Social Icons

Sunday, November 28, 2010

T- PAIN ALIVYO WAPAGAWISHA MASHABIKI BONGO!!

Dancehall kutoka Jamaica, Windel Benetol Edward “Gyptian” akifanya vitu vyake jukwaani wakati wa STR8 Muzik Festival Inter-College Special 2010 katika viwanja vya Posta Kijitonyama Dar es Salaam jana na kudhaminiwa na kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kupitia chapa yake ya SM.
Mwana Hipi Hop kutoka nchini Marekani , Faheem Rasheed Najm, “T-Pain” akitumbuiza wakati wa Tamasha Maalum la STR8 Muzik Festival Inter-College Special lililofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama Dar es Salaam usiku wa kuamkia jana na kudhaminiwa na kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kupitia chapa yake ya SM.


Baadhi ya wanenguaji wa T-Pain wakionyesha Swagger zao
T-Pain akimwaga Swagger zake kwa mashabiki waliofurika ndani ya viwanja hivyo.
Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Shawn Mims “Mims” akishambulia jukwaa.

Joh Makini akikamua katika tamasha hilo.
C Pwaa , akitumbuiza jukwaa wakati wa Tamasha Maalum la STR8 Muzik Festival Inter-College Special 2010 lililofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

C Pwaa akiwajibika na vijanawake jukwaani hapo.
Baadhi ya mashabiki wakishangilia baada ya kupagawishwa na wanamuziki waliokuwa wakitumbuiza katika Tamasha hilo.
Baada ya kutoka katika tamasha hilo Mateja20, ilitembele pande za Kinondoni katika Ukumbi wa Mango Garden, ambako Bendi ya African Stars International 'Twanga Pepeta' walikuwa wakimwanga burudani zao na kubahatika kumnasa Mwanamuziki kutoka nchini Kongo Bozi Boziana akifatilia kwa makini shoo ya Bendi hiyo.
Bozi Boziana akiangalia jinsi nyonga za watoto wa Asha Baraka, zilivyokuwa zikizungushwa. (kulia kwake), ni baadhi ya wanenguaji wake wakifuatilia makamuzi hayo kwa pamoja.
Kevi, wa pili kushoto akiwa kwenye pozi na washikaji zake katika shoo ya T- Pain, iliyofanyika katika Viwanja vya Posta jijini Dar, usiku wa kuamkia leo.
Muba (kulia), akiwa kwenye pozi na marafiki zake ndani ya ukumbi wa Mango Gardeni jijini Dar es Salaam.
Khaleed Chuma 'Chokoraa' (Kulia), akimnong,oneza jambo Pedeshee Bitus muda mfupi baada ya kukutana ndani ya ukumbi wa Mango Garden.
Pedeshee Bitus (kushoto) akimsikiliza kwa makini Chokoraa.
Viburudisho vikiwa kwenye pozi makini katika shoo ya T-Pain iliyofanyika ndani ya Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Miss Bagamoyo 2010 Winifrida David (kulia), akijimiminia kilaji kwa kwenda mbele.

Thursday, November 25, 2010

SENDOFF YA DADA 'AKE AUNT EZEKIEL YAFANA

Baadhi ya wanakamati wa shughuli hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Usiku wa kuamkia leo pale pande za Victoria, katika Ukumbi wa Estana, kulifanyika Sherehe ya kumuaga Zawadi Ezekiel, ambaye ni dada yake na muigizaji wa filamu nchini Aunt Ezekiel. Sherehe hiyo ilianza majira ya saa 12:00 jioni na kumalizika mishare ya saa 6:30 usiku.
Kwa mjibu wa wageni waliohudhuria sherehe hiyo walisema kuwa walifurahishwa na maandalizi ya kamati tendaji na kwamba waliburudika vilivyo na hakuna sehemu iliyopwaya hata kidogo.
We' Sajenti kama vipi nyanyuka basi unisindikize ... si unajua nimepombeka kiana bwana eeh!!
Aunt Ezekiel (Kulia) akiwa na Dada yake Zawadi, ambae ni Bi. Harusi mtarajiwa, muda mfupi baada ya kumalizika sherehe hiyo.
Bi. Harusi akiwa kwenye pozi na baadhi ya wageni waarikwa.
Nice Chande akliomba msaada wa kunyanyuliwa baada ya kushindwa kubalansi viatu vyake.

Nice Chande akiwa kwenye pozi na Habiba.
The Great Kanumba akijiandaa kutupia mpunga na swahiba yake Ray katika sherehe hiyo.


Bi. Harusi akimrisha keki mshenga wake.
Aunt Ezekiel na wenzake wakizungusha nyonga .
Mayasa, akimkabidhi keki Bi. Harusi tayari kwa kuwakabidhi wazazi wake.
Johari (katikati), akibadirishana mawazo na wenzake aliyokuwa ameketi nao.

Mama Jesca (katikati), akifuatilia sherehe hiyo kwa makini zaidi.
Mc wa shughuli hiyo Maimartha Jesse akiongea jambo katika hafla hiyo.

VIJIMAMBO VYA KAMERA YA MATEJA20 KITAANI

Kama hivi mshikaji alinaswa akiwa ameuchapa usingizi mkali usiku wa manane bar.
Mrembo nae akiwa ....
Unaona Baaana ...
Mbonji mtindo mmoja.
Aaah!! freshii...

PATCHO MWAMBA AMSHUKURU KIRUA!!

MWANAMUZIKI wa Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' Patcho Mwamba, Hatimaye ameipua Single yake mpya inayokwenda kwa jina la Kirua.
Akiongea na Mateja20, hivi karibuni Patcho alisema kwamba amelazimika kufikisha shukrani zake kwa Pedeshee Mohamed Kirua, kwa njia ya wimbo kutokana na mambo mengi mazuri aliyomfanyia.
Patcho alisema kwamba tangu amekuwepo kwenye geme, kumekuwa na Mapedeshee wengi wanaomsapoti na yeye kuwapa shukrani zake lakini hajaona mwenye upendo na moyo wa kusaidia kama ilivyo kwa Kirua.
Single hiyo yenye ujumbe wa shukrani na sifa kende kede. Baada ya kukaa chini na kufiria sana namna ya kutoa shukrani hizo ambapo njia pekee aliona atumie sanaa yake ambayo pia itawafikia watu wengine wenye vipaji na sifa kama hiyo.


JUKWAA LA SANAA LAPITISHA KIAPO NA AGANO WA PARAPANDA

Mwanamitindo maarufu nchini Lisa Jensen akiwasilisha mada kuhusu ‘Fursa ya Wasanii Katika Fani ya Matangazo’ kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu hii.Wengine kutoka kushoto ni Mratibu wa Jukwaa Ruyembe Mulimba na Mkurugenzi wa Parapanda,Mgunga Mwamnyenyelwa.

Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa la Parapanda,Mgunga Mwamnyenyelwa akizungumzia wimbo wa Kiapo na Ahadi uliozinduliwa na kundi lake kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu hii.Kulia kwake ni Lisa Jensen na Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego.
Kundi zima la Parapanda likiutambulisha rasmi wimbo wa Kiapo na Agano kwenye Jukwaa la Sanaa.Wimbo huo ni mkali na uliwavutia wadau wa sanaa.

Wadau wakiusikiliza kwa makini wimbo wa Kiapo na Agano.



KUNDI la Muziki wa asili nchini la Parapanda Jumatatu hii kupitia Jukwaa la Sanaa limezindua wimbo wake mpya wa Kiapo na Agano unaolenga kuwabana wanasiasa walioahidi ahadi mbalimbali wakati wa kampeni za uchaguzi kuzitekeleza kwa vitendo na kumaliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Akizungumza kabla ya uzinduzi wa wimbo huo ambao umebeba ujumbe mzito kwa wanasiasa, Mkurugenzi wa kundi hilo,Mgunga Mwamnyenyelwa alisema kwamba, wimbo huo ambao una ushairi ndani yake unalenga kuwakumbusha wanasiasa kwamba ahadi zilizoahidiwa ni agano baina yao na wanachi hivyo hawapaswi kuwahadaa na kuwalisha maneno matupu bali wanachotakiwa kufanya ni kuhimiza, kusimamia na kuwaletea maendeleo ya kweli bila kujali tofauti zao.
“Kila aliyekuwa akiomba kura alikuwa akiingia agano na wananchi hivyo, wimbo huu unasisitiza kwamba, miaka mitano ijayo kuna wananchi wametoka jasho na machozi katika kuwaingiza madarakani watataka waone wanatekelezewa ahadi zote” alisisitiza Mgunga.
Naye Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego mbali na kuwapongeza wasanii waliopata nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa mwaka huu, aliwataka wasanii kuwa mstari wa mbele kuwabana wanasiasa juu ya ahadi mbalimbali walizoahidiwa ili wasiwe ni wa kutumika tu wakati wa chaguzi kisha kubaki na shida zao.
“Wasanii tumeshiriki sana kuwaingiza wanasiasa bungeni lakini turudi nyuma na tuanze kufanya tathimini ya kina na kuwafuatilia ni kwa kiasi gani wanatekeleza yake waliyotuahidi.Tusipofanya hivyo tutakuwa tunajisaliti wenyewe,Parapanda wameanza nawapongeza kwa hili” aliongea kwa msisitizo Materego.
Awali,Mwanamitindo maarufu nchini,Lisa Jensen aliwasilisha mada yake kususu ‘Fursa ya Wasanii Katika Fani ya Matangazo’ ambapo aliwaasa wasanii kuwa na maadili bora, kuingia darasani na kusaka fursa mbalimbali ili kujenga uwanja mpana zaidi katika uelewa wa mambo na kuwa na fani zaidi ya moja katika kusaka mafanikio kisanaa.
Alisisitiza kwamba, tasnia ya mitindo inaweza kutoa ajira kubwa zaidi kwa wasanii kama wadau wataamka, wakajituma, kusaka wigo mpana wa uelewa wa mambo na kuichukulia sanaa kama kazi ya kuwapa kipato na maisha kwa ujumla.Katika hili alisema kwamba, lazima wasanii wahame kutoka kwenye dhana ya kutegemea makampuni ya watu na badala yake wajenge umoja imara na kuwa na ushirika ambao utawasaidia katika kujiendesha wenyewe badala ya kuwa tegemezi.
Jukwaa la sanaa litaendelea tena Jumatatu ijayo Tarehe 29/11/2010 ambapo muasisi wa blog nchini ambaye ni mmiliki wa blogu maarufu ya jamii Issa Michuzi atawasilisha mada kuhusu Mchango wa Blogs katika kukuza Sanaa..



BARAZA LA MAWAZIRI MABADLIKO SURA 24 MPYA



RAIS Jakaya Kikwete jana alitangaza Baraza lake jipya la Mawaziri, huku akiwatema mawaziri tisa wa zamani, akiwemo Profesa Juma Kapuya na Mohameid Seif Khatib ambao wamekuwa mawaziri kwenye awamu tatu tofauti.
Baraza hilo jipya pia halina sura za wabunge ambao wamekuwa wakitajwa sana na vyombo vya habari kuwa wamepewa uwaziri, akiwemo Januari Makamba ambaye ni mtoto wa katibu mkuu wa CCM, mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango na waziri wa zamani wa fedha, Zakhia Meghji.
Pia kwenye orodha hiyo, hakuna jina la mweka hazina wa CCM, Amos Makalla ambaye pia alikuwa akitajwa sana kuwa ameteuliwa kuwa waziri mdogo wa fedha baada ya kushinda ubunge kwenye Jimbo la Mvomero.
Hata hivyo, majina mengine yaliyotajwa sana kama spika wa zamani wa Bunge, Samuel Sitta, mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe na Lazaro Nyalandu yamo kwenye baraza jipya ambalo lina kazi kubwa ya kuhakikisha ilani ya CCM, ambayo inajumuisha ahadi nyingi kubwa alizozitoa Rais Kikwete kwenye kampeni, zinatimizwa ili nguvu ya chama hicho iliyotikiswa kwenye uchaguzi wa mwaka huu iweze kurejea.
Katika uteuzi huo mpya Kikwete amemuacha Profesa Kapuya ambaye katika serikali iliyopita alikuwa Waziri wa Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana, nafasi ambayo aliishikilia kuanzia mwaka 2008. Katika baraza la kwanza la JK, Kapuya alipewa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Nafasi ya Kapuya sasa imechukuliwa na Gaudensia Kabaka
na imebadilishwa na kuwa Wizara ya Kazi na Ajira, huku Dk Makongoro Mahanga akiendelea kuwa naibu wa wizara hiyo.
Kikwete pia amemtema Mohammad Seif Khatib, ambaye alikuwa waziri tangu enzi za serikali ya awamu ya pili. Katika baraza lililopita, Seif Khatib alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye alishughulikia masuala ya Muungano, nafasi ambayo sasa imekwenda kwa Samia Suluhu.
Rais Kikwete pia amemtema Profesa Peter Msolla aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia pamoja na naibu wake Dk Maua Daftari.
Badala yake Rais Kikwete amemteua Profesa Makame Mnyaa Mbarawa aliyempa ubunge wa kuteuliwa wiki iliyopita, Charles Kitwanga akiteuliwa kuwa naibu waziri.
Kikwete pia amemuacha Prof David Mwakyusa, ambaye alikuwa daktari wa Mwalimu Julius Nyerere. Prof Mwakyusa aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwenye serikali iliyopita na nafasi yake imekwenda kwa Dk Haji Hussein Mpanda huku naibu wake akiwa ni Dk Lucy Nkya ambaye serikali iliyopita alikuwa naibu wa Wizara wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto.
Aliyekuwa naibu waziri katika wizara hiyo Dk Aisha Kigoda alishindwa kupenya katika mchakato wa awali wa kuwania ubunge ndani ya CCM.
Margareth Sitta, aliyeshika Wizara Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na kuongoza kwa mafanikio kuundwa kwa Sheria ya Mtoto, hayumo kwenye baraza jipya na badala yake nafasi yake imekwenda kwa mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wa CCM, Sophia Simba, ambaye atasaidiwa na Umi Ali Mwalimu.
Rais pia hakumteua katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, John Chiligati kuingia kwenye baraza jipya baada ya kuiongoza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kipindi cha miaka mitatu. Naibu wake, Hezekiah Chibulunje pia ametemwa.
Nafasi ya waziri imekwenda kwa mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-Habitat), Anna Tibaijuka, ambaye atatakiwa kupunguza migogoro mingi ya ardhi inayoendelea kukua. Mama Tibaijuka atasaidiwa na Goodluck Ole Madeye.
Mwanasiasa mkongwe Philip Marmo, ambaye alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) hakuwa na nafasi ya kuteuliwa kurejea kwenye nafasi yake baada ya kupigwa kikumbo katika uchaguzi mkuu alipojaribu kutetea kiti cha ubunge Jimbo la Mbulu.
Wizara hiyo sasa itaongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, William Lukuvi ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) katika serikali ya awamu ya tatu ya Rais Benjamin Mkapa.
Marmo amefuata njia inayofanana na ile ya Lawrence Marsha ambaye pia aliangushwa kwenye uchaguzi wa Jimbo la Ilemela na hivyo kukosa nafasi ya kurejea kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani.
Nafasi yake imechukuliwa na Waziri Kiongozi wa zamani wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha ambaye alianguka kwenye kinyang'anyiro cha urais wa visiwa hivyo, lakini akateuliwa na rais kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.Naibu wake atakuwa Khamis Kagasheki.
Wengine walioanguka kwenye uchaguzi ni Shamsa Mwangunga na Dk Batilda Buriani, ambao kila mmoja alianguka kwenye hatua tofauti.
Wakati Mwangunga, ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii alianguka katika kura za maoni ndani ya CCM, Dk Buriani aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), alipigwa mwereka katika uchaguzi mkuu Oktoba 31 alipoangushwa na mgombea wa Chadema kwenye Jimbo la Arusha Mjini.
Kuanguka kwa Mwangunga kumempandisha aliyekuwa naibu wake, Ezekiel Maige ambaye sasa anakuwa waziri kamili wakati nafasi ya unaibu imeondolewa.
Nafasi iliyoshikiliwa na Dk Buriani katika serikali iliyopita, safari hii itashikiliwa na Dk Terezya Luoga Hovisa aliyeteuliwa kuwa miongoni mwa mawaziri wataokamilisha malengo ya mpango wa maendeleo wa milenia wa 2015.
Katika baraza hilo jipya la mawaziri Kikwete pia amemtema, Dk James Wanyancha, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Mawaziri wengine walioanguka kwenye uchaguzi mkuu ni Mwantumu Mahiza, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Joel Bendera, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo.

Chanzo Mwananchi.

Monday, November 22, 2010

HIVI NDIVYO AIRTEL ILIVYOZINDULIWA

Dk. Jakaya Kikwete (katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Airtel, na Viongozi wa Serikali katika Uzinduzi wa huo, uliofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Ambwene Yesaya 'AY' (kulia) akiwa na wadau wake katika uzinduzi wa Airtel.
Masanja wa Orijino Komedi (kulia), akisalimiana na Madam Litta.
Dah! bora nimekuona Mkurugenzi baaana siku zilikuwa nyingi...
Madam akitoka ukumbini hapo.
Hapa Madam alijaribu kuunda Swagger kiaina.
Wafanyakazi wa Airtel katika pozi.
Ali Kiba akikamua na mrembo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Airtel wakiwa kwenye Swagger tofauti.
Warembo waki...
Wafanyakazi wa Airtel...
Mambo hayo...
Beatrice Singano Mallya, akifurahia nyimbo za Ali Kiba.
Oya umecheki Ali anavyokamua eehee......
Paul Mashauri katika pozi.
Ali Kiba akimwaga burudani katikaUzinduzi huo.
Adam Mchomvu akijaribu kuunda Swagger katika uzinduzi huo.
Mafundi mitambo wakiwajibika.
Asha Baraka (kushoto), akibadirishana mawazo na Meneja wa Global Publishers, Abdalla Mrisho.
Ssebo naye alikuwepo.
Banana Zorro (kushoto), akisikilizia jambo kutoka kwa Abdalla Mrisho.
Madam Litta akisalimiana na mmoja wa wageni waliohudhuria uzinduzi huo.
Swagger kama hizi zilichukua nafasi pande hizo.
Beatrce wa Airtel (kushoto), na wageni wake.
Mambo hayo.
Ali Kiba alifurahia kukutana na DK. Kikwete.
Kiba alizidisha furaha kama hivi.
Kiba haamini macho yake baaaanaa kushikana mkono na DK. Kikwete, kwa mara ya kwanza.
AY akiwa na marafiki zake.
Kiba, akimsikiliza kwa makini DK. JK Kikwete.
Haaa! hata wewe ....
DK.Kikwete, akiagana na viongozi wa Airtel.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jorodan (kulia) akijimiminia kilaji na wenzake ukumbini hapo.
Meneja Uhusiano wa Airtel TZ Munganyizi Mutta, akijipatia mlo wa usiku na Maimartha Jesse.
Mkurugenzi wa Clouds TV Ruge (kushoto), akifuatilia mchakato huo.
Mustapha (kulia) akiwa na Paul Mashauri.
Madam Litta na wenzake wakipata msosi mahari hapo.