Social Icons

Monday, December 19, 2011

XXL AFTA SKUI BASHA 2011 IMETISHA!!!

Msanii wa muziki wa kizazi Kipya Bongo, Shetta akitumbuiza jukwaani.


MPANGO mzima jana ulikuwa ndani ya Tamasha la XXL Afta Skui Bash 2011, lililofanyika katika Ufukwe wa Mbalamwezi Mikocheni, Dar es Salaam ambapo umati ulijitokeza kujumuika katika kufanikisha sherehe za likizo ya masomo kwa mwaka huu.

Tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka na kuandaliwa na Kampuni ya Clouds Media Group kupitia kipindi cha XXL, lilifana vilivyo huku wasanii kibao wakali wakishambulia jukwaa vilivyo.

Baadhi ya wasanii walikonga mioyo ya mashabiki ni Godzilla, Young Dee, AT, Ommy Dimpoz, Bob Junior, Linex, Ditto, Mataluma, Hemedy Suleiman, Stamina, Shetta, Amini, Makomandoo, THT Dances na chipukizi kibao.

Katika tamasha hilo, pia kulifanyika michezo mbalimbali kama mashindano ya kucheza muziki, urembo, kufananisha sura na staa na kumatafuta Mr & Miss XXL 2011.


Bob Junior na Nuru wakiimba kwa pamoja wimbo wao wa Muhogo.

Msanii kutoka THT, Amini Mwinyimkuu akifanya makamuzi.


Baadhi ya wanenguaji wa THT wakikamua stejini.


Godzila alipoteza ajabu.


Mr XXL 2011, Sospeter Elias (kushoto), akiwa katika pozi na Miss XXL, Rahmada Baga muda mfupi baada ya kutangazwa washindi.


Warembo hao wakishindana kusakata rhumba mahali hapo.


Wasanii wanawakilisha kundi la Makomandoo wakiwajibika mari hapo.


DJ Choka (kulia), akiwa katika pozi na vijana wanaomiliki mtandao wa G5CLICK kwenye fukwe hizo.


Young Dee akikamua kwa staili yake.
Young Dee akicheza na jukwaa namna hii.

Msanii wa Top Band, Ommy Dimpoz akitumbuiza kwa hisia kali huku akiwa amemkamatia mbwa wake jukwaani hapo.


Mtangazaji machachari wa Kipindi cha XXL Cha Clouds FM, Hamis Mandi ‘B12’ akisherehesha tamasha hilo.


Msanii kutoka THT, Mataluma akionyesha uwezo wake.


Watangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu (kushoto), Fatuma Hassan ‘DJ Fety, na Ruben Ndege ‘Ncha Kali’ wakishindana kuchana jukwaani hapo.


DJ Zirro wa Clouds FM, akisongesha burudani hizo.


Mmoja wa mashabiki waliohudhulia tamasha hilo akijinafasi mbele ya umati baada ya kupewa nafasi ya kuonyesha uwezo wake.


Baadhi ya mashabiki waliofurika mahali hapo.

0 comments: