Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye foleni ya mafuta katika Kituo cha Mafuta cha Bamaga, Mwenge jijini.
SAKATA la kuadimika kwa nishati ya mafuta nchini limeibuka tena leo, ambapo wakazi wa jiji la
Tatizo
Baadhi ya wateja wa nishati ya mafuta ya petroli na dizeli leo wamelalamikia utaratibu wa vituo vya mafuta kuendelea kugoma kuwauzima nishati hiyo kwa madai ya kwisha katika vituo vyao.
“Inanikela sana hali ni mbaya maana nimetafuta mafuta tangu asubuhi sijapata, na nikiangalia sababu hata sielewi, nini kinachowafanya Ewura kutosema tatizo kwetu wateja wao ili tusisumbuke?” alihoji mkazi mmoja huku mwingine naye akilalamika kuwa:
“ Hawa Ewura hawafai kabisa, yaani leo wamenifanya kutoenda kazini kwa ajili ya kuhangaika huku na kule kutafuta mafuta, huwezi kuamini, gari limenizimikia Sinza Mugabe na sasa niko hapa kituo cha mafuta Bamaga tangu saa tatu asubuhi na mafuta sijapata, wauzaji wanatuyeyusha tu.” Alisema mkazi huyo.
: Jamaa huyu anaonekana akilalamika akiwa kwenye foleni hiyo.
Baadhi ya madumu ya kuchukulia mafuta yakiwa yamepangwa kwenye foleni na wateja, tayari kwa kutiwa mafuta iwapo yatapati.
Magari yakiwa kwenye msululu wa kugoja kujaziwa mafuta.
0 comments:
Post a Comment