Social Icons

Tuesday, December 13, 2011

FRANSIC CHEKA USO KWA USO NA KALAMA NYILAWILA JANUAR 28

MIAMBA ya masumbwi nchini, bingwa wa Mabara Francis Cheka [SMG] na bingwa wa Dunia Karama Nyilawila [Kapten] wanatarajia kupanda ulingoni Januari 28 mwaka huu kuoneshana umwamba. Cheka na Nyilawila hawajawahi kutwangana mpambano ambalo limewafanya mashabiki kuhisi kuwa mabondia hao wanaogopana. Akizungumza Dar es Salaam jana, promota wa pambano hilo Philemon Kyando 'Don King' alisema pambano hilo litapigwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro nyumbani kwa Cheka. Alisema pambano hilo litakuwa la raundi 10 uzito wa kg 72 Alisema kutakuwa na pambano kati ya Maneno Osward [mtambo wa gongo] na Pasco Ndomba raundi nane uziti wa kg 75, Chaulembo Palasa na Deo Njiku kg 68, Venance Mpoji na Ibrahim Clases kg 63, Anthon Mathias na Juma Afande kg 54 na pambano la mwisho kati ya Hassan Kidebe na Arbert Mbena kg 54 ambapo mapambano hayo yatakuwa ya raundi sita kila moja. Promota huyo alisema lengo la kumuandalia pambano Nyilawila na Cheka ni kuondoa uvumi kuwa mabondia hao wanaogopana lakini pia ni kuurudisha mchezo wa ngumi katika chati.
Picha: Full Shangwe Blog

0 comments: