU MCHOMVU: DEMU WANGU ANA WIVU ILE MBAYA!


Leo katika pande hizi tunakudondoshea presenta mwenye heshima kubwa kwa vijana ‘anayehosti’ programu ya XXL kunako Redio ya Watu, Clouds FM, Adamu Mchomvu ‘Brother from another Mother’.
Huyu jamaa alizaliwa miaka 26 iliyopita huko Kahama mkoani Shinyanga, lakini akakulia kwa ‘machalii’ Arusha maeneo ya Silentini Sakina ambapo aligonga Primary katika Shule ya Meru kabla ya kujiunga na Sekondari ya Kaloleni, zote za mkoani Arusha. Kutoka hapo Adamu alikwenda kugonga ‘five na six’ nchini Uganda katika Shule ya Ntinda View iliyopo katika Jiji la Kampala. Ili kujua ‘in and out’ ya Brother from another Mother, tuungane katika sindano kumi za maswali ya moto.

TQ: Unaweza kukumbuka ni lini na ilikuwaje ukajiunga na fani ya utangazaji?

ADAMU: Utangazaji nilianzia Uganda na stori nzima ilikuwa hivi; Ilitokea noma pale skuli nikatimuliwa baada ya kuingilia ugomvi wa mademu wawili mmoja kutoka Bongo. Katika lile soo nilikuwa nawaamulia wale mademu ndipo mtangazaji mmoja aliyeitwa Isack akasikia sauti yangu na kunifuata kisha akanitaka nifanye Tangazo la Vicks Kingo ambapo nilipoteza mbaya. Baada ya hapo nilipata chansi ya kuruka hewani na kipindi changu cha burudani katika chaneli ya Redio ya Green FM ya nchini Uganda. Baadaye nilirudi nyumbani na kuwaeleza wazazi stori ilivyokuwa na wakaniruhusu kufanya kile kilichokuwa moyoni.

TQ: Baada ya hapo ilikuwaje hadi hapa ulipofikia?
ADAMU: Nilipotimba Dar nilijiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari cha DSJ ambapo nilisomea Diploma ya fani hiyo, lakini kabla sijamaliza Clouds FM waliniona na wakanichukua na ndiyo unaniona kama hivi nakimbiza ile mbaya.

TQ: Kazi yoyote ina vikwazo vyake. Je, wewe ni mambo gani unakutana nayo yanakunyima kupiga mzigo ili kufikia malengo yako?
ADAMU: Unajua watu wananichukulia tofauti, mara najisikia, naringa, ukipanda bajaj umefulia na mengine yanayofanana na hayo yanayosababishwa na umaarufu.

TQ: Usumbufu wa Mademu vipi?
ADAMU: Kusema kweli usumbufu ni mkubwa. Kwa siku naweza kupokea meseji zaidi ya kumi za mademu wanaotaka niwe nao ‘but’ mimi huwa nawapigia kimya ‘coz’ nina demu mwenye wivu ile mbaya.

TQ: Wewe unahusika na kuwapromoti maandagraundi, Je, usumbufu ukoje?
ADAMU: Hawa jamaa wanaishia tu kueneza lawama kwamba sisi ni wabaya na tunawabania, lakini ukweli ni kwamba pale ofisini kuna utaratibu wa kupokea kazi mpya na kuzikiliza kisha kuzipeleka hewani, sasa jamaa ukiwaelewesha hawaelewi kabisa, wanaona mimi ndiyo mbaya wao.

TQ: Kuna tuhuma kwamba mnaweka kapuni baadhi ya kazi za wasanii na wengine mnawapa promo, je, hii ikoje?

ADAMU: Kama nilivyoeleza awali hakuna kitu kisicho na utaratibu. Wengine ukiwaambia wafuate utaratibu wa kuleta kazi zao zisikilizwe kwanza ndipo ziende hewani, hawataki na badala yake wanaishia kulalama na kueneza mbovu mbovu kitaa.

TQ: (swali la kifuta jasho) Umeoa? Na kama bado, utaoa lini?
ADAMU: Sijaoa ila nina wangu. Muda wa kuoa ukifika nitasema but siwezi kusema lini.

TQ: Mafanikio vipi?
ADAMU: Nina gari, ploti mbili Arusha na Dar. Nina uwezo wa kubadili jinsi (suruali) na msosi ‘so’ namshukuru Mungu.

TQ: Baadhi ya mastaa Bongo ni zoa zoa wa mademu, hii kwako imekaaje?
ADAMU: Hayo mambo mimi sina kabisa mzazi.

TQ: Nini matarajio yako ya baadaye?
ADAMU: Nina mpango wa kuja kumiliki kampuni moja kubwa sana ya burudani.





0 comments: