Social Icons

Tuesday, December 13, 2011

WABONGO WASHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU UGIRIKI

WATANZANIA waishio Ugiriki walisherehekea nchi yao kutimiza miaka 50 ya uhuru kwa shangwe na burudani mbalimbali zilizofanyika katika ofisi ya ubalozi wao katika Mtaa wa Lemesoy jijini Athens. Miongoni mwa matukio ya kuvutia ni sinema iliyoonyesha jinsi wakoloni wa Uingereza walivyokabidhi madaraka kwa viongozi wa nchi siku ya Desemba 9, 1961.

Mdau wetu aliyekuwa huko alihakikisha wateja wa mtandao huu wanapata kwa uhakika kile kilichotokea huko katika picha hapo juu.


0 comments: