Social Icons

Wednesday, June 23, 2010

Vengu, tutemee mate chini

Na Richard Bukos
Ni tukio la kuhuzunisha lililobeba majonzi tele ambapo staa wa Kundi la Orijino Komedi, Joseph Shamba ‘Vengu’, amekumbwa na mkasa mzito ambao umesababisha mashuhuda watoe kauli ya kutemea mate chini.

The 5star Paper, Risasi Mchanganyiko lina ‘full details’ kwamba Vengu, anadaiwa kufanyiwa mchezo mbaya baada ya kugida ‘tingas’ kwa pesa zake za mfukoni lakini mwisho wa sinema alikutwa ‘amejitelekeza’ bila kujitambua, Sinza, Dar.
Staa huyo ambaye ‘hufiti’ zaidi anapoigiza kama demu, alikutwa akiwa hana fahamu, umbali wa mita chache kutoka Klabu ya Sun Cirro, Sinza, alfajiri ya Jumapili iliyopita.

Mapaparazi wetu, ‘walinyetishwa’ kuhusu mkasa huo wa Vengu, Jumapili majira ya saa 5 asubuhi na kufika eneo la tukio ambapo walimkuta staa huyo wa kuwavunja watu mbavu ‘runingani’ akiwa amehifadhiwa nyumbani kwa msamaria mwema mmoja.
Ishu nzima inasimuliwa na mashuhuda kuwa usiku wa kuamkia Jumapili, Vengu ambaye inadaiwa ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa, alionekana akifakamia pombe kwa staili ya ‘kata mti panda mti’ au ukipenda unaweza kuita ‘bandika bandua’.

Mmoja wao ambaye hakutaka jina lake lipambe ukurasa, alidai kwamba mpango mzima wa ‘kutandika maji’ ulifanyika kwenye baa moja ‘bubu’ na aligida hadi usiku mnene ambapo alihamia kiwanja jirani na kuendeleza libeneke hadi alipopoteza ‘netiweki’.
Alifafanua kwamba wakati Vengu anatia ‘maguu’ kwenye baa hiyo alionekana na majeraha mdomoni ambayo haikueleweka yalitokana na nini, ingawa zilikuwepo hisia kwamba alifanyiwa mchezo mbaya.

Mpashaji huyo aliendelea kudai kwamba alipofika kwenye baa hiyo, Vengu aliendeleza makamuzi ya kukata maji hadi alipopoteza ‘netweki’.
“Si unajua tena wikiendi, kila mtu na hamsini zake lakini alfajiri watu ndiyo wakashtukia kumbe jamaa aliangusha gari kwenye kona moja hivi ambayo ilimsababishia kutoonekana haraka,” alisema ‘sosi’ wetu na kuongeza:
“Ile alfajiri katika kumsaidia ndiyo tukamhifadhi kwa huyo msamaria mwema.”

Akizungumza na paparazi wetu, msamaria huyo alisema kuwa baada ya kumpokea Vengu, alitafuta namba ya msanii mmojawapo wa Orijino Komedi ambapo aliipata ya Emanuel Mgaya ‘Masanja’ kisha kumpa taarifa hizo.
“Nilipompigia simu Masanja kumpa taarifa alionesha kukasirishwa na kukemea tabia za mwenzake halafu akakata simu. Baadaye meneja wa kundi lao, Seki (Sekioni David), alikuja kumchukua,” alisema msamaria mwema huyo.

Mara kadhaa Vengu amekuwa akiripotiwa kukutwa na matukio ya aina hiyo ambapo ukiachilia mbali hilo, mwaka jana alizimika na kulala barabarani nyuma ya usukani wa gari.
Kutokana na kupitiwa usingizi akiwa anaendesha, Vengu alisababisha foleni kwenye Barabara ya Shekilango, Bamaga, Dar, hivyo madereva wengine kumpigia honi mfululizo lakini hakuzinduka.

Baadaye, watu walilizunguka gari la Vengu na walipomuona, Seki alipigiwa simu ambaye alifika haraka na kuvunja kioo cha gari, akachomoa ‘loki’ na kuliendesha.
KWETU SISI
Tunamtaka Vengu kubadilika haraka iwezekanavyo kutoka kwenye tabia aliyo nayo ya ulevi wa kupindukia. Pia anahitaji kujitambua kuwa yeye ni msanii ambaye ni kioo cha jamii, hivyo anapaswa kuwa mfano wa kuigwa.

0 comments: