Chialo akiwaonyesha wandishi wa habari madawa hayo.
Sehemu ya madawa yakiwa kwenye gari.
JESHI la polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kukutwa na madawa ya kulevya.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo asubuhi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolph Chialo, alisema mwanajeshi huyo mwenye namba MT 86879, Milolo Elumbe (26) wa kikosi cha 34 Lugalo jijini Dar es Salaam akiwa na sare za jeshi hilo, alikamatwa na askari waliokuwa doria akiwa na magunia 12 ya madawa ya kulevya aina ya bangi eneo la Tumbaku barabara kuu ya Morogoro-lringa.
"Mwanjeshi huyo akiwa na wenzake wawili, Ally Mustapha (26) na ldd Said (30) ambao ni wakazi wa jijini Dar es Salaam kwa pamoja walikitwa na magunia hayo ya bangi eneo la Tumbaku wakiisafirlishwa kuelekea jijini Dar es salaam kwa kutumia gari aina ya Toyota Mark ll yenye namba za usajili T 602 ABJ na wakati wowote watuhumiwa hao watafikishwa mahakami kujibu shitaka linalowakabili," alisema bosi huyo wa polisi.
Gari lililotumika kusafirishia madawa hayo.
0 comments:
Post a Comment