Balozi Ngemera (katikati) akiwa na viongozi wa Umoja wa watanzania Ujerumani UTU
kamada ketu Ras Makunja wa FFU alikuwepo
Ras Makunja na mzimu wake wa Ngoma za Afrika band
Washambuliaji wa magitaa wa FFU wakichakaza vitu vyao.
Watanzania waishio Ujerumani hakuna aliye lala nyumbani siku hiyo.
SIKU ya Ujumaa ya 9.12.2011 na jumamosi 10.12.2011 Watanzania waishio Ujerumani na nchi jirani
wakishirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani,walifanikiwa kulitingisha jiji la Berlin "!
katika sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara, sherehe hizo zilizoongozwa na Balozi
Bw.Ngemela na maofisa wa ubalozi akiwemo Bw.Ali Siwa zilianzia katika ukumbi wa Martim
ambako kulikua na mkusanyiko wa mabalozi wa nchi mbali mbali,vingozo wa ngazi za juu wa
serikali ya Ujerumani,watanzania, mashirika NGO's,na marafiki wahisani wa Tanzania walikuapo
kusherekea na kuipongeza Tanzania kwa kufikia miaka 50 ya uhuru kwa amani, Tanzania pia
ilipongezwa na kutajwa kuwa nchi ya Amani barani afrika ambayo wananchi wake wameshikama
kwa amani na upendo.
Ngoma Africa Band aka FFU chini ya uongozi wake Ras makunja aka Kamanda wa FFU,
muziki wa bendi hiyo ulifanaikiwa kuwachanganya uwanjani madipromasia na wadau walioudhuria katika sherehe hizo ijumaa na jumamosi bendi hiyo maarufu inatamba na
CD mpya Shangwe 50 Uhuru anniversary.
Pia sherehe hizo ziliambata na ufunguzi wa chama cha Watanzania ujerumani (UTU) ambacho
kilifunguliwa rasmi siku ya jumamosi 10.12.2011 na Balozi Mhe.Ngemera ambaye pia ndie
aliyetilia mkazo kwa kuanzishwa kwa umoja huo ambao ndio mwavuli wa watanzania wote
waishio Ujerumani,Umoja huo umesajaliwa na serikali ya Ujerumani kama NGO's na mwenyekitiki wake Bw.Mfundo Peter Mfundo.
0 comments:
Post a Comment