Social Icons

Saturday, December 3, 2011

FALLY IPUPA APAGAWISHA USIKU WA KIAFRIKA DAR !

Fally akinengua na mrembo jukwaani.
Fally Ipupa akiwajibika jukwaani hapo.
… akiserebuka na mrembo mwingine.
… akiserebuka na mrembo mwingine.
: Baadhi ya wanamuziki wa Fally Ipupa
: Msanii wa filamu Bongo, Steven Kanumba ‘akizama’ ukumbini hapo.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Ali Kiba (kulia), akikamua katika shoo hiyo na Dully Sykes.


Mmoja wa wasanii waliotumbuiza ukumbini hapo akionyesha mazingaombwe, na hapa akiwa amemlaza hewani mwenzake aliemtia usingizi na kupaki akiwa ameegemea kichwa tu.
Msanii huyo akionyesha kumlaza mwenzake kwenye viti.
: … akiwa amemlaza katika ubao uliokuwa juu ya viti kabla ya kuvitoa.

Wasanii wa sarakasi wakionyesha uwezo wao.


Kuwa hivi yanahitajika mazoezi ya nguvu.


Fally Ipupa akimkokota mrembo kumuondoa stejini hapo.


Mboni Masimba (kushoto) na rafikiye wakipiga makofi.


Kanumba akiwa katika pozi na mrembo.



Baadhi ya mashabiki wakiofrika ukumbini hapo wakifuatilia shoo hiyo.

MSANII wa muziki wa Dansi kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Fally Ipupa, usiku wa kuamkia leo amepagawisha vilivyo katika Tamasha maalum la Usiku wa Kiafrika lililokuwa limeandaliwa na Club E ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, huku akisindikizwa na Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba na Bendi ya THT.

Tamasha hilo lilikuwa hususani kwa kuonyesha uafrika zaida ambapo baadhi ya vitu vilivyokuwa vikionyeshwa ukumbini hapo ni pamoja na mavazi ya kiasili ya mwafrika na michezo mbalimbali yenye tamaduni ya Kiafrika.



0 comments: