SIKU CHACHE BAADA YA KUACHIWA HURU JERRY MURO AKABIDHIWA TUZO YA MWANDISHI BORA
Akizungumza Jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Kajubi Mkajanga, alisema tuzo hiyo imeambatana na fedha taslimu shilingi milioni 6 na laki mbili na kuwa walishindwa kuitoa mwaka huo kutokana na Mshindi huyo kukabiliwa na kesi ya kuomba Rushwa ya shilingi milioni 10 kutoka kwa aliyekuwa mhasibu wa Wilaya ya Bagamoyo Michael Wange.
Kwa upande wake Mshindi huyo Bwana Jerry Muro , ameishukuru MCT, na kuwataka waandishi wa habari kushirikiana na kutokata tamaa pindi wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali katika majukumu yao.
Picha: Habari na Matukio Blog
Picha: Habari na Matukio Blog
0 comments:
Post a Comment